Waraka wa Profesa Anna Tibaijuka kuhusu Maendeleo ya Mkoa wa Kagera. "Kagera Twafa"

Alipokua wazili alisaidiaje huko bukoba?
Wakitoka ndo akili zinwarudia baada ya kuwa watu wa kawaida.
Ila wakiwa madarakani hawajui shida za watu wa chini
 
Nyie mmewekeza wapi? Mambo mengine nilawama tu kwa serikali. Mwenyeweshule zake na uwekezaji wake kaweka Dsm analaumu... Siasa hatari sana

Wachaga shule nzuri ipo kilimanjaro. Nyumba nzuri kilimanjaro. Unaambiwa ktk Tz sehem nyumba kupanga ni bei chee ni Kilimanjaro.. wenzenu wanaishi mikocheni ila wama magorofa Kilimanjaro nyie mnalia lia tu...
 
Wahaya hamrudi makwenu baada ya kufika town haswa Dar
Mama Mboga ( Tibaijuka) na wenzako wengi mmewekeza Dar. sasa hilo pato la wananchi wa kwenu per capita litakua vipi? Wenzenu Wachaga wanawekeza kwao baada ya kuchuma wewe na kaka zako mmejimilikisha ardhi na kuwekeza Changanyikeni ; hivyo kupaisha pato la Bandari ya Salama!
Bojo Acha kulalamika rudini Kagera .
Nyerere aliwafundisha self reliance ulipokuwa unasoma au hukulielewa somo?
 
MamaTiba hana shule Mwanza
 
Kiongozi akiwa nje ya baraza ,kumbukumbu huwa inarudi katika uchambuzi na tathimini ya viashiria vya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya mwananchi.
Kuna suala la sera na sheria mbalimbali zilizotungwa na kutekelezwa ni kikwazo kwa maendeleo na ukwamuaji wa mwananchi wa kawaida:mfano;
1.Mkulima kukatazwa kuuza mazao aliyolima nje ya nchi.
2.Kuwa na sifa ya kiongozi wa kisiasa ya kuchaguliwa kuwa ni kujua kusoma na kuandika.
3.Viongozi kupeleka watoto wao shule za "English medium",huku wakijua kuwa kila mtu mwenye kipato anataka mtoto wake aende kusoma shule zenye mikondo ya kiingereza(English medium),je kubadilisha sheria na mfumo wa elimu ni gharama kiasi gani?!
 
Ya kwanza ilikuwa kifo cha BCU. Hiki chama cha ushirika kilisomesha watu wengi. BCU ilileta benki, ilifundisha wakulima na kuwekeza Kagera. Ilipokuja WERECU iliyoundwa na Serikali, mali zote zilitudi serikalini na watu wakaachwa hoi. Pili ni ile sera ya "even distribution of development". Hii iliwakwamisha sana, kwani hata kwenye ufaulu wa kwenda vyuoni, Wahaya wliachwa wakachukuliwa Wamang'ati na wengineo. Sera hii iliacha raslimal zikapelekwa kwa wasio nacho.

Ilifika wakati, Wahaya wakahamishia watoto Mwanza na kuwapa majina ya Kisukuma ili wasitambuliwe. Nakumbuka rafiki yangu aliitwa Ntemi Nangika huku ni mhaya. Tulisoma naye Sekondari Bukoba akiwa anatoka Magu.

Wakati wa kampeni ya uhujumu uchumi, enzi ya Mwalimu, Wahaya waliumizwa sana na Nsa Kaisi, enzi hizo mkuu wa mkoa. Ilifika wakati barabara za kwenda nchi jirani zikachimbwa mitaro watu wasifanye biashara.

Mambo mengi na mengine kama hayo yaliwakatisha tamaa sana Wahaya.
 
Prof. Tibaijuka ameibua hoja ambayo ameishadadia kwa takwimu kwa vigezo vya maendeleo ya kiuchumi ili kuweka msisitizo. Ameweza kuamsha uchokozi wa kifikra ili wana Kagera waweze kujipima wao wenyewe kupitia historia yao ya kimaendeleo.

