Waraka wa Bashir Yakub: Tundu Lissu japo unaumwa lakini umeshindwa

Waraka wa Bashir Yakub: Tundu Lissu japo unaumwa lakini umeshindwa

Usichokijua ni kuwa hao unaodhani wameshinda ndio wapuuzi na kuna mengi sana wametuficha chini ya carpet..

Anyways, hii ndio TZ ya viwonder na acha sinema liendelee
 
Hamna haja ya kutoa lugha kali !! Tusubiri "MWANASHERIA WETU MSOMI" Atafungua kesi "MAHAKAMA YA KIMATAIFA" Kupinga makubaliano yaliyofikiwa kwani wale WAZUNGU WAMESAINI WAKIWA WAMELEWA !!!
 
Tuliwaita waizi tukawapelekea invoice ya trillion 484 leo wamekubali kulipa dola millioni 300 sawa na billioni 700. Hivi kutoka trillion 484 hadi billion 700 huu si ni ukichaa? Lisu hakukosea aliposema zile ripoti za kina prof Mruma na Ossoro ni Rubish. Yaani tunalipwa 0. Halafu tunajivuna. Mchanga uliopo bandarini vipi mbona kimya? Bado tunaendelea kupigwa sana
 
Ni bwabwa mmoja ambae anapenda sana kushobokashoboka alaf anashobokea ovyo ovyo dawa ni kumpa za uso mama huyu..alaf anaona kingereza ndo maisha alaf nshamwambia mie mzaramo ntakuchamba kizaramo kingereza huko huko unakooshea vyombo sio hapa kwangu
Sipendagi kuingilia ugomvi Wa watu, lk hapa ngoja nicheke kidogo.....hahahahaaaaaaa!!!
Kweli we mzaramo
 
Naona tayari watu wamebweteka na million 300. Mpska mkalimani alitetemeka akawa anakosea hiyo amount. Sjui ingekuwaje kama wangesema billion!!! Mleta nada angetuambia pia kama serikali ingefuata ushauri wa Lissu tungepoteza kiasi gani. Maana inawezekana faida ingekuwa kubwa zaidi kuliko tuliyoipata.

Nonetheless, tukubali kuwa Lissu ameshindwa!!

Je, USD 194 billion zitakuja lini?

Tatizo watu wameshindwa kulinganisha tulichopata na tunachodai!!
 
Mwanzoni mlisema hivyohivyo kukatisha watu tamaa lkn hamtafanikiwa.

Hatafanikiwa nani?

Wengine hatukurupuki kushangilia visivo natija

Mwenye akili timamu angehoji uhalali wa kupewa 0.01..% ya maadai ya maprofesa wetu unapewa uwongo unashangilia!

Maana yake walipika ripoti.... Walidanganya

Wewe unaona nini hapo?
 
Kama walijua Angeshindwa kwanini walimtandika Risasi?
Walijua yeye ni kitisho cha kuwaumbua.




Nchi hii kuna watu wa ajabu sana... Kwa Mwananchi wa kawaida ambae anajua kushangilia tu yeye atapokea taarifa kama ilivyo na kushangilia.., ni ngumu sana kudanganya watu wote kwa wakati wote.. Wengi wameingia mkenge.. Naona propaganda kwamba "WANAUME wamekubali kutulipa"..,

.., kuweka kumbukumbu sawa,
USD300M sio deni..., ni kulinda uaminifu.. ni kama bonus.., hakuna deni lolote walilokubali kwa mujibu wa maelezo ya pande zote mbili..., bonus haiwezi kuwa deni., "Kama malipo ta kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kupitia biashara ya kampuni hiyo"


Kwa hiyo BARRICK watalipa bilioni 600 (USD300M) na sio ile trilioni 450 ambayo tulielezwa na kuaminishwa awali kwamba ndio tunawadai!? Tunashangilia tena.. Sisi watu wa maajabu na hatujawahi kuacha kujishangaza.., Zile kelele za trilioni 400 ambazo tulielezwa tunawadai BARRICK zimeyeyuka ghafla..

Bado BARRICK wanakwenda kuchenjua wenyewe. Wanakwenda kupeleka wenyewe sokoni, kwenye masoko ya kimataifa Belgium, RSA, Britain. Baadae Mauzo baada ya safari yote ndio analeta mezani faida ya Mauzo GOT na BARRICK wagawane 50/50 percent . Hii unaona iko sawa tu!?

Ukimsikiliza Profesa Kabudi na Dr. John Thornton, kuna eneo Kabudi anasema WAMEKUBALI lakini Thornton anazungumzia subject to APPROVAL ya wakubwa zake huko kuliko na head quarter zao ambazo huenda zikahamia Mwanza kwa mujibu wa makubaliano..

..., ukimsikiliza Dr John Thornton anasema "proposal zote lazima zipitishwe na London Board of Directors na Acacia ..." Tunafanya propaganda ambazo hazina faida hata.L kidogo....., changa la macho ....., kutoka madai ya trilioni 426 hadi bilioni 700 bado unashangilia tu.

My prudence would have been to hold this press conference until everything has been approved by their shareholders and the board in London.., to avoid any potential embarrassment in future.

