WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

Daah nafarijika sana na hizi nyaraka za kitume kutoka kwa viongozi wetu wa kiimani, hakika wabarikiwe sana maana ni mwanzo mzuri wa serikali kujitafakari muenendo wake kwa watu wake
 
"Kisiasa Kikatiba, nchi yetu inafuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Katiba na Sheria mbalimbali zimeainisha utaratibu wa kazi na shughuli za vyama vya siasa. Ili kuhakikisha kwamba kazi na shughuli za vyama vya siasa zinakuwa endelevu, vyama vyenye kukidhi vigezo hupewa ruzuku kupitia Bajeti ya Serikali inayopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania. Hata hivyo, shughuli za siasa bado zinaendelea kuzuiwa kwa kutumia vyombo vya dola. Maana yake ni kwamba shughuli za kiuenezi za vyama vya siasa, kama vile mikutano ya hadhara, maandamano, makongamano, mijadala na hata mikutano ya ndani, ambayo ni haki ya kila raia, zimekoma mpaka uchaguzi mwingine. Kisheria, huu ni uvunjifu wa Katiba na Sheria za nchi.

Vile vile baadhi ya vyombo vya habari vimefungiwa au kusimamishwa kwa muda, na hivyo kupunguza uwigo wa uhuru wa wananchi wa kupata habari, maoni na wa kujieleza. Kufungiwa huku kwa vyombo vya habari kumeenda sambamba na kuminya uhuru wa Mahakama na Bunge kwa njia ya kuminya haki ya wabunge na kutowapa nafasi ya mikutano ya hadhara kama haki yao ya msingi ya Kikatiba. Katika mazingira haya ni rahisi kwa jamii kufarakana na hata kujenga chuki kiasi cha kuhatarisha amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu. Kumekuwapo pia hali ya vurugu katika chaguzi mbalimbali. Chaguzi hizi zinaacha nyuma uchungu, hasira, tamaa ya kulipa kisasi na hata kususia chaguzi nyingine. Hali hii ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu. Tukiiachia hali hii izoeleke tushishangae huko mbeleni kujikuta katika mifarakano mikubwa zaidi itakayobomoa misingi ya amani na umoja wa kitaifa"
Mwisho wa kunukuu

CC: JIWE
 
Hili swali sijui kwa nini walilichagua "Je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? " Hili swali aliliuliza Kaini kwa Mungu baada ya Mungu kumuuliza Kaini alipo Abel nduguye, ilikuwa ni baada ya Kaini kumuua ndugu yake, Abel.
 
Sijasoma....

Ila nchi hii kuna tatizo pahala...

Wale wanaomuwekeaga mikono na kumuombea ni kina nani.

!??

I'll be back at 20th page.
Hakuna watu wanaFki kama wakristo hasa
linapokuja swala la watawala
 
Mara baada ya habari ITV leo wakaweka 'wosia wa Baba wa Taifa. Na ujumbe wa leo ulikuwa "Mtu yeyote ambaye haijali katiba aliyoapa kuilinda HATUFAI".

Viogozi wetu wa kiroho tunashukuru sana kwa kutusemea sisi wanyonge, Taifa letu linaelekea shimoni. Ni lazima tusimame na tuseme HATUFAI. Tunagoja maaskofu wa makanisa ya Pentekoste nanyi simameni mseme ili mhesabiwe. Tunangojea mashehe wa kiislamu wajitokeze nao waseme HATUFAI.

Tarehe 26/4 sijui itakuwaje.
 
Pengo kama kiongozi pekee mwenye hadhi ya kumchagua Papa Tanzania ameupinga waraka huo, asikilizwe na kuheshimiwa!
 
Mwenye kuwanao na ule wa KKKT afanye kuunganishia hapo ili niwe naisoma kwa pamoja kila siku ninapoamka asubuhi na usiku kabla ya kwenda kulala.
 
Inasikitisha sana kwakweli namna viongozi wetu wa dini wanavyotia bidii Katika kuharibu taswira za makanisa yetu.

Sasa kuna mstari mdogo sana unaotenganisha makanisa na vyama vya siasa.
 
nimeona jina la pengo hapo
kesho atakataa kuhusika na huu waraka
 
Viongoz wa Dini ni mawakala wa Mwenyez Mungu ktk kuwaongoa wanadam na kuwatia nguvu ktk mapambano dhidi ya shetani na matendo yake maovu, ni wajibu wa viongoz wa dini kuikemea serikali hii ambayo imekuwa/inaelekea kuwa na characteristics za kishetani.
 
Inasikitisha sana kwakweli namna viongozi wetu wa dini wanavyotia bidii Katika kuharibu taswira za makanisa yetu.

Sasa kuna mstari mdogo sana unaotenganisha makanisa na vyama vya siasa.
kila mtu anawapinga
kuna tatizo mahali ila ni wagumu kukubali
 
Vipi katika matamko yote hayo kuna mahali wamegusia mashehe wetu wa uamsho??
 
Inasikitisha sana kwakweli namna viongozi wetu wa dini wanavyotia bidii Katika kuharibu taswira za makanisa yetu.

Sasa kuna mstari mdogo sana unaotenganisha makanisa na vyama vya siasa.
Alaumiwe Lowassa kwa kuandaa ile MoU!
 

mathayo daniel

Member

#9
22 minutes ago

Joined: Jan 23, 2018
Messages: 35
Likes Received: 6
Trophy Points: 15

Maaskofu wamesababisha ujiunge JF au uanzishe ID mpya sambamba na ya zamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…