Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Naona mmehamia kwa Mwita sasa,hivi nyie pesa zenu hizo si bora hata mkasome walau muwe na ufahamu wa kupambanua mambo?
 
Mkuu bado Mwita Maranya hujue huyu Waitara alikuwa mwiba kwa John Heche kule Tarime.

Ritz wewe mmanyema wa mtaa wa kipata, gerezani Kariakoo unapata shida kuandika Kiswahili huoni aibu japo kidogo?

Hakuna kitu kinaitwa "hujue" hapo ulitakiwa kuandika "ujue".

Usipende kukaa kwenye vijiwe vya gahawa bila kujifunza kitu kipya, matokeo yake unabaki kuwa poyoyo kila kukicha.
 
Last edited by a moderator:
Huo waraka ulipelekwa kwenye vikao vya chama ili wanachama waujadili?
Huo waraka ulikuwa wa ushindi,within chadema.Ni kama vile Hilary v/s Obama.sasa waupeleke kwenye kamati wa nini?Waraka wa kamati ni ule amabao ungeandaliwa ili kuikabili CCM 2015.Hebu muwe waelewa basi
 
Ila wakuu Mwita ni bonge la 'snitch', namkumbuka tangu Azania, jamaa ni msaliti mbaya!
 
Mkuu, sidhani kama matakwa ya hawa jamaa yako nje ya katiba ya chama. Kama katiba ya chama inasema mwenyekiti atachaguliwa kila baada ya miaka 5 haimaanishi kuwa wafate kama vyama vingine vinavyofanya. Katiba ndio muongozo na lazima ifatwe na kama waliiandika wenyewe kwa kukubaliana iweje mtu mmoja aje kutumia mabavu na kufanya kama chama ni chake?

Embu tafakari halafu urudi kimya kimya bila kelele. Kinyume na hapo nadhani utakuwa ni shabiki wa chama na sio hoja zilizotolewa.

Kama CDM hawafuati katiba yao, is ndio kete nzuri kwa CCM? Kwasababu definately itakufa ambalo ndilo ombi la kila asubuhi, mchana na usiku la CCM. Sasa Nyie Magamba, mnaumizwa na kitu gani? Jiti akalie mwenzio, miuona ukatike wewe. Wanafiq wakubwa nyie!
 
We sixgates anza kupaki kenge wewe.
Mlizoea kuburuza vyama vya upinzani kama CUF, TLP ,NCCR hapa ni ngoma nzita anza kupaki ---- wewe.

Chadema si ndio kinaburuza wanachama. Namuonea huruma sana mohamed mtoi, ana uwezo ana akili ila nafasi yake kapewa Tumaini Makene hyu anachojua ni kupiga picha na tablet yake haji kutupa new feeds. Sasa ivi joh heche kamfanyia fitna mwaikabe. Chadema kwa kuuwa vipaji hamjambo.
 
Last edited by a moderator:
Labda wewe ndei huelewi. Kwani Katiba ya CDM ina kipengele kisemacho mtu haruhusiwi kugombea zaidi ya mara 2. Na hata km basi katiba inasema kuwa uchaguzi ufanyike kila baada ya miaka 5 ni haki Zitto kutengeneza Kikundi ndani ya Chama!? Je huko sio ndiko tunakotafsiri kua ni kukigawa chama makundi?
Kwanini asisubiri hadi muda wa uchaguzi ufike na agombee na km akizuiwa kugombea ndipo alalamike?

Na vipi kuhusu katiba ya CCM haisemi uchaguzi uwe unafanyika kila baada ya miaka mingapi? Na km inasema je ni lini CCM iliwahi kufanya uchaguzi wa mwenyekiti wa Taifa?
Na je mbona Ccm wanarithishana kile cheo cha Mwenyekiti au Demokrasia inatakiwa tu ionekane Cdm lakini kwa wengine hapana?

