Uchaguzi 2020 Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania

Status
Not open for further replies.
Unajua chanzo lakini mpaka kupelekea kuhamisha hao wahadhiri hapo chuoni? Issue ilikuwa waislam walikuwa wanataka wajenge msikiti kwenye sehemu waliopewa na uongozi wa chuoni hapo lakini baadae mpango ule ulisitishwa na makamu mkuu wa chuo mama Kabaka aliyekuwa waziri wa awamu ya nne na kupelekea kufumua uongozi mzima wa chuoni hapo kwa kuwaondoa baadhi ya walimu 11wenye iman ya kiislamu na kuteua wengine 11 baada ya seke seke hilo maguful alikuja kuzima hilo na hatimaye wanafunzi walipatiwa hitaji lao....sometimes tuwe wakweli waislamu wana hoja za msingi katika haya ila nahisi ni chuki zetu kwao ndio kunapelekea haya...
 
Hilo daraja la kwanza ni lipi ambalo waislamu hawapo? Mbona sometimes mnajitoa ufahamu kiasi hicho?
 
Historia huwa haizeeki hata hicho unachokisema pia kinaweza kuja kuwa sehemu ya historia!
 
Shida wa waislamu ni BAKWATA kugeuzwa kuwa shina la CCM
 
Kwa asilimia kubwa nakubaliana na huo waraka hasa maeneo yanayogusa maslahi ya jamii nzima.

Kwenye hili la uteuzi, ukiangalia pasipo fikra za udini, unaeza usilalamike. Eg walioondolewa hakukuwa na prof hata mmoja, na 6 kati yao hata phd hawana!!!
(Na kuna uwezekano kuwa hata hawa, awamu iliyotangulia waliteuliwa kwa upendeleo wa kidini tuu).

Walioingizwa: 7 ni profs, 4 ni phd holders.. hapo huoni tija kweli??

Na kwenye uonevu wa kuswekwa ndani, ni kweli.. ila mbona hawatajwi akina Mbowe na wenzake wanaorundikwa lupango Kila leo, wala Tundu Lissu aliyepigwa risasi lukuki na utawala huu huu??
 
Na wewe haupo sawa, wote mmepotosha hilo suala la UDOM
 
Shida wa waislamu ni BAKWATA kugeuzwa kuwa shina la CCM
Hapo mkuu ndo tatizo la waislamu linapokuja,ndio maana wanalipiga vita sana hili baraza kutokana na jinsi lilivyoundwa na hata jinsi linavyojiendesha kwake...kumbukumbu zangu kuna masheikh wengi wameeleza udhaifu wa hili baraza ikiwemo sheikh ILUNGA na wengio...

Hawa wabakwata nahisi wapo kimkakati na wanakula sahani moja na wataawala...yaani huu wanaraka nimeupenda kwa jinsi walivyo analyze mambo na kutoa mapendekeza nn kifanyike...mambo haya bakwata huwezi kuyakuta wao waambie kuna mgogoro wa kugombania msikiti asee watakuja hapo wakisindikizwa na maaskari walioshikilia mitutu...

Tuache ubinafsi na tutende yaliyo mema yenye kumpendeza Mungu,kwani dunia na vyote vilivyomo ardhini tutaviacha,maisha ya dunia ni starehe ya muda mfupi sna yatupasa kutengeneze kesho.
 
Na wewe haupo sawa, wote mmepotosha hilo suala la UDOM
Haya tuelezee wewe kuhusu usawa wa hili suala la UDOM.....

Kuna nyuzi humu kibao kuhusu suala hili,tafuta nyuzi za MISSILE of nation lakini pia hili suala nililifuatlia kiundani...nasubiri kupata ukweli wa jambo hili toka kwako mkuu
 
Acheni kuendekeza udini

Utakuwa mfaidika wa system iliyopo. Kula bata tu, lakini jaribu kufuatilia jinsi gani jamii ya upande mwingine inavyoathirika. Machungu haya yataendelea mpaka lini?

Jana mlisema hawajasoma, hivi mpaka leo bado hawajasoma? Mungu si Athumani, jaribuni kuangalia mataifa yaliyoendeleza tabia hizo yalipofikia.
 
Kweli Leo nimetoka gizani na kuletwa kwenye mwanga,nimetafakali sana,kumbe ndivyo tunavyoongozwa!Nimeamini siasa ni mchezo mchafu,tena ni jinamizi,ukimuona mwanasiasa muogope ni zaidi ya muuaji

Baba wa taifa katudanganya sana na hapa ndipo alipotufikisha. Eti anatudanganya alipokuwa anachagua baraza la mawaziri hakuwa anajua kuna waislam wangapi na wakristo wangapi? Mmmmmm mdini hatari yule aka Mtakatifu baba wa taifa, Saint JKY. Na huyu wa sasa ndio anafuata nyayo zake.

Akaendele kutudanganya eti tunapofanya sensa hatuhitaji kujua Dini zetu, akakitoa kipengele cha kutambulika kuwa mhesabiwa ni dini gani, (Japo duniani kote wanakipengele hicho, hata ulaya na Marekani - Gwajima alizitumia Takwimu hizo kueleza sura ya Ulaya ktk dini). Akisema anapotoa maendeleo haangalii Dini, eti hata anapochagua mawaziri haangalii dini - Upotoshaji. Pengi na huyu wa sasa atatueleza kuwa naye haangalii Dini
 
Kean kwa teuz hizo wakristo wamefaidi nini na waislamu wamekosea nini?

