Waraka Mfupi Kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
697
Reaction score
1,358
Awali ya yote natumai umzima wa Afya popote ulipo Rais pia nikupe pole Kwa majukumu ya kulitumikia Taifa hili letu pendwa ambalo lina changamoto lukuki!

Rais naomba niende moja Kwa moja kwenye hoja ambayo imezua maswali pasi na majibu siku mbili hizi juu ya mjadala "Tata' kuhusu Serikali yetu kuingia ubia na DP World kutoka Dubai kupitia Bandari yetu ya Dar es salaam.

Rais "Taharuki' imekuwa kubwa juu ya mjadala huu, naomba uitishe mjadala wa Kitaifa wananchi tupate kujua ukweli wote ndo huo mchakato Uende Bungeni.

Hakuna mtu yoyote yule ambae anapinga uwekezaji au Ubia, Kinachopingwa na ambacho kimezua maswali ni jinsi mchakato unayoenda pasi na kuwa na majibu toshelezi Kwa wananchi wako.

Rai yangu kwako Rais Sisi Watanzania tunaitaji kusikia kauli kutoka kwako Zaidi tukae Kama Taifa kujua mchakato wote Kwa uwazi ndio upelekwe Bungeni.

Chonde chonde Rais kataa au kuwa Makini na wanao kushauri Kwa Nia "Ovu 'ili kuleta kilio Kwa Uwekezaji wa hovyo ambao utakuwa kilio Kwa vizazi vijavyo ambavyo navyo vinastahili kuja kufaidi hii Keki ya Taifa.

Natambua pasi na Shaka wewe Rais Samia ni mtu msikivu na mwenye busara kwahiyo wananchi wanaitaji Uwazi kuhusu huu Uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam kuondoa sintofahamu iliyopo sasa.

Asante

Alex Fredrick
+255 655 308494
 
Huu ushauri hauna maana. Walishasaini IGA, ukihitaji Sana m mjadala ndio utazidi kuongopewa
 
Imani yangu ni kwamba Sa100 huwa anaingizwa chaka sana na wasaidizi wake wa karibu, ni kama vile wana take advantage fulani hv ya mapungufu ya boss wao ambayo wameshayagundua.

Hii ni tofauti kdg na enzi za JPM ambapo kwakuwa alikuwa anaogopwa sn kwa ukali wake wasaidizi kama walimdanganya ni kwa kiasi kdg makosa kama yalitokea yalitokea kwa sabb ya ujeuri/ubabe wake.

Mh Rais inabidi awe mkali hasa kwa wazembe na wezi...yaani mijitu inatuibia kodi zetu we unayaita stupid halafu?
 
Heri nusu Shari kuliko Shari kamili bado tuna muda wa kujadili Kama Taifa
 
Tatizo nchi hii tunashindwa karibia kila kitu. Tunachoweza kwa asilimia kubwa ni majungu, porojo, unafiki, na udokozi.

Kilimo tunashindwa, madini tunashindwa, utalii tunashindwa, upangaji wa miji tunashindwa, kutambua vipaumbele tunashindwa, utawala bora tunashindwa, tekinolojia ndiyo zero, upangaji wa mipango ya uchumi na maendeleo tunashindwa, demokrasia tunashindwa; halafu umaamini tutaweza kwenye bandari pekee yake?

Ndiyo maana tunasema kuwa rasiliamali kubwa kwa mwanadamu ni akili. Ukinyimwa tu akili,umenyimwa vyote vilivyo vya thamani.
 
Awali ya yote natumai umzima wa Afya popote ulipo Rais pia nikupe pole Kwa majukumu ya kulitumikia Taifa hili letu pendwa ambalo lina changamoto lukuki!

Rais naomba niende moja Kwa moja kwenye hoja ambayo imezua maswali pasi na majibu siku mbili hizi juu ya mjadala "Tata' kuhusu Serikali yetu kuingia ubia na DP World kutoka Dubai kupitia Bandari yetu ya Dar es salaam.

Rais "Taharuki' imekuwa kubwa juu ya mjadala huu, naomba uitishe mjadala wa Kitaifa wananchi tupate kujua ukweli wote ndo huo mchakato Uende Bungeni.

Hakuna mtu yoyote yule ambae anapinga uwekezaji au Ubia, Kinachopingwa na ambacho kimezua maswali ni jinsi mchakato unayoenda pasi na kuwa na majibu toshelezi Kwa wananchi wako.

Rai yangu kwako Rais Sisi Watanzania tunaitaji kusikia kauli kutoka kwako Zaidi tukae Kama Taifa kujua mchakato wote Kwa uwazi ndio upelekwe Bungeni.

