Membe ni Kati ya watu wenye uwezo mkubwa sana wa Akili na Uongozi.
Ni kwa sababu tu hapa nchini hatuna utaratibu wa kuwafanyia midahalo Viongozi wetu wanaogombea cheo cha Urais
Kama tungefanya midahalo ya wagombea ni wagombea wachache sana wangeweza kufikia kiwango cha Membe cha kujieleza.
Membe ni Genius, huwezi simama nae kwenye mdahalo na ukamshinda kirahisi.
Jambo jingine, Membe Yuko humble, hana makuu na anawajari watu sana.
Cheo cha Uraisi ni kama bahati vile, ila Membe ana hadhi ya kuwa Raisi wa Tanzania.
Namna moja ya kumpima mtu mwenye IQ kubwa ni kumsikia anavyo weza kujieleza na kuyaelezea maswala mbali mbali.
Ndio maana nchi zilizoendelea Kama Marekani wagombea Uraisi hupitia midaharo mingi.
Hapa nasema ukweli mtu Kama Lowasa uwezo wa kujieleza ni Zero. Na angebahatika kupata Urais mambo mengi yangefanywa naw engine
Nchi hii kutoka na taratibu mbovu zinazofatwa ili kumpata Raisi wa nchi iko siku tutampata Raisi Zero Brain, au MWENDAWAZIMU.
La tuanze kuwafanyia midahalo wagombea wetu ili tujiridhishe na utimamu wao.