Kwan Kuna barabara au shule au hospital nk Za wakritu na Za waislamu?

Hapo sasa ndo watanzania wajue kwamba waislamu wana hiden ajenda na hizo teuzi

Bara bara, miradi ya maji, zahanati, vituo vya afya vinajengwa na kutumiwa na kila mtu
 
Waraka umegusia kansa ya udini inayotafuna Taifa hili
Waraka umeonyesha bila kupepesa macho udini uliokubuhu katika teuzi zilizofanywa na awamu hii.
Awamu hii inafanya yaleyale yaliyokuwa yakifanywa na Nyerere ya 80% to 20% rule kwamba kanuni isiyo rasmi ya utumishi nchini ambapo Wakiristo huwa ni 80% na Waislamu 20%.

Sijajua kwa nini maraisi Wakatoliki wakiingia madarakani huwa na nongwa sana dhidi ya Waislamu

Labda tukipata Wakiristo Waprotestant watakuwa fair Kidogo.
Utawala wa Mkapa ulikutana na resistance kubwa kutoka kwa Waislamu ukajikuta unafanya baadhi ya vitu kutuliza joto kwa mfano kuvunja na kuinda upya bodi ya Parole ambayo mwanzo ilisheheni Wakiristo watupu.

Kuwapa Waislamu chuo cha Morogoro lakini ikiwa ni kusawazisha malengo ya serikali yake kuwarudishia Wakiristo shule zao ambazo Serikali ilizitaifisha miaka ya 1960's na kuzifanya za serikali

Hata kuzitaifisha huko kulitokana na Nyerere kupigwa presha na Waislamu kuwa nao wanataka kusoma na kwa hiyo ni lazima awape elimu kama wenzao wakiristo walivyonufaika na mifumo ya elimu kutoka kwa kanisa lilikuwa linapewa kila aina ya msaada na serikali za wakoloni kwenye sekta ya elimu. Akakimbilia kutaifisha shule hizo ili kutuliza joto la madai hayo badala ya kujenga mpya kwa wingi.
 
Hapo sasa ndo watanzania wajue kwamba waislamu wana hiden ajenda na hizo teuzi

Bara bara, miradi ya maji, zahanati, vituo vya afya vinajengwa na kutumiwa na kila mtu
Hakuna cha hidden ajenda hapo, kama Wakiristu 80% wanapata ajira na teuzi huku waislamu wakipata only 20% maana yake keki ya Taifa kama vile mishahara, manufaa ya bima za Afya, Viinua mgongo na benefits nyingi zinazotokana na kufanya kazi serikalini zinakwenda kwa watu wa jamii moja zaidi, matokeo yake jamii hiyo inakuwa na maisha mazuri zaidi, wataweza kusonesha watoto wao kwenye shule bora zaidi na muendelezo huo wa jamii hiyo kuwa ju ya jamii nyingine utaendelea tu.

Lazima Keki ya Taifa igawanywe kwa wote kwa usawa. Wote tunalipa kodi, na wote tunalilinda Taifa hili.

Lazina fairness katika nchi iwepo!
 
Sijausoma huu waraka wote ila kuna maeneo napenda niyagusie kidogo;

Kwanza kuhusu hao wafungwa wote,Pili kuhusu hao wahadhiri,tatu kuhusu uwiano wa watumishi wa umma

Hayo maeneo yote hapo juu ukiyaangalia hasa yanaonesha kwamba waislamu wanakandamizwa kwa kiwango kikubwa sana ila je ni ugandamizaji wa kimfumo?Je kuna tatizo kuwa na wakristo wengi kuliko waislamu katika utumishi wa umma?Je Dini nayo iwe ni kigezo katika kufanya teuzi za viongozi?Kwa nini iwe kigezo.Je huoni kama kuna tatizo labda la Waislmu kutazama kila jambo katika miwani ya dini kiasi cha kujikuta wakiona patern flani ambayo haipo?

Mfano mzuri ni serikali ya Zanzibar ambapo majority ya Raia ni Waislam ila sio kwamba hakuna wakristu wapo ila ukiangalia muundo wa serikali kuanzia juu mpaka chini utakuta wamejaa waislamu.Ukiangalia kwa jicho la kidini utaona kwamba wakristu wanabaguliwa ila ukweli ni kwamba wakristo ni wachache.Nafikiri hata kwa huku Bara pia kuna weza kuwa na ukweli huu hasa kuhusu uhaba wa waislamu wenye Vigezo vyote ikiwamo,ujuzi,uwezo,utayari na uzoefu.Kama kunafikra kwamba kuhamishwa kwao kuna uhusiano na dini yao basi kunaweza pia kuwa na uwezekano kwamba walileta maswala ya udni katika kuendesha taasisi hio.Hilo linaweza kuwa limepelekea hali hio.

Kuhusu hao wafungwa,Je wamefunguliwa mashtaka kwa mujibu wa sheria gani?Walikamatwa tu nyumbani kwao wakiwa na wake zao wamelala au kulikuwa na mienenndo fulani ambayo haiko sawasawa au kauli tata.

Najua waraka huu ni mzito na Jamii ya uislamu inaweza kuchagua kutazama kila kitu katika miwani ya udini au kuchagua kuona fursa na kutafuta namna ya kushiriki katika uongozi kwa kujitokeza kugombea uongozi na kuchagua viongozi wenye uwezo na nia ya kujenga taifa
 
BAKWATA tatizo ni maslahi mbele badala ya kuweka maslahi ya waislamu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…