Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Waraka uliowaondoa Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo CHADEMA huu hapa

Mi nilidhani unauliza ni kwa nini ajira yake serikalini haijasitishwa kama ya baregu ukizingatia nafasi zao za kisiasa ndani ya Chadema ni zilezile??

Kwa hiyo jamaa pandikizi la gov chadema...hapana siamin hivyo...jamaa mwenyewe kateleze tuu hasa baada ya kujiona yeye ni kila kitu
 
By Zogwale
Hakika umenena mkuu, huyu Kitila Mkumbo alichomekwa pale UDSM akawa President wa DARUSO kipindi kile cha machafuko!!! Miaka ya tisini UDSM ilikuwa ni balaa!!! Akawa anajifanya kuwa ni strict kumbe anatekeleza masuala ya TISS!!! Walimweka pale kwa kuwa chuo kilikuwa kinachemka sana!!! Aliuza demokrasia ya wanafunzi!!!! Hivi hujiulizi hadi leo ni kwa nini yeye ni Lecturer pale Chuo chini ya VC Mkandala? Lecturers wengi waliokuwa na siasa za mrengo wa kushoto waliondoka kabisa hawakuruhusiwa kuwa chuo, na kama walikuwepo basi walikuwa wanaundia mizengwe sana!!!! Kitla umemsikia akiundiwa mizwengwe? Hapana!!! Kwa kuwa yuko kazini!!! Poleni sana CDM!!
 
Hata mimi naungana na wenzangu kukupongeza kamanda Lema japo ulipofanya kitendo kile cha kutumia mabavu nilikuwa miongoni mwa watu waliokulaumu sana na nikadhani huna busara, ila sasa nakuomba radhi sana kwa lawama zangu, nakufananisha na Petro mwanafunzi wa Bwana Yesu ambaye alikuwa anatumia nguvu na kufanya mambo kwa haraka na wala hakufukuzwa na Bwana , naona Zitto amekuwa kama Yuda aliyemwuza Bwana kwa vipande thelathini vya fedha. Hongera kamanda Lema!!!!!
 
...kwa wale tuliokuwa UDSM 1996 hadi 1999/2000, mnamkumbuka rais wa DARUSO aliekuwa FoE? (Naomba mtu anikumbushe jina lake maana nimelisahau ila alikuwa msukuma). Huyu bwana alifanya vizuri tu undergraduate yake mbona hakuwa retained kuwa Tutorial Assistant kama Dr Mkumbo? Na jamaa huyu nisiemkumbuka jina lake alifukuzwa maeneo ya chuo wakati anasubiri kufanya interview Dar (hakuwa mwenyeji wala kuwa na ndugu Dar) na nakumbuka jamii ya wanafunzi wa UDSM kutoka Uganda ndio waliomchangia pesa ya kuishi akisubiri interview yake wakitambua mchango wake kwao (Mungu anisamehe kwani hata mie sikuchangia japo shilling!).

Am asking myself aloud : Je, sababu ya Dr Mkumbo kuwa retained na rais wetu wa DARUSO kabla yake kunyimwa haiwezi kuwa alienyimwa alikuwa anatetea haki wakati aliepewa alikuwa kibaraka???
JUST THINKING ALOUD!

Unalosema ina ukweli ndani yake, kwani licha ya kuendelea kufanya kazi pamoja na kwamba yuko CHADEMA ni bora ujiulize maswali yafuatayo kuhusu Dr. Kitila Mkumbo.

1. Ni kwanini ameendelea kufanya kazi UDSM ambayo VC (Prof. Mukandala) wake ni mtu muhimu sana katika serikali ya CCM, kwani Prof., ni mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2. Ni kwanini Dr. Mkumbo ameendelea kupewa vyeo UDSM, kwani baada ya kuwa Head wa Department of Psychology pale UDSM, sasa ni Dean School of Psychology DUCE?

Kumbuka kwamba hivi vyeo vyote ni vya kuteuliwa na VC pamoja na DVCs. Naelewa kuna watu watakuja kusema kwamba katika nafasi hizo alizoshikilia kuna Search Team inayopendekeza majina na teuzi husika. Ni kweli ki utaratibu ilitakiwa kuwa hivyo, lkn practically siyo. Nasema hivi kwasababu ya yanayoendelea pale UDSM. Kwa ufupi ni kwamba bila VC wa UDSM kukubali, wewe hutopata cheo kama hicho.Tuna mifano hai kwa yanayoendelea pale UDSM katika baadhi ya Shule ambapo uzoefu (hali halisi) inaonyesha kwamba BILA KUWA MTU WA VC, then sahau kabisa hizo posts kubwa za teuzi pale UDSM.

