Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Sote tunaona yanayoendelea ndani ya CHADEMA ya leo. Uchaguzi ndani ya chama umezaa kizaazaa baada ya madalali wa kisiasa nchini kupigwa chini.
Takriban miaka 12 iliyopita, wakati huo Kijana Zitto Kabwe, Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba walipanga mkakati wa kumng'oa Freeman Mbowe, hoja yao kuu ilikuwa ni kuwa Mwenyekiti hatoshi, anawachelewesha.
Zitto, Mwigamba na Kitila wakasuka mpango kabambe wa kuwasaidia kushinda uchaguzi wa mwenyekiti ambao ulikuwa unafanyika mwakani. Kwa bahati mbaya mkakati huo ukadakwa. Akina Zitto wakaitwa kwenye kikao maalum cha chama kuhoji mpango wao huo. Hii ikapelekea kuvuliwa nyadhifa zao zote ndani ya chama na kufukuzwa uanachama. Zitto alijaribu kupambana kupinga kuvuliwa uanachama lakini baadae akasema kuwa kama wenzako hawakutaki inabidi uondoke. Akaondoka akaenda kuipa nguvu ACT Wazalendo.
Hata hivyo cha ajabu katika siasa za Tanzania, Wale tuliodhani ni makamanda kweli akina Silinde, Lijualikali, Katambi, Joshua Nassari walikuja kwenda CCM. Na wale wengine kama Halima Mdee, Shonza, Matiko na Bulaya wakakisaliti chama kwa kughushi nyaraka ili waingie bungeni.
Na wale tuliodhani ni makamanda wa msitari wa mbele, akina Kigaila na Salum Mwalimu wapenzi wao ndo hao COVID-19, na inasemekana wao ndo wakiiba mhuri wa chama kuwezesha hilo!.
Sasa baba lao ni huyu Mbowe, tuliyedhani ni mwamba, na tukamuimbia hata ule wimbo wa "Mwamba tuvushe". Leo chama kinapata mashambulizi kila kona yeye kanyuti as if hana interest na kuna kila dalili yuko nyuma ya huu uasi unaoendelea ndani ya chama.
Swali la kujiuliza, Je akina Zitto walifahamu jambo ndani ya CHADEMA wakataka kulitatua kwa kumng'oa mwamba kwenye uenyekiti wa chama?.
Zitto tulimshusha kisiasa kwa kumuita msaliti je leo tumsafishe kuwa alikuwa mzalendo wa kweli wa CHADEMA ila wasaliti halisi ni hawa wanaoivuruga CHADEMA leo?.