Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu bado Mwita Maranya hujue huyu Waitara alikuwa mwiba kwa John Heche kule Tarime.
Huo waraka ulikuwa wa ushindi,within chadema.Ni kama vile Hilary v/s Obama.sasa waupeleke kwenye kamati wa nini?Waraka wa kamati ni ule amabao ungeandaliwa ili kuikabili CCM 2015.Hebu muwe waelewa basiHuo waraka ulipelekwa kwenye vikao vya chama ili wanachama waujadili?
Mkuu, sidhani kama matakwa ya hawa jamaa yako nje ya katiba ya chama. Kama katiba ya chama inasema mwenyekiti atachaguliwa kila baada ya miaka 5 haimaanishi kuwa wafate kama vyama vingine vinavyofanya. Katiba ndio muongozo na lazima ifatwe na kama waliiandika wenyewe kwa kukubaliana iweje mtu mmoja aje kutumia mabavu na kufanya kama chama ni chake?
Embu tafakari halafu urudi kimya kimya bila kelele. Kinyume na hapo nadhani utakuwa ni shabiki wa chama na sio hoja zilizotolewa.
We sixgates anza kupaki kenge wewe.
Mlizoea kuburuza vyama vya upinzani kama CUF, TLP ,NCCR hapa ni ngoma nzita anza kupaki ---- wewe.
Mkuu unanipasua mbavu.
Labda wewe ndei huelewi. Kwani Katiba ya CDM ina kipengele kisemacho mtu haruhusiwi kugombea zaidi ya mara 2. Na hata km basi katiba inasema kuwa uchaguzi ufanyike kila baada ya miaka 5 ni haki Zitto kutengeneza Kikundi ndani ya Chama!? Je huko sio ndiko tunakotafsiri kua ni kukigawa chama makundi?
Kwanini asisubiri hadi muda wa uchaguzi ufike na agombee na km akizuiwa kugombea ndipo alalamike?
Na vipi kuhusu katiba ya CCM haisemi uchaguzi uwe unafanyika kila baada ya miaka mingapi? Na km inasema je ni lini CCM iliwahi kufanya uchaguzi wa mwenyekiti wa Taifa?
Na je mbona Ccm wanarithishana kile cheo cha Mwenyekiti au Demokrasia inatakiwa tu ionekane Cdm lakini kwa wengine hapana?
Elezea makundi ndani ya chama chenu cha mapinduzi acha na CDM kama ulivyotamka hapo mwanzoChadema si ndio kinaburuza wanachama. Namuonea huruma sana mohamed mtoi, ana uwezo ana akili ila nafasi yake kapewa Tumaini Makene hyu anachojua ni kupiga picha na tablet yake haji kutupa new feeds. Sasa ivi joh heche kamfanyia fitna mwaikabe. Chadema kwa kuuwa vipaji hamjambo.
Kugombea ubunge kwenye kura za maoni ndani ya chama ni kitu kingine, kwasababu hayuko mwenyewe. Wapo makamanda kibao akiwepo John Heche.
Hapa tunataka M2 ajisalimishe mwenyewe kabla hajatolewa kama nyoka
Waraka una maudhui ya kumwandaa Zitto Kabwe awe mwenyekiti. Waraka haukuwa na mikakati ya kudai uchaguzi.Suala la uchaguzi kwanini hawakulipeleka kwenye vikao vya Chama? Usitufanye sisi kuwa hatuna akili
Mkuu, ukiwa unajenga nyumba yako unakopi ya jirani au unaangalia matakwa yako na bajeti uliyonayo?
Kuna tatizo kubwa naliona ambalo ni hatari sana. Msifanye vitu kwa kuwa CCM wanafanya.
Naona katika utetezi wako umeainisha mambo ya CCM. Kwani CCM ndo inayo run CDM?
Au utakuwa unaishi kwa kuangalia jirani yako anafanyaje na we ndio ukopi?
Ningekuelewa vizuri sana kama ungeleta vipengele hapa na tubishane kihoja zaidi kuliko kuweka vitu in comparison.
Kumbuka, hapa kinachojengwa ni CDM na sio CCM. Unless uwe ni double minded man ndo ntakuelewa.
Rudi tena mdau nakusubiri.
Punguza jazba. Twende taratiiibuuuuu
Muraa!Ritz wewe mmanyema wa mtaa wa kipata, gerezani Kariakoo unapata shida kuandika Kiswahili huoni aibu japo kidogo?
Hakuna kitu kinaitwa "hujue" hapo ulitakiwa kuandika "ujue".
Usipende kukaa kwenye vijiwe vya gahawa bila kujifunza kitu kipya, matokeo yake unabaki kuwa poyoyo kila kukicha.
Kwani CCM imemfunga maisha Mzee Abood Jumbe?alidai nini?
Kweli?Mbowe anaingiaje hapa? Hebu tulieni