Mkuu, ukiwa unajenga nyumba yako unakopi ya jirani au unaangalia matakwa yako na bajeti uliyonayo?
Kuna tatizo kubwa naliona ambalo ni hatari sana. Msifanye vitu kwa kuwa CCM wanafanya.
Naona katika utetezi wako umeainisha mambo ya CCM. Kwani CCM ndo inayo run CDM?
Au utakuwa unaishi kwa kuangalia jirani yako anafanyaje na we ndio ukopi?
Ningekuelewa vizuri sana kama ungeleta vipengele hapa na tubishane kihoja zaidi kuliko kuweka vitu in comparison.
Kumbuka, hapa kinachojengwa ni CDM na sio CCM. Unless uwe ni double minded man ndo ntakuelewa.
Rudi tena mdau nakusubiri.
Punguza jazba. Twende taratiiibuuuuu
 
Chadema si ndio kinaburuza wanachama. Namuonea huruma sana mohamed mtoi, ana uwezo ana akili ila nafasi yake kapewa Tumaini Makene hyu anachojua ni kupiga picha na tablet yake haji kutupa new feeds. Sasa ivi joh heche kamfanyia fitna mwaikabe. Chadema kwa kuuwa vipaji hamjambo.
Elezea makundi ndani ya chama chenu cha mapinduzi acha na CDM kama ulivyotamka hapo mwanzo
 
kweli mwalimu wangu Kitila Mkumbo umewehuka!? matusi haya kwa mbowe na slaa ndio demakrasia unayosema unaipigania!? Hats darasani sitakuamini tena mwalimu wangu your too low. fahamu wazi wanafunzi wako tunakudharau
 
Last edited by a moderator:
Kugombea ubunge kwenye kura za maoni ndani ya chama ni kitu kingine, kwasababu hayuko mwenyewe. Wapo makamanda kibao akiwepo John Heche.

Hapa tunataka M2 ajisalimishe mwenyewe kabla hajatolewa kama nyoka

Kamanda Mungi huwa sikupingi hata siku moja. Ni kweli kuwa kugombea ubunge ndani ya Chama ni jambo kingine ila nilimuhusisha Waitara na hili la kugombea ubunge na huu Usaliti wanaoufanya ndani ya chama kwa kuwa km kweli yeye ni Mwana chadema "Mwaminifu"na anaetarajia kuja kuwa mgombea wa ubunge kwa kupitia Cdm, ni Chadema ipi hiyo wakati wanakipasua?

Unajua Bwana Mungi, watu au Wasaliti hawa sio tu lengo lao ni kuwa viongozi wakuu wa CDM bali pia ni Kukiuwa ili kufanikisha malengo ya waliowatuma.
Sasa najiuliza ikiwa Cdm kitakufa huku wao wakitamani kuwa viongozi je wataongoza nini sasa!?

Ndio maana nimemtaja Waitara na kuhusika kwake ktk huo Mkakati wa MM2013 huku yeye akiwa ni M2! Na anaetaka kuwa Mbunge atakuwa mbunge kivipi huku kukiwa na Mkakati wa kuiuwa Chadema?
Kumbuka kwamba mlipa Zumari ndio Mchagua wimbo!
 
Waraka una maudhui ya kumwandaa Zitto Kabwe awe mwenyekiti. Waraka haukuwa na mikakati ya kudai uchaguzi.Suala la uchaguzi kwanini hawakulipeleka kwenye vikao vya Chama? Usitufanye sisi kuwa hatuna akili

Hakuna aliyekufanya usie na akili. Cha msingi ni hoja ndio zinazosimama zaidi kwenye ulimwengu wa leo. Matusi na kejeli ni kelele tu ambazo hazimzuii hata mtoto mdogo kulala usingizi.
Kama hoja ya waraka ndio hiyo, kwa nini taratibu zisifanywe kwa chama kuwaita walioandika huo waraka na kukaa nao mezani na ikistahiki hatua za msingi zichukuliwe?
We umeangalia hoja ya uchaguzi tu na ndiyo uliyojibu kwa haraka. Zile nyingine za ununuzi wa vifaa vya chama, uongozi wa mwenyekiti nakadhalika, kwa nini hazijajibiwa?
 
