Wapo wanawake wanaotongoza wanaume na bado ni waaminifu ukiachana na vicheche wanaojigonga kwa pesa/umaarufu?

Wapo wanawake wanaotongoza wanaume na bado ni waaminifu ukiachana na vicheche wanaojigonga kwa pesa/umaarufu?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
katika kuelezea hisia za mapenzi, sio lazima kila siku mwanaume tuu ndio awe mwanzilishi wa kusema hisia zake kwa mwanawake, kuna kipindi mwanamke anaweza kufunguka.

achana na vicheche kadhaa vinavyokomalia watu vyenye mapenzi ya mikwanja, majina na umaarufu
ambavyo ukiwa chata tu vinajigonga.

Je kuna wanawake wanaotongoza kwa nia ya dhati kabisa ya penzi na ni waaminifu?
 
Sio zama hizi mkuu!
Ukifatilia vizuri haya mambo ya wanawake kujiongeza kwenye kuelezea hisia zao yameanza siku hizi, zamani ilikuwa mwiko.

Sasa ndio nawaza hapa katika huu mfumo mpya kama wapo wenye kuaminika bila kuwa na ajenda za pembeni.
 
Mwanamke mwenye maadili kukutongoza ni ishu, yeye ni matendo tu yatakufanya uelewe. Vile vile anakuheshimu na kukusikiliza pia.

Ukiona demu anakutongoza mwambiye 'ntakupa jibu'.

Halafu hawa wengine! 🙌
Kwanza ni wasumbufu, umemwambia haupo home ye anakuja tu! 😁
 
hapo kuna kosa lipi mkuu, kama kakufata wewe kama wewe ni kwamba amekumisi.
Kosa ni kutokuwa msikivu. Kunimiss isiwe taabu mpaka ayazime masikio yake.

Sisi kama binadamu unaweza amka unamambo yako binafsi unatakiwa uyatatue/uyamalize ukiwa pekeyako bila miingiliano. Na unakuta ni ya muhimu, so hunabudi kumzuia hata yeye kulingana na unavomjua.

Kuna mabinti/Wanawake ni watulivu unaweza kaa naye wakati unaendelea na shughuli zako, lakini kunawengine ni kero!
 
Chamsingi hakikisha anayekutongoza hajakuzidi shida. Unaweza dhani kakupenda kumbe mwenzako anatafuta sponsor
Mimi yule alimaanisha toka moyoni.
Sema nami sikumwelewa tu lkn daah niishie hapa
 
katika kuelezea hisia za mapenzi, sio lazima kila siku mwanaume tuu ndio awe mwanzilishi wa kusema hisia zake kwa mwanawake, kuna kipindi mwanamke anaweza kufunguka.

achana na vicheche kadhaa vinavyokomalia watu vyenye mapenzi ya mikwanja, majina na umaarufu
ambavyo ukiwa chata tu vinajigonga.

Je kuna wanawake wanaotongoza kwa nia ya dhati kabisa ya penzi na ni waaminifu ?
Siku hizi Wana Uhuru wa kueleza hisia zao,zamani walikuwa "jela"

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Write your reply...Ukiona mwanamke amekuja kukutongoza jua Kuna kitu kakiona kwako tofauti na Mapenzi yenywewe, especially Hawa wanawake wa ckuiz Ni masnitch Sana.
 
Back
Top Bottom