Chonde chonde Rais kataa au kuwa Makini na wanao kushauri Kwa Nia "Ovu 'ili kuleta kilio Kwa Uwekezaji wa hovyo ambao utakuwa kilio Kwa vizazi vijavyo ambavyo navyo vinastahili kuja kufaidi hii Keki ya Taifa.

Natambua pasi na Shaka wewe Rais Samia ni mtu msikivu na mwenye busara kwahiyo wananchi wanaitaji Uwazi kuhusu huu Uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam kuondoa sintofahamu iliyopo sasa.

Asante

Alex Fredrick
+255 655 308494
Unashauri nini Mkuu wakati watu washalamba asali,Bunge linageuzwa Rubber-stamp kupitisha mambo yao.
Screenshot_20230607_112705.jpg
Screenshot_20230607_112631.jpg
 
Imani yangu ni kwamba Sa100 huwa anaingizwa chaka sana na wasaidizi wake wa karibu, ni kama vile wana take advantage fulani hv ya mapungufu ya boss wao ambayo wameshayagundua.

Hii ni tofauti kdg na enzi za JPM ambapo kwakuwa alikuwa anaogopwa sn kwa ukali wake wasaidizi kama walimdanganya ni kwa kiasi kdg makosa kama yalitokea yalitokea kwa sabb ya ujeuri/ubabe wake.

Mh Rais inabidi awe mkali hasa kwa wazembe na wezi...yaani mijitu inatuibia kodi zetu we unayaita stupid halafu?
Haingizwi chaka anafahamu vizuri sana maana hata siku hizi anachelewa kupumzika kutokana na kupitia taarifa na mafaili kadhaa kwa hiyo sio kweli hafahamu manyanga yanayojitokeza kuhusiana na maslahi na usalama wa nchi
 
Chonde chonde Rais kataa au kuwa Makini na wanao kushauri Kwa Nia "Ovu 'ili kuleta kilio Kwa Uwekezaji wa hovyo ambao utakuwa kilio Kwa vizazi vijavyo ambavyo navyo vinastahili kuja kufaidi hii Keki ya Taifa.
Vilio kwa vizazi vijavyo haviwezi kuwepo kwa sababu Hata hivyo vya Sasa na vijavyo haviwezi kukubali maamuzi ya washauri wenye Nia OVU.

Na huyo mwekezaji ambaye atakubali kushiriki Nia OVU ajue anajitapeli. Maana hatakubalika kufanyabiashara yenye vigezo vyote vya Nia ovu.

Kwa kumsaidia huyo mwekezaji aambiwe ukweli kuwa kama atalazimisha kupitisha uwekezaji wake nchini wakati Kuna viashiria vya Nia ovu ajue anajitapeli yeye na wenzake na familia yake.

Usiwe na wasiwasi, Mkuu.
 
Mama kila kukicha yuko kwenye sherehe na maazimisho atasoma sangapi haya mambo mazito. ..Isitoshe akimaliza tu mda wake anaenda kwa wajomba zake Omani.
 
Kwa sasa hakuna jambo linalomtia doa Mama kama mkataba wa DP World. Ukiwa kwenye mikusanyiko ya watu, kwenye vyombo vya usafiri, vijiweni nk. hukosi kusikia watu wakijadili suala, tena wanajadili NEGATIVELY.

Nadhani mpaka sasa kukubalika kwa Mama kunaweza kuwa kumeshuka kwa zaidi ya 75%.

Ushauri wangu ni kwamba, kama hakuna cha pekee sana, Mama afanye maamuzi magumu ya kuachana na hii kitu.
 
Shida mlungula ushaliwa, watarudishaje fadhila, ila zitawatokea Puani. Just wait TZ ya Sasa sio Ile yamiaka 20 iliyopita.
 
Kwa sasa hakuna jambo linalomtia doa Mama kama mkataba wa DP World. Ukiwa kwenye mikusanyiko ya watu, kwenye vyombo vya usafiri, vijiweni nk. hukosi kusikia watu wakijadili suala, tena wanajadili NEGATIVELY.

Nadhani mpaka sasa kukubalika kwa Mama kunaweza kuwa kumeshuka kwa zaidi ya 75%.

Ushauri wangu ni kwamba, kama hakuna cha pekee sana, Mama afanye maamuzi magumu ya kuachana na hii kitu.
Mpaka anaombewa madua mabaya. Machozi ya wengi ni moto usiozimika
 
Back
Top Bottom