Pia naomba niwafahamishe wale watakaokuja na hoja ya seniority kwa Dr. Mkumbo. Ukweli ni kwamba posts kama za Dean pamoja na Heads wa Departments wanaangalia Senior Lectures. Lkn si kweli kwamba mara zote hili nalo linafanya kazi, kwani pale UDSM kwenye baadhi ya maidara kwenye shule mbalimbali zinaongozwa na Lecturers (siyo Siniors) pamoja na kwamba kwenye idara husika kuna senior lecturers wengi. Pia hata katika School of Education kuna Senior Lecturers wengi sana, hivyo siyo jambo jepesi kwa Dr. Mkumbo kupewa hizo nafasi bila kuwa na YES na Bwana mkubwa. Naomba nissisitize kwamba ili VC akupe nafasi za teuzi ni LAZIMA UWE MTU WAKE, sas swali hapa ni Je, Dr. Mkumbo ambaye amekuwa Senior Lecturer mwaka juzi naye ni mtu wa system?

3. Jambo lingine ambalo mimi toka awali ilinifanya niwe na mashaka na Dr. Kitila ni jinsi alivyomtetea Juliana Shonza kipindi kile anavuruga BAVICHA kwa kuita press conference na kuanza mashambulizi dhidi ya mwenyekiti wake ndugu Heche. Kama mtakumbuka vizuri ni kwamba huyu Dr. Mkumbo aliandika hapa JF na kwenye gazeti moja (nafikiri ni Raia Mwema kama kumbukumbu zangu zipo sahihi) akimtetea Juliana Shonza kwamba bado ni mtoto hivyo aachwe. Jambo hili lilinifanya niamini kwamba Dr. Mkumbo yuko CHADEMA kwa lengo maalumu na si vinginevyo.
Ahsanteni.
 
Katika Waraka uliosababisha mkawa fired, ambao Kitika amekiri kwamba anaufahamu na alishiriki kuutengeneza, kuna ombi lilitolewa mle ndani muwaweshe wenzenu wawili katika swala zima la mshiko, kwa kuanzia wakatoa ombi la kupata japo M Mbilimbili japo waweze kuacha kitu nyumbani.

Na pia ikajitokeza issue ya kuhakikisha wanasaidiwa kupaja ajira sehemu sehemu,

Kwa sababu katika waraka husika, mmejiinua na kujitanua kwamba nyie ni watu wa kusimamia strategy mpaka zifanikiwe kwa ufasaha tofauti na uongozi wa sasa wa CHADEMA ambao unaruka ruka kutoka stragegy moja kwenda nyingine kwa sababu ya upungufu wa elimu.

Swali langu ni moja tu.

Mmekwisha wawezesha jamaa...???

Sangara,
Haya majungu yasiyo na msingi ndio yatakayokiua CHADEMA. Kuwasingizia Zitto na Kitila kuwa wanatumiwa na maadui bila kuwa na ushahidi, sijui kama inaisaidia CHADEMA au inaongeza tu umbea na chuki.

Jadili ubora au ujinga wa hoja zao bila kuingiza fitina zisizo na ushahidi. Aliyosema Kitila sio siri na wengi nje ya CHADEMA wameshayasema sana. Sio ajabu CCM wanatamani yaendelee maana yakiendelea, ChaDEMA itaendelea kuonekana kama chama cha watu fulani tu (Mbowes) na sio cha umma au demokrasia. Kwa hiyo ukiendeleza huu ujinga na ushabiki, utakuwa unasaidia kukidumisha CCM na kukifanya CHADEMA kidumae hapo kilipo na mashabiki bumbuazi.

Funguka macho, siasa ya kujenga nchi sio ushabiki wa Simba na Yanga.
 
Kwa hiyo jamaa pandikizi la gov chadema...hapana siamin hivyo...jamaa mwenyewe kateleze tuu hasa baada ya kujiona yeye ni kila kitu

Wafukuzwe tu, na mimi nasema wafukuzwe. Kitila, Zitto, M2, etc. wameikuta CHADEMA na wataiacha CHADEMA ikiwa na nguvu ile ile.
 
Mkakati huu ulikuwa kwa maslahi ya nani? wanachadema? au Watanzania au watu wachache wenye tamaa ya uongozi?

Hata hivyo kuna mambo mengine yanahitaji kufanyiwa kazi kama yataonekana kuwa ya ukweli ndani ya mkakati huu.

