Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

CHADEMA inahitaji watu wenye uthubutu kama G. Lema. Mimi binafsi namkubali sana huyu jamaa. Ni mtu mwenye uchungu wa kulikomboa taifa hili na hakubali mtu yeyote aonekane msafi wakati ni mchafu na anatumia mbinu haramu aonekane kinara wakati ni mnafiki wa kutupwa. Inatia hasira sana pale mtu anakuwa hafanyi yale anayoyahubiri Zitto anarangi nyingi kuzidi hata kinyonga, Ni muuaji wa fikra za ukombozi wa kweli. Viongozi wa chama wamejitahidi sana kumvumilia kwa mambo yote mabaya aliyofanya ndani ya chama, thanks wameona sasa yatosha. To youth, if you want to succeed in politics find people like Lema to be your role model not hypocrite mysterious like Zitto.
 
g. J. Lema daima pongezi atapata ndani ya nchi yetu.
Ni wale mafisadi tu ndiyo wanafiki.

kwa taarifa yenu zitto anamwogopa kama simba!!!inasemekana alivyonyanganywa ubunge zitto ni mmoja kati wanacdm ambao hawakuhuzunika!!!!lema ni kiona mbali na mzalendo wa kweli.alikataa kununuliwa na mafisadi mjue.
 
Mi naamini wakumshukuru ni Mwigamba, nadhani yaliyotokea ni kwa ridhaa ya huyu bwana. Lile zengwe ni la kuwaingiza mkenge zito na mkumbo na M2
 
Lema alikataa kununuliwa na Mh sana na malipo yake ameifuta kabisa ccm arusha , juhudi zinaendelea ili kumalizia kazi monduli , kuna haja ya wana arusha kujenga mnara wa lema .
 
Huyu jamaa mungu ampe maisha marefu maana ni jembe balaa siyo lile,la monduli alilolitaja Mzee wa Kaya
 
kwa taarifa yenu zitto anamwogopa kama simba!!!inasemekana alivyonyanganywa ubunge zitto ni mmoja kati wanacdm ambao hawakuhuzunika!!!!lema ni kiona mbali na mzalendo wa kweli.alikataa kununuliwa na mafisadi mjue.

Kumnyang'anya ubunge Lema ulikuwa mpango wa JK na ZITTO ni swahiba wa JK!
 
Mi naamini wakumshukuru ni Mwigamba, nadhani yaliyotokea ni kwa ridhaa ya huyu bwana. Lile zengwe ni la kuwaingiza mkenge zito na mkumbo na M2

Wacha wee ! Kumbe Mwigamba naye jembe !
 
Mi naamini wakumshukuru ni Mwigamba, nadhani yaliyotokea ni kwa ridhaa ya huyu bwana. Lile zengwe ni la kuwaingiza mkenge zito na mkumbo na M2

Wacha wee ! Kumbe Mwigamba naye jembe !
 
Aisee sikujua kumbe Lema ndio alisababisha ule waraka kupatikana. Big up Lema
 
Leo narudia tena,Pamoja na kuwa mh. G.Lema ni binadamu! Lkn sijawahi KUTOKUMUAMINI na kumtilia shaka pindi anaposimamia hoja zake! Na labda nikiri tu najifunza mengi sana kupitia huyu jamaa! Na ninashawishika kuhisi ni kweli ipo nguvu ya Mungu inayomuongoza huyu jamaa.Mungu aendelee kukutia nguvu na kukuongoza, Wewe mi miongoni mwa watu muhimu sana ktk harakati hizi za ukombozi wa awamu ya pili.
 
Huo ni full unafiki tuu. Eti adui anachukizwa na kuporomoka kwako na eti anajifanya kukuelekeza njia sahihi za wewe kuwa imara.
Hili jambo liko wazi kuwa maamuzi yaliyofanywa ni pigo takatifu kwa CCM na wamebaki kuweweseka bila kificho.
Mbinu za CCM zote za kudhoofisha CHADEMA zimeshindikana, hii ndio ilikuwa karata yao ya mwisho, kumtumia Zitto na wafuasi wake akina Mkumbo ili kugawa CHADEMA, na ikiwezekana kumuweka huyo mamluki wao Zitto kuwa mwenyekiti, nayo imeshindikana.

CHADEMA ina ulinzi imara unaoonekana na usioonekana, hawawezi 'kuishukisha'.
 
Wachaga waliopo Chadema ni waaminifu sana. rekodi zangu zinaonyesha hakuna mchaga aliyewahi kufukuzwa Chadema.
Uenezaji wa chuki za ukabila Tanzania hautafanikiwa, nakuapia.
Watanzania wamechanganyikana, wengi wasio wachaga wameoa au kuolewa uchagani, wachaga nao wameoa na kuolewa katika makabila mengine, leo hii huwezi kunishawishi mimi niwachukie wachaga kwa sababu za kisiasa. Mnachosha midomo bure.
 
Ambavyo huwa unamtukuza huyu jamaa mwishowe utakufuru, Maanake Dr halafu majina kibao, ongezea na MTUKUFU basi ili roho yako iridhike.
Hayanihusu? pata ujumbe mdogo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM:


"Mtakwenda mtarudi mimi ndio Rais wenu hakuna mwingine mtakae mkimbilia"

Dr. Jakaya Khalfan Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM.
 
Back
Top Bottom