...kwa wale tuliokuwa UDSM 1996 hadi 1999/2000, mnamkumbuka rais wa DARUSO aliekuwa FoE? (Naomba mtu anikumbushe jina lake maana nimelisahau ila alikuwa msukuma). Huyu bwana alifanya vizuri tu undergraduate yake mbona hakuwa retained kuwa Tutorial Assistant kama Dr Mkumbo? Na jamaa huyu nisiemkumbuka jina lake alifukuzwa maeneo ya chuo wakati anasubiri kufanya interview Dar (hakuwa mwenyeji wala kuwa na ndugu Dar) na nakumbuka jamii ya wanafunzi wa UDSM kutoka Uganda ndio waliomchangia pesa ya kuishi akisubiri interview yake wakitambua mchango wake kwao (Mungu anisamehe kwani hata mie sikuchangia japo shilling!).
Am asking myself aloud : Je, sababu ya Dr Mkumbo kuwa retained na rais wetu wa DARUSO kabla yake kunyimwa haiwezi kuwa alienyimwa alikuwa anatetea haki wakati aliepewa alikuwa kibaraka???
JUST THINKING ALOUD!
Unalosema ina ukweli ndani yake, kwani licha ya kuendelea kufanya kazi pamoja na kwamba yuko CHADEMA ni bora ujiulize maswali yafuatayo kuhusu Dr. Kitila Mkumbo.
1. Ni kwanini ameendelea kufanya kazi UDSM ambayo VC (Prof. Mukandala) wake ni mtu muhimu sana katika serikali ya CCM, kwani Prof., ni mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2. Ni kwanini Dr. Mkumbo ameendelea kupewa vyeo UDSM, kwani baada ya kuwa Head wa Department of Psychology pale UDSM, sasa ni Dean School of Psychology DUCE?
Kumbuka kwamba hivi vyeo vyote ni vya kuteuliwa na VC pamoja na DVCs. Naelewa kuna watu watakuja kusema kwamba katika nafasi hizo alizoshikilia kuna Search Team inayopendekeza majina na teuzi husika. Ni kweli ki utaratibu ilitakiwa kuwa hivyo, lkn practically siyo. Nasema hivi kwasababu ya yanayoendelea pale UDSM. Kwa ufupi ni kwamba bila VC wa UDSM kukubali, wewe hutopata cheo kama hicho.Tuna mifano hai kwa yanayoendelea pale UDSM katika baadhi ya Shule ambapo uzoefu (hali halisi) inaonyesha kwamba BILA KUWA MTU WA VC, then sahau kabisa hizo posts kubwa za teuzi pale UDSM.
Pia naomba niwafahamishe wale watakaokuja na hoja ya seniority kwa Dr. Mkumbo. Ukweli ni kwamba posts kama za Dean pamoja na Heads wa Departments wanaangalia Senior Lectures. Lkn si kweli kwamba mara zote hili nalo linafanya kazi, kwani pale UDSM kwenye baadhi ya maidara kwenye shule mbalimbali zinaongozwa na Lecturers (siyo Siniors) pamoja na kwamba kwenye idara husika kuna senior lecturers wengi. Pia hata katika School of Education kuna Senior Lecturers wengi sana, hivyo siyo jambo jepesi kwa Dr. Mkumbo kupewa hizo nafasi bila kuwa na YES na Bwana mkubwa. Naomba nissisitize kwamba ili VC akupe nafasi za teuzi ni LAZIMA UWE MTU WAKE, sas swali hapa ni Je, Dr. Mkumbo ambaye amekuwa Senior Lecturer mwaka juzi naye ni mtu wa system?
3. Jambo lingine ambalo mimi toka awali ilinifanya niwe na mashaka na Dr. Kitila ni jinsi alivyomtetea Juliana Shonza kipindi kile anavuruga BAVICHA kwa kuita press conference na kuanza mashambulizi dhidi ya mwenyekiti wake ndugu Heche. Kama mtakumbuka vizuri ni kwamba huyu Dr. Mkumbo aliandika hapa JF na kwenye gazeti moja (nafikiri ni Raia Mwema kama kumbukumbu zangu zipo sahihi) akimtetea Juliana Shonza kwamba bado ni mtoto hivyo aachwe. Jambo hili lilinifanya niamini kwamba Dr. Mkumbo yuko CHADEMA kwa lengo maalumu na si vinginevyo.
Ahsanteni.