Katika mambo ambayo yameathiri mno maendeleo ya wana Kagera ni chuki za wanasiasa dhidi yao. Hali iliyowatokea wana Kilimanjaro katika kipindi cha utawala wa JPM, ndicho ambacho kiliwakuta wana wa Kagera.

Walionekana kuwa ni jamii iliyokuwa imejaa wasomi na wenye hamu kubwa ya maendeleo, hivyo wanasiasa wakapata sababu ya kuwalaghai ili kuwachelewesha kimaendeleo kwa makusudi, kisingizio kikubwa ikawa wawasubiri wengine. Yaani zile jamii ambazo hazikuwa na wasomi wengi au maendeleo duni.

Wakati wana Kilimanjaro walipingana na uzwazwa huu kwa vitendo wao walikubaliana nao na hatimaye kujikuta imekula kwao mazima. Huu ndio ukawa mwanzo wa wasomi wa mkoa huu kuutelekeza mkoa wao, ili wapate sifa kutoka kwa wanasiasa wenye hila ya kupeleka maendeleo sehemu nyingine.

Prof. Tibaijuka kaibua mjadala, ni vyema watu wajikite kwenye hoja na sio kumshambulia yeye kama yeye kwa kigezo cha nini ambacho alikifanya alipokuwa na madaraka. Wana Kagera wengi wamejenga mahekalu ya gharama katika maeneo maarufu na nyeti karibu katika majiji yote hapa nchini.

Wengi wanamiliki mali nyingi na makampuni makubwa, lakini ni kwa nini hawapendi kuendeleza makwao. Prof. Tibaijuka karusha jiwe gizani, kwa hiyo yeyote litakaye mpata atoe kilio cha uchungu nini ambacho kinatakiwa kufanyika.

Not one, not two but all of them. Attack the matter and not personality.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Ebu fanya haraka urudishe ardhi ya Kyamyorwa watu wapate sehemu ya kulima. Milibinafsisha ardhi we na Mkapa nawe ukafakamia..
Kwanza takwimu hizi ni feki, na Ummy kabla ya kuhamia wizara nyingine, mkoa wa kagera umeonyesha kufikia kiwango cha ukusanyaji kodi.
2. Mwezi wa kumi na moja, watu walionyesha tambo za kupanuka miji midogo midogo mingi, hii ni dalili bora ya maendeleo
3.wakula wamebadirika wanalima vanilla hadi wachuuzi wanashindwa kuwalipa kwa wingi wa zao hili.
4. Samaki zimewaendeleza sana watu wa mwambao
5. Ugonjwa wa munyauko umebaki asilimia ndogo sana hivyo neema ya chakula imerudi
6. Kufufliwa meli mbili uchumi umebadirika, hata hivyo wingi wa mabasi ya mwanza bukoba yote yanajaa na yanaenda kila siku uje useme hakuna maendeleo twafa

7. Wingi wa magari na pikipiki huko vijijini umeongezeka sana
8. Majengo mazuri ya kisasa nyumba za tembe hakuna kwa sasa, huyu mama anatuzalolisha
9. Magari ya bia za pilsner na balimi yanapishana watu wameacha kunywa gongo wanabwia bia.
10. Ulimaji wa miti ya paini umeshamili na umewatoa sana
 
... sana! Ni ajabu kusikia mkoa wa Kagera ni mkoa masikini; ajabu mno! Mkoa ambao ni evergreen throughout the year kwanini uwe masikini? Dah!
 
Kinawaumiza Wahaya ni mbegu mbaya ya Ubaguzi ni watu ambao wanaakili lakini haziwasaidii wanabaguana mpaka KOO HII na KOO NYINGINE ukipangiwa kazi Bukoba umekwishaaa majungu masufuria wahaya ni WAMBEYA NAMBA MOJA KWENYE HII NCHI SIO NAWATUKANA FANYENI UTAFITI maana mtu mbaguzi mwenzake ni umbeya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…