Waraka wa Bashir Yakub: Tundu Lissu japo unaumwa lakini umeshindwa

Waraka wa Bashir Yakub: Tundu Lissu japo unaumwa lakini umeshindwa

Walitaka kumuua ili ujinga wao baadae usipate wa kuweka wazi na kukosoa.

Lissu atakuja kukueleza Mr Yakubu ujinga wa rushwa mlopokea kutrade off usd bilioni 400 kwa ajili ya share 16% na m300usd
 
Kama walijua Angeshindwa kwanini walimtandika Risasi?
Walijua yeye ni kitisho cha kuwaumbua.




Nchi hii kuna watu wa ajabu sana... Kwa Mwananchi wa kawaida ambae anajua kushangilia tu yeye atapokea taarifa kama ilivyo na kushangilia.., ni ngumu sana kudanganya watu wote kwa wakati wote.. Wengi wameingia mkenge.. Naona propaganda kwamba "WANAUME wamekubali kutulipa"..,

.., kuweka kumbukumbu sawa,
USD300M sio deni..., ni kulinda uaminifu.. ni kama bonus.., hakuna deni lolote walilokubali kwa mujibu wa maelezo ya pande zote mbili..., bonus haiwezi kuwa deni., "Kama malipo ta kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kupitia biashara ya kampuni hiyo"


Kwa hiyo BARRICK watalipa bilioni 600 (USD300M) na sio ile trilioni 450 ambayo tulielezwa na kuaminishwa awali kwamba ndio tunawadai!? Tunashangilia tena.. Sisi watu wa maajabu na hatujawahi kuacha kujishangaza.., Zile kelele za trilioni 400 ambazo tulielezwa tunawadai BARRICK zimeyeyuka ghafla..

Bado BARRICK wanakwenda kuchenjua wenyewe. Wanakwenda kupeleka wenyewe sokoni, kwenye masoko ya kimataifa Belgium, RSA, Britain. Baadae Mauzo baada ya safari yote ndio analeta mezani faida ya Mauzo GOT na BARRICK wagawane 50/50 percent . Hii unaona iko sawa tu!?

Ukimsikiliza Profesa Kabudi na Dr. John Thornton, kuna eneo Kabudi anasema WAMEKUBALI lakini Thornton anazungumzia subject to APPROVAL ya wakubwa zake huko kuliko na head quarter zao ambazo huenda zikahamia Mwanza kwa mujibu wa makubaliano..

..., ukimsikiliza Dr John Thornton anasema "proposal zote lazima zipitishwe na London Board of Directors na Acacia ..." Tunafanya propaganda ambazo hazina faida hata.L kidogo....., changa la macho ....., kutoka madai ya trilioni 426 hadi bilioni 700 bado unashangilia tu.

My prudence would have been to hold this press conference until everything has been approved by their shareholders and the board in London.., to avoid any potential embarrassment in future.

Usishangae BARRICK/ACACIA wakagoma..., au wakaja na counter proposal.. maana hata kama BARRICK ni majority share holder wa ACACIA.., minority wakigoma itabidi kutumia kwenye usuluhishi au kuwalipa minority kama watakubali kununuliwa. its bit tricky.. lets remain sober for now.. Nasubiri press release ya BARRICK/ACACIA..
Kwa hiyo utaenda London kuwambia wasikubali au siyo!!!?cc watz wanyonge machozi yetu yanakudondokea kwenye paji lako la USO haya bwana poa tu lkn Mungu yuko nasi!
 
Nyumbu hazikubaligi kushindwa, hizo hata zikikuta dem zao zinapigwa miti zitakataa na kusema jamaa amepiga ila hakufika mwisho, hapo bado watabeza juhudi za serikali, kisu kimeingia kwenye mfupa
 
Hatafanikiwa nani?

Wengine hatukurupuki kushangilia visivo natija

Mwenye akili timamu angehoji uhalali wa kupewa 0.01..% ya maadai ya maprofesa wetu unapewa uwongo unashangilia!

Maana yake walipika ripoti.... Walidanganya

Wewe unaona nini hapo?
Mm naona kuna hatua imepigwa na bado tunaendelea na majadiliano hadi kitaeleweka.HUO NI MWANZO TU.
Hatafanikiwa nani?

Wengine hatukurupuki kushangilia visivo natija

Mwenye akili timamu angehoji uhalali wa kupewa 0.01..% ya maadai ya maprofesa wetu unapewa uwongo unashangilia!

Maana yake walipika ripoti.... Walidanganya

Wewe unaona nini hapo?
 
Kwa hiyo unatakaje,! We unataka wasilipe or? Maana wameshakubali bado unapayuka kama kware!

Malipo mengine yanafanyika kwa kuwa wana uhakika wa kuendelea kupiga tu hivyo wana pretend kuwa waungwana waendelee kupiga
 
Mm naona kuna hatua imepigwa na bado tunaendelea na majadiliano hadi kitaeleweka.HUO NI MWANZO TU.

Hatua hupigwa kwa kuanisha mambo makuu ya msingi yote kwenye katiba bora.

Ili tunapokosea tunafanya rejea, sasa hawa wamekubalia baada yakupiga kahawa magogoni

Ebo akiingia mwingine?
 
Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255784482959.

Pole sana msomi Lissu kwa kuumwa. Lakini sasa kwa taarifa za jana ni kuwa unapata nafuu na Mungu Mwenyezi awe nawe urejee.

Hata hivyo huku ulipotuacha ni umeshindwa vibaya. Wale uliosema watatushitaki na kuwalipa mabilioni sasa wao ndio wanatulipa sisi mabilioni.