Umenena safi.hata zito na mkumbo wakifukuzwa yaliomo kwenye ule waraka yafanyiwe kazi
 
Sioni dhambi ya hawa jamaa. Mkakati huu uboreshwe na ufanyiwe kazi!
 
Ajira ya Baregu ilisitishwa kutokana na ushiriki wake kwenye siasa.

nakumbuka Baregu alifikisha umri wa kustaafu na ilikuwa aongezewe muda kama ilivyokuwa kwa wengine walioongezewa muda kipindi kile lakini yeye akagomewa watu wakaipigia kelele serikali kuhusiana hilo na waziri wa utumishi akasisitiza kuwa hawatampa mkataba kwa kuwa yeye anajishughulisha na siasa na ana wadhifa kwenye chama chake (Mjumbe wa CC), waziri akaulizwa iweje hiyo itokee kwa Prof. Baregu peke yake, mbona kuna Dr. Sengondo Mvungi naye ni kama Prof. Baregu, waziri akajibu kwa kifupi kuwa watachunguza, kupata ukweli wa swali la mwandishi.
Issue ikafa kibugu and Prof. Baregu was easily kicked out just like that, but Tumaini wakamchukua ndani ya muda mfupi tu.
 
Sangara,
Haya majungu yasiyo na msingi ndio yatakayokiua CHADEMA. Kuwasingizia Zitto na Kitila kuwa wanatumiwa na maadui bila kuwa na ushahidi, sijui kama inaisaidia CHADEMA au inaongeza tu umbea na chuki.

Jadili ubora au ujinga wa hoja zao bila kuingiza fitina zisizo na ushahidi. Aliyosema Kitila sio siri na wengi nje ya CHADEMA wameshayasema sana. Sio ajabu CCM wanatamani yaendelee maana yakiendelea, ChaDEMA itaendelea kuonekana kama chama cha watu fulani tu (Mbowes) na sio cha umma au demokrasia. Kwa hiyo ukiendeleza huu ujinga na ushabiki, utakuwa unasaidia kukidumisha CCM na kukifanya CHADEMA kidumae hapo kilipo na mashabiki bumbuazi.

Funguka macho, siasa ya kujenga nchi sio ushabiki wa Simba na Yanga.

we nae Bwana,umekaririshwa mambo ya kuandika humu nini? Umeusoma waraka? Haujaona ombi la pesa? Haujaona ahadi ya ajira?
 
Mtu mwenyewe mnaomsifia sio riziki. Tumesha jua anapenda nini zaidi.


Yule totolii wa Moshi na mfanyakazi wake walikamatwa fasta na polisi baada ya kulawitiana. Huu uzushi wenu kwa Lema ungekuwa kweli sidhani Polisi ingewachukua hata sekunde kumtia mbaroni na kupaaza sauti kwenye media zote duniani. Inashangaza mnaopiga kelele ni LB7 yaani hadi mnadharaulika.
 
we nae Bwana,umekaririshwa mambo ya kuandika humu nini? Umeusoma waraka? Haujaona ombi la pesa? Haujaona ahadi ya ajira?

Sangara,
Kama hayo yangekuwwepo na kama ni makosa yangeidhinishwa kwenye sababu za kuwafukuza. Majungu utayajua tu maana yanaandikwa kwa muelekeo wa kumchafua mtu.

Jadili hoja ya Dr. Kitila inayosema kuwa, wakati umefika kumuondoa Mbowe na kuwa na uongozi wa wasomi.

 
Last edited by a moderator:
Umenifanya na mie nicheke. Kumbe huwa unaelewa, ila basi tu....
...Mkuu hawa jamaa Marcopolo, Ritz, Chama, na FF wana akili zao nzuri tu. ukitaka kujua waambie waunchukue mkakati wa Zitto na Kitila wautekeleze kumng'oa JK uone watakavyolipuka. Hawatamani kabisa akina Zitto watimuliwe CHADEMA.
 
Sangara,
Kama hayo yangekuwwepo na kama ni makosa yangeidhinishwa kwenye sababu za kuwafukuza. Majungu utayajua tu maana yanaandikwa kwa muelekeo wa kumchafua mtu.

Jadili hoja ya Dr. Kitila inayosema kuwa, wakati umefika kumuondoa Mbowe na kuwa na uongozi wa wasomi.



Malizia mkuu "waliosoma ktk vyuo vya kueleweka"
Dhambi ya ubaguzi.....
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom