Alex Fredrick
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 697
- 1,358
Awali ya yote natumai umzima wa Afya popote ulipo Rais pia nikupe pole Kwa majukumu ya kulitumikia Taifa hili letu pendwa ambalo lina changamoto lukuki!
Rais naomba niende moja Kwa moja kwenye hoja ambayo imezua maswali pasi na majibu siku mbili hizi juu ya mjadala "Tata' kuhusu Serikali yetu kuingia ubia na DP World kutoka Dubai kupitia Bandari yetu ya Dar es salaam.
Rais "Taharuki' imekuwa kubwa juu ya mjadala huu, naomba uitishe mjadala wa Kitaifa wananchi tupate kujua ukweli wote ndo huo mchakato Uende Bungeni.
Hakuna mtu yoyote yule ambae anapinga uwekezaji au Ubia, Kinachopingwa na ambacho kimezua maswali ni jinsi mchakato unayoenda pasi na kuwa na majibu toshelezi Kwa wananchi wako.
Rai yangu kwako Rais Sisi Watanzania tunaitaji kusikia kauli kutoka kwako Zaidi tukae Kama Taifa kujua mchakato wote Kwa uwazi ndio upelekwe Bungeni.
Chonde chonde Rais kataa au kuwa Makini na wanao kushauri Kwa Nia "Ovu 'ili kuleta kilio Kwa Uwekezaji wa hovyo ambao utakuwa kilio Kwa vizazi vijavyo ambavyo navyo vinastahili kuja kufaidi hii Keki ya Taifa.
Natambua pasi na Shaka wewe Rais Samia ni mtu msikivu na mwenye busara kwahiyo wananchi wanaitaji Uwazi kuhusu huu Uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam kuondoa sintofahamu iliyopo sasa.
Asante
Alex Fredrick
+255 655 308494