Upo katika huu uzi kwa msukumo wa "dini" ya Zitto Kabwe..... bhaaasi!
NANI TUMUUNGE MKONO KUCHUKUA NAFASI YA MKUU:
Baada ya utangulizi huo unaoonyesha kinagaubaga kwamba tunahitaji mabadiliko, hatua iliyofuata ilikuwa ni kuangalia nani anaweza kuleta mabadiliko tunayohitaji. Ni vema ikazingatiwa kwamba mtu ambaye tungemuunga mkono lazima awe ni mtu mwenye uwezo mkubwa kuliko tunayetaka kumtoa. Awe ana qualities za kiuongozi na zaidi sana awe na uwezo wa kupambana na mkuu aliyeko. Tukileta mtu asiyefahamika sana kwenye mifumo ya taasisi yetu hata kama angekuwa mzuri kiasi gani hatachagulika na mkuu aliyeko atarudi kwa urahisi na kuendelea kuididimiza taasisi.
Katika kuchunguza ndani ya taasisi tuliridhika kwamba mtendaji mkuu msaidizi ana sifa zote tulizozitaja hapo juu ingawa kila mwanadamu ana udhaifu wake. Ni dhahiri pia kwamba udhaifu wa mtendaji mkuu msaidizi unarekebika kuliko wa mkuu aliyepo. Kwa ujumla mtendaji mkuu:
Ni kiongozi anayeweza kuongoza taasisi bila kujenga makundi akijali zaidi kazi ya taasisi kuliko maslahi binafsi.
Ameonyesha kwa vitendo kwamba hana maslahi binafsi kwa kuwa tumeshuhudia akifanya kazi nyingi za taasisi bila kudai malipo kwa njia ya posho ama vinginevyo.
Anaheshimika na viongozi wa ndani na nje ya taasisi jambo ambalo ni la muhimu sana kwa ustawi wa taasisi na kwa yeye kuwa mkuu wa taasisi tunatarajia wakubwa wengi sana kutoka nje ya taasisi yetu kuiamini na hata kujiunga nasi katika kuhakikisha tunafanikisha lengo la taasisi.
Ni msomi wa kiwango cha juu na mwenye uwezo mkubwa katika kuchanganua mambo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii, kimichezo, nk jambo ambalo ni muhimu sana kwa kuwa ni hatari kuwa na kiongozi asiye na ujuzi wa kutosha kwenye masuala kama hayo.
Ndani ya taasisi anakubalika kwa makundi yote ya vijana, wazee na akina mama.
Uongozi wa sasa wa taasisi yetu umefanya tuonekana kwamba taasisi yetu ipo kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi. Yote hii ni kwa sababu tumekuwa hatuna mbinu mpya za mapambano zinabadilikabadilika zaidi ya maandamano ya kila mara. Kwa kuzingatia utamaduni wa watanzania wa kupenda amani, kuna haja ya kufuta hii taswira na njia rahisi ni kubadilisha uongozi wa taasisi haraka iwezekanavyo.
Uelewa wake wa mambo ya kiuchumi ni muhimu sana kwa taasisi kwa sasa. Tunahitaji kuja na vyanzo vipya vya mapato ikiwa tunahitaji kufanikiwa. Mkuu aliyepo si kwamba ameishiwa bali hana mbinu za maana za kuiimarisha taasisi kimapato kwa ajili ya malengo yake ya mbele.
Exposure kubwa na kukubalika katika siasa za kimataifa. Tunahitaji kiongozi ambaye anazifahamu siasa za kimataifa na anayeweza kuungwa mkono na viongozi wengi wa kimataifa. Ni hatari kutegemea utaweza kufanikisha malengo kama ya taasisi yetu bila mpango kabambe wa kuungwa mkono na jumuia ya kimataifa. Mpaka hivi sasa hakuna mpango wowote wala hata mchakato wa maana kuwa connected na jumuia ya kimataifa. Kiongozi wetu mkuu wa sasa yupo too local na hana mawasiliano yeyote ya maana na viongozi wengine katika kanda na kimataifa. Ndio maana mkuu huyo na mtendaji wake mkuu wamekuwa hawaonekani katika matukio makubwa ya kimataifa. Hata katika kutoa maoni katika mambo makubwa ya kitaifa na kimataifa viongozi hawa hawapo. Kwa kifupi kwa sababu ya aina ya viongozi tulio nao, nafasi ya taasisi yetu katika nyanja za kimataifa haipo!
Aina na staili ya uongozi wa sasa wa taasisi yetu ni kina kwamba nchi hii haipo hadi taasisi yetu itakapochukua dola. Yaani tunafanya mambo kama kwamba tutaanza upya kabisa tukichukua dola. Ni kwa sababu tumegombana na kila mtu katika utawala wan chi, vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama. Ukweli ni kwamba tutavihitaji vyombo hivi kabla na baada ya kuingia madarakani na ni ndoto kudhani kwamba tutakabidhiwa nchi kwa kugombana na kila mtu. Ni kwa sababu ya mtazamo kama huu ndio maana wakuu wetu wa sasa hawaonekani kabisa katika shughuli za kitaifa kama vile sherehe za uhuru wan chi, n.k.
Uwezo wa kuwaunganisha wasomi wa kada mbalimbali, wafanyabiashara wakubwa, watumishi wa umma na sekta binafsi, nk katika kupata muunganiko wa mawazo na kutoka na sera murua zinazogusa kila sekta. Hili la kuwashirikisha litaenda sambamba na kutoa elimu kwa wote waelewe na watuunge mkono. Tunasema hivi kwa kuwa watu wa kada mbalimbali hawajaelewa sera zetu juu ya mambo yanayowahusu mfano wafanyabiashara wakubwa, wawekezaji, wakulima, watumishi, wanafunzi,nk na hivyo hawajawa tayari kutuunga mkono. Kile kinachofanywa wakati wa uchaguzi kwa njia ya ilani ya uchaguzi na elimu kutolewa kwa njia ya kampeni majukwaani hakitoshi. Tunahitaji watu wajue tumeunda think tank kwa ajili hiyo na baadaye wajue nini kimetokana na think tank hiyo ili wajadili na kutoa maoni na hatimaye tutoke na kitu kinachokubalikwa na wananchi wote. Na tuna imani hilo tunayempendekeza ana uwezo nalo.
Kubwa zaidi ni kwamba alishaiangalia taasisi yetu na kuona mambo yanayohitaji mabadiliko na kujiangalia yeye na kuridhika kwamba ataweza kuleta mabadiliko tunayoyahitaji na ndipo mwaka 2009 aliamua kujitosa kuutafuta ukuu wa taasisi yetu kabla ya kuombwa kumwachia aliyepo.
-MM3