Usishangae BARRICK/ACACIA wakagoma..., au wakaja na counter proposal.. maana hata kama BARRICK ni majority share holder wa ACACIA.., minority wakigoma itabidi kutumia kwenye usuluhishi au kuwalipa minority kama watakubali kununuliwa. its bit tricky.. lets remain sober for now.. Nasubiri press release ya BARRICK/ACACIA..

Mkuu you are on the money, unajua ukitaka kumtega tembo muekee pipa la maji, mikeke na mihemko yote inaisha kiulaini.

Ngoja chairmen arudi tuangalie the true pictures ya hii migodi, halafu tufanye makubaliano ya kweli, na sio movie.
 
Umeweka na namba ya simu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] alafu umeandika pumba kiasi hiki?? Swali wamelipa cash?? Umeziona?? Ebu toka bana
 
Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255784482959.

Pole sana msomi Lissu kwa kuumwa. Lakini sasa kwa taarifa za jana ni kuwa unapata nafuu na Mungu Mwenyezi awe nawe urejee.

Hata hivyo huku ulipotuacha ni umeshindwa vibaya. Wale uliosema watatushitaki na kuwalipa mabilioni sasa wao ndio wanatulipa sisi mabilioni.

Kile ulichosema kuwa ni makosa yetu ya mikataba na ulofa, wamekubali kuwa ni makosa yao na wako tayari kwa marekebisho ya "terms" vipengele vipya kwenye mikataba.

Hata zile kesi ndogondogo tulizokuwa nao katika mahakama "tribunal" mbalimbali sasa nazo wamekubali iundwe kamati ya kuzimaliza kwa mazungumzo.

Lakini kubwa kuliko yote msomi Lissu ni kuwa wamekubali mgao wa 50/50 wa faida na Tz kuwa na wawakilishi kwenye bodi ya wakurugenzi na mengine mengi yenye kutia moyo. Sijui, lakin nadhan habari hizi sio njema sana kwako.

Msomi Lissu, siku nyingine ukiambiwa wako watu wana akili kuliko wewe uwe mwepesi tu kuelewa. Ukiambiwa wako watu wanaona maili 50 zaidi yako uelewe haraka.

Hatukatai, unaweza kuwa mzungumzaji mzuri lakin sio mwenye upeo. Upeo hupimwa kwa matokeo ya matendo. Na kwa matokeo haya twaweza tu kupima nani mwenye upeo kati ya wale uliowaita wa hovyo na wewe. Pia twaweza kujua wa hovyo ni nani sasa.

Nilikushangaa sana uliposema huoni kosa la Acacia. Watu wamedanganya uzito wa madini, wamedanganya sampuli walizobeba na ushahidi upo, msomi unasema huoni kosa !!!? , Looh.

Unajua vyema kuwa hawa jamaa wangekuwa upande salama kama ulivyopiga chapuo wasingefikia makubaliano kama haya. Wangeenda kwenye tribunal za kimataifa kama ulivyowasaidia kupendekeza na wangeshinda na tungelipa mabilioni kama ulivyokuwa umetabiri.

Ulikera sana hapa :

Makontena yakazuiwa, ukasema kimkataba ni yao na yamezuiwa kimakosa.

Ripoti ya kwanza ikasomwa,ukasema ripoti hiyo ni takataka"rubbish".

Ripoti ya pili ikasomwa, ukasema hamna jipya.

Akaja bosi wa Acacia Prof. John.L.Thompton akasema watalipa, ukasema hajasema kama watatulipa na hawawezi kutulipa.

Ulidhihirisha uadui na nia ovu na ndio maana ni halali leo kusema JAPO UNAUMWA LAKINI UMESHINDWA. Haikujulikana ulitaka nini hasa.

Msomi, hawa watu hawakuwa wasafi na hili kila Mtanzania aliliona isipokuwa wewe. Kwa matokeo haya sasa twaweza kujua nani ana maamuzi ya KUKURUPUKA na kuzungumza hovyo.

Tunakutakia afya njema lakini upunguze kidogo kuropoka msomi. Watu wako makini kuliko unavyofikiria.
wee Yakubu wewe tumia kidogo hata 0.0001% ya ubongo wako.
hivi ukiwa unaoga kwenye bafu la uswahilini akaja chizi na kuchukua taulo uliloning'iniza, kweli utamkimbilia kumnyang'anya taulo au utakubali sharti lake dogo tu la kumwamkua "shikamoo"?

$300B ni peanut ukilinganisha na investment ya Barrick nchini, they cant risk their massive investment while all what they need to do is to shout a "shikamoo" ($300M). also remember it's a meagre 0.16% of the TRA's reported tax bill against them ($190B) - labda uniambie TRA walitudanganya.

Lissu was, still is and will always be right. hawa jamaa (Barrick) siku wakiamua kama noma na iwe noma hatuna chetu.

hiyo 50/50 bado ni conversation kwa ajili ya baadae. which "baadae"? only God knows ukizingatia lifetime iliyobaki, as well as the gold deposit, ya migodi ya Barrick ni kidogo sana ukilinganisha na ambacho tayari kimechimbwa na kuchukuliwa na hawa rafiki zenu mliowatetea kwa siku nyingi!
 
Back
Top Bottom