Mkuu, ukiwa unajenga nyumba yako unakopi ya jirani au unaangalia matakwa yako na bajeti uliyonayo?
Kuna tatizo kubwa naliona ambalo ni hatari sana. Msifanye vitu kwa kuwa CCM wanafanya.
Naona katika utetezi wako umeainisha mambo ya CCM. Kwani CCM ndo inayo run CDM?
Au utakuwa unaishi kwa kuangalia jirani yako anafanyaje na we ndio ukopi?
Ningekuelewa vizuri sana kama ungeleta vipengele hapa na tubishane kihoja zaidi kuliko kuweka vitu in comparison.
Kumbuka, hapa kinachojengwa ni CDM na sio CCM. Unless uwe ni double minded man ndo ntakuelewa.
Rudi tena mdau nakusubiri.
Punguza jazba. Twende taratiiibuuuuu

Kama najenga nyumba yangu halafu wewe Jirani unakuwa na Nyege za kuwashwa kuhusu jinsi ninavyojenga kwanini nisikuambie kwamba mbona unaniingilia na kunishauri kuwa jenga nyumba ya Ramani hii kwani hii unayoijenga haiendani na Wakati tuliopo,kwanini nisikuambie Jirani yangu mbona mwenyewe nawe unajenga na hujengi nyumba inayoendana na wakati lakini mimi unanishauri nijenge?

Siku zote ukiona Jirani yako anahangaika na mambo yako huku akiwa na yake yanayofanana na yako basi ujue kuwa hapo kuna agenda ya siri!
Kwanini CCM hakuna Makundi? Kwani CCM kuna Demokrasia? Kwani CCM uchaguzi wa Mwenyekiti uliwahi kufanyika? Kwani CCM hawajawahi kuwavua au kuwafukuza watu waliokiuka taratibu za chama?

Mbona mnataka kuwachagulia CDM viongozi? Km Chadema hakuna Demokrasia si waende Nccr,Tlp,Cuf, Udp,nk ambako kuna DEMOKRASIA? Kwanini Cdm tu?
 
Huo waraka hauna shida..tatizo umefanywa kwa siri..nalafu kwani uchaguzi ndani ya chama umetangazwa..?

Kingine jaribu ku connect dots..the same time CCM ikiongozwa na Nape wanalilia uchaguzi ndani ya Chadema.. Yaani wamejaribu mbinu zote wameshindwa sasa wanafikiri hili la uchaaguzi litaibomoa Chadema..na hawataamini..litakwenda kinyume na matarajio ya Nape..
 
Ritz wewe mmanyema wa mtaa wa kipata, gerezani Kariakoo unapata shida kuandika Kiswahili huoni aibu japo kidogo?

Hakuna kitu kinaitwa "hujue" hapo ulitakiwa kuandika "ujue".

Usipende kukaa kwenye vijiwe vya gahawa bila kujifunza kitu kipya, matokeo yake unabaki kuwa poyoyo kila kukicha.
Muraa!

Mimi ni muuza kahawa taachaje kukaa vijiweni.
 
Last edited by a moderator:
Kama hawana nia ovu inakuwaje wasimtaje mshirika mwenzao MM2? wana agenda gani? na zile email za mwigulu na nchimbi zikimhusisha zitto na kujenga mtandao wa ushindi wa uenyekiti kwa msaada wa maccm mbona hawakani hadharani? hawa watu kweli wanatumika na chama kiongeze intelijensia juu ya hawa mamluki.kuhusu mwikwabe kama anavujisha siri za chama chake akibainika afukuzwe chamani arudi alikotoka.
 
Kweli?Mbowe anaingiaje hapa? Hebu tulieni

Wakati tukiufanyia mwongozo wetu mabadiliko mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Lakini wakati mwongozo unachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa na yenye athari zisizomithirika kwa taasisi yetu.-Kitila Mkumbo
 
Back
Top Bottom