Mimi kama muumini mzuri wa kanisa katoliki ninayeamini katika kanisa la kisinoni Ushirika, Ushiriki na Umisionari siamni katika matamko ya kanisa kwa masuala ya kisiasa.
Kanisa haliwezi kuwa ndio muongozo wa namna gani serikali itende na kutekeleza wajibu wake. Tukiendekeza haya ipo siku serikali haitafanya lolote mpaka kanisa litoe kauli.
Bahati mbaya sana baraza la maaskofu katoliki nchini limekuwa biased kila inapotokea nchi inayoongozwa na Rais Muislamu.
Rais Mkapa aliingia mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa viwanja vya ndege na kampuni ya Swissport TEC haikutoa tamko, Rais Magufuli aliiongezea mkataba kampuni ya TICTS kuendesha bandari ya Dar es Salaam TEC haikusema neno...
Awamu ya 5 ya Rais Magufuli ndio kipindi kigumu ambacho utawala wa sheria na misingi ya demokrasia ilinyongwa hata kupelekea baadhi ya watu kuishi uhamishoni, wengine kupotea mpaka leo, CAG kung'olewa ofisini baada ya kubaini upotevu wa takribani shilingi trilioni moja nk TEC hawakutoa neno
Tuliwasikia TEC wakidai serikali tatu kupitia rasimu ya katiba ya Jaji Warioba....hatukuwahi kuwasikia TEC wakihoji maaskofu wao waliopata mgao wa escrow na benki yao kutumika kupitishia fedha za ufisadi benki ya mkombozi ambayo ni mali ya kanisa katoliki.
Hatujawahi kuwasikia TEC wakitoa tamko kuhusu mapadre wanaozaa na waumini na wanaowalawiti watoto nk
Nasema hivi Tanzania haiwezi kuendeshwa na matamko ya kanisa. Tunaheshimu maoni yao lakini sio ithibati kwamba lazima yafuatwe wachape injili kama wanataka siasa Wasajili chama cha siasa au wavue majoho na kujiunga na siasa sio kutumika.