Kile ulichosema kuwa ni makosa yetu ya mikataba na ulofa, wamekubali kuwa ni makosa yao na wako tayari kwa marekebisho ya "terms" vipengele vipya kwenye mikataba.

Hata zile kesi ndogondogo tulizokuwa nao katika mahakama "tribunal" mbalimbali sasa nazo wamekubali iundwe kamati ya kuzimaliza kwa mazungumzo.

Lakini kubwa kuliko yote msomi Lissu ni kuwa wamekubali mgao wa 50/50 wa faida na Tz kuwa na wawakilishi kwenye bodi ya wakurugenzi na mengine mengi yenye kutia moyo. Sijui, lakin nadhan habari hizi sio njema sana kwako.

Msomi Lissu, siku nyingine ukiambiwa wako watu wana akili kuliko wewe uwe mwepesi tu kuelewa. Ukiambiwa wako watu wanaona maili 50 zaidi yako uelewe haraka.

Hatukatai, unaweza kuwa mzungumzaji mzuri lakin sio mwenye upeo. Upeo hupimwa kwa matokeo ya matendo. Na kwa matokeo haya twaweza tu kupima nani mwenye upeo kati ya wale uliowaita wa hovyo na wewe. Pia twaweza kujua wa hovyo ni nani sasa.

Nilikushangaa sana uliposema huoni kosa la Acacia. Watu wamedanganya uzito wa madini, wamedanganya sampuli walizobeba na ushahidi upo, msomi unasema huoni kosa !!!? , Looh.

Unajua vyema kuwa hawa jamaa wangekuwa upande salama kama ulivyopiga chapuo wasingefikia makubaliano kama haya. Wangeenda kwenye tribunal za kimataifa kama ulivyowasaidia kupendekeza na wangeshinda na tungelipa mabilioni kama ulivyokuwa umetabiri.

Ulikera sana hapa :

Makontena yakazuiwa, ukasema kimkataba ni yao na yamezuiwa kimakosa.

Ripoti ya kwanza ikasomwa,ukasema ripoti hiyo ni takataka"rubbish".

Ripoti ya pili ikasomwa, ukasema hamna jipya.

Akaja bosi wa Acacia Prof. John.L.Thompton akasema watalipa, ukasema hajasema kama watatulipa na hawawezi kutulipa.

Ulidhihirisha uadui na nia ovu na ndio maana ni halali leo kusema JAPO UNAUMWA LAKINI UMESHINDWA. Haikujulikana ulitaka nini hasa.

Msomi, hawa watu hawakuwa wasafi na hili kila Mtanzania aliliona isipokuwa wewe. Kwa matokeo haya sasa twaweza kujua nani ana maamuzi ya KUKURUPUKA na kuzungumza hovyo.

Tunakutakia afya njema lakini upunguze kidogo kuropoka msomi. Watu wako makini kuliko unavyofikiria.

Hii ndio sifa yetu kuu ambayo imeifanya Tanzania yetu kuwa masikini na fukara hadi wa leo hii.

Bado siamini kama kweli hayo tulotangaziwa leo ndo hasa matokeo ya mazungumzo tulojuzwa huko nyuma.

Nini kipo nyuma ya hii movie hata Leo wajitokeze hadharani tena kimya kimya bila hata zile "amsha amsha " na promo za kuwataka wananchi kuwa karibu na luninga zao!!Kuna namna hapa
 
Lissu ni mropokaji msomi hana lolote huyo case anazoziweza ni case za kuku hizi nyingine mnamuonea tu masikini wa Mungu.
 
Walitaka kumuua ili ujinga wao baadae usipate wa kuweka wazi na kukosoa.

Lissu atakuja kukueleza Mr Yakubu ujinga wa rushwa mlopokea kutrade off uds bilioni 400 kwa ajili ya share 16% na m300usd
Lisu kwisha habari yake.
 
Hatua hupigwa kwa kuanisha mambo makuu ya msingi yote kwenye katiba bora.

Ili tunapokosea tunafanya rejea, sasa hawa wamekubalia baada yakupiga kahawa magogoni

Ebo akiingia mwingine?
Tumalize kwanza tulichokianza
 
Kwa hyo ni sawa na tumeshtakiwa??
Hawakuwa na sababu tena ya kutuishtaki, bado wanahitaji kuendelea na biashara yao hapa Tz. Maadamu tumenywea na kukubali kulipwa hivyo vijisenti kwa nini wapoteze muda wao na kesi? Wao wana uhakika wa kuzirudisha huzo pesa kwa muda mfupi tu wakiendelea na biashara yao hapa Tz. Huitaji kuwa na akili kubwa kutambua jambo kama hilo. Hicho kiasi cha 700bil. ni kidogo sana kulinganisha na walivyotupiga. Na wana uhakika wa kuendelea kupiga tu, hii ni bongo mkuu.
 
Mkuu hapo tumepewa rushwa in the name of Good faith
Hauwezi ukapewa ahadi ya 0.15% ya unachokidai ukajisifu mshindi . Hiyo ni bakshishi a.k.a rushwa ili unyamaze, uache makelele ya kuwaharibia kwenye soko la hisa duniani.
Mkuu najua umeumia sana na bado unaendelea kukwazika na hayo makubaliano. Pambana na hali yako.
 
Ha ha haa...! Wajinga ndio waliwao. Tumefikia kiwango cha ujinga kinachohatarisha si tu hatma yetu tulipo, hapana, ni hatma ya vijukuu na vitukuu wetu. Yaani tunajadiliana na wezi na kufikia muafaka, duh!
 
Back
Top Bottom