Waraka kwa Rais Samia kuhusu vilio vyetu sisi Wahandisi tulioajiriwa kama Walimu

Waraka kwa Rais Samia kuhusu vilio vyetu sisi Wahandisi tulioajiriwa kama Walimu

Shemeji yangu ndo kamaliza sheria,alisota mtaani anajitolea kwenye makampuni bila malipo juzi kuna jamaa kamwambia atamfanyia connection kwenye kampuni moja kuuza bidhaa atalipwa laki tatu,ninavoongea shemeji yupo kwenye maombi angalau apate hiyo kazi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nyie watu jaman khaaaaaah
 
Pole sn wachapakazi wa Taifa. Baada ya pole niseme tu kuwa nyie sio Walimu ktaaluma. Kuwa Mwalimu kitaaluma Kuna kozi zake lazima uzisome km mtaala wa elimu unavyoelekeza. Kwa kutokujua hili ndio maana Kila mtu amekuwa akichukulia hawa ndungu zetu Walimu km watu wa chini na kuwabeza kumbe sio kweli bali ni ukosefu wa elimu kwa watu walio wengi.

Ndio maana huwezi kusoma sheria, habari na utangazaji, maendeleo ya jamii nk ukawa Mwalimu bila kusoma kozi zinazohusiana na ualimu. Hata uwe na PhD huwezi kuajiliwa ualimu.

Tukumbuke kuwa si Kila mtu anaweza kuwa Mwalimu kwa taaluma hata km umesoma vyuo vyote Duniani umemaliza huwezi kuwa Mwalimu hadi usomee kozi za ualimu kwa taaluma. Kuna wachungaji, wafundaji, waelimishaji jamii juu ya jambo flani, Walimu wa madrasa, hawa wote ni Walimu lakini siyo Walimu kitaaluma.

Unakumbuka programme ya huko nyuma ambayo watu waliajiliwa baada ya kusoma vyuo vya ualimu muda wa miezi 3/6 a.k.a voda faster(watu waliwaita hivyo). Hawa mbali na kupata elimu kidogo ya ualimu lakini serikali iliwaamuru wafikapo kazini wahakikishe wanajiendeleza ili kupata Diploma/degrees za ualimu kwa taaluma ndani ya miaka 2 tangu kuajiliwa. Unajua kwa nini serikalini iliweka huo utaratibu. Jibu ni kuwa hao walikuwa hawajawa Walimu kamili na mahili (complete and competent professional teachers).

Serikali iliaamua kuwaajili kipindi hicho kutokana na uhaba wa Walimu shuleni hasa elimu sekondari ambako shule nyingi za kata zilifunguliwa pasipo kuangalia mahitaji ya idadi ya walimu.

Hata nyie serikali iliona Kuna uhaba wa Walimu wa shule za ufundi ikaamua kutumia utaratibu wa huko nyuma wa voda faster ili kutatua hii changamoto, kwamba yeyote aliehitimu uhandisi (engineering) aombe ualimu. Ila ukweli unabaki kuwa huwezi kuwa Mwalimu kwa taaluma km wewe hujasomea ualimu. Mwalimu yeyote awe wa msingi, sekondari, cheti, diploma, au chuo kikuu lazima kasomea kozi za ualimu. Ndio maana laboratory technicians wa sekondari sio Walimu maana hawajasomea kozi za ualimu, wao wanabaki tu km wataalamu wa maabara, sio Walimu kwa taaluma.


Mwisho, nyie nendeni mkasomee kozi za ualimu kitaaluma vinginevyo hamtathibitishwa kazini. Na hilo litakuwa ni balaa kwenu kwani mtakuwa mnafanya kazi lakini kwenye Data base ya waajiliwa serikalini hampo na ukipata tatizo lolote kazini au la kifamilia mtapata tabu. Hata mikopo Bank hamuwezi kupewa maana nyie sio waajiliwa (najua hili ndo limekufanya ulete Uzi hapa jf). Kwa lugha nyingine bado majina yenu yameandikwa kwa chaki muda wowote yatafutika (am just kidding). Km hamtaki kujiendeleza acheni kazi mkasubiri hizo zenu mlizosomea za uinjinia.
Upo sahihi kabisa, na kwa taarifa tu ni kwamba wale jamaa wa Voda fasta alipoingia Magufuli aliwafukuza kazi wote ambao hawakwenda vyuo vya Ualimu kusomea taaluma ya Ualimu.

Waliobaki makazini ni wale tu ambao walijiongeza kwenda kusoma ama Diploma au Degree za Ualimu.

Na hawa wahandisi isije ikawakuta zahama hiyo!!
 
Back
Top Bottom