Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Sijausoma huu waraka wote ila kuna maeneo napenda niyagusie kidogo;
Kwanza kuhusu hao wafungwa wote,Pili kuhusu hao wahadhiri,tatu kuhusu uwiano wa watumishi wa umma
Hayo maeneo yote hapo juu ukiyaangalia hasa yanaonesha kwamba waislamu wanakandamizwa kwa kiwango kikubwa sana ila je ni ugandamizaji wa kimfumo?Je kuna tatizo kuwa na wakristo wengi kuliko waislamu katika utumishi wa umma?Je Dini nayo iwe ni kigezo katika kufanya teuzi za viongozi?Kwa nini iwe kigezo.Je huoni kama kuna tatizo labda la Waislmu kutazama kila jambo katika miwani ya dini kiasi cha kujikuta wakiona patern flani ambayo haipo?
Mfano mzuri ni serikali ya Zanzibar ambapo majority ya Raia ni Waislam ila sio kwamba hakuna wakristu wapo ila ukiangalia muundo wa serikali kuanzia juu mpaka chini utakuta wamejaa waislamu.Ukiangalia kwa jicho la kidini utaona kwamba wakristu wanabaguliwa ila ukweli ni kwamba wakristo ni wachache.Nafikiri hata kwa huku Bara pia kuna weza kuwa na ukweli huu hasa kuhusu uhaba wa waislamu wenye Vigezo vyote ikiwamo,ujuzi,uwezo,utayari na uzoefu.Kama kunafikra kwamba kuhamishwa kwao kuna uhusiano na dini yao basi kunaweza pia kuwa na uwezekano kwamba walileta maswala ya udni katika kuendesha taasisi hio.Hilo linaweza kuwa limepelekea hali hio.
Kuhusu hao wafungwa,Je wamefunguliwa mashtaka kwa mujibu wa sheria gani?Walikamatwa tu nyumbani kwao wakiwa na wake zao wamelala au kulikuwa na mienenndo fulani ambayo haiko sawasawa au kauli tata.
Najua waraka huu ni mzito na Jamii ya uislamu inaweza kuchagua kutazama kila kitu katika miwani ya udini au kuchagua kuona fursa na kutafuta namna ya kushiriki katika uongozi kwa kujitokeza kugombea uongozi na kuchagua viongozi wenye uwezo na nia ya kujenga taifa
Zanzibar asilimia 98 ni waislamu wakati Tanganyika Waislamu ni around 40% hadi 55%
Haiwezekani katika jamii yenye composition ya watu namna hiyo kila teuzi wao hawajawahi fika hata 30%, Yaani kila teuzi inayoinvolve watu zaidi ya watatu basi wao ni kiduchu tu siku zote.
Hapa lazima kuna namna, kuna mfumo in place katika awamu hii wa kuhakikisga Waislamu ni wachache katika teuzi