MUONGOZO WA SHURA YA MAIMAMU TANZANIA UCHAGUZI MKUU WA TAIFA OKTOBA 2020
Shura ya Maimamu wa Tanzania imetoa waraka unaohusu Uchaguzi Mkuu.
Katika waraka huu au muongozo huu kuna mengi ya kufikirisha sana kiasi mtu atajiuliza haya yanawezekana vipi kutendeka katika nchi inayojinadi kuwa inazingatia haki na usawa kwa wananchi wake wote na inapiga vita ubaguzi wa aina yoyote.
Katika mengi niliyosoma hili hapo chini nikilijua siku nyingi na limekuwa likinisikitisha sana.
Kwa kuwa waraka wamelieieza naona itakuwa vyema nikaliweka hapa kwa faida ya wasomaji:
Uadilifu I
''Januari 11, 2019, serikali ilifanya uhamisho mkubwa wa kushitukiza kwa wahadhiri na watumishi wandamizi katika Chuo Kikuu cha Serikali cha Dodoma-UDOM.
Waliohamishwa walikuwa 11, lakini wote walikuwa Waislamu:
Dk. Maryam Khamis (Director of Graduate Studies), Dk. Ibun Kombo (Political Science), Dk. Mwinyikombo Amir (Mwalimu wa Udaktari wa Binadamu), Dk. Yusuf Kambuga (College of Education), Dk. Masoud Masoud (Informatics) , Bw. Subira Sawasawa (Mkurugenzi Mkuu Rasilimali Watu), Bw. Mohamed Mwandege (Bursar/Mhasibu Mkuu), Bi. Aziza Gendo (Seniour Estate Oficer), Bw. Simba Omary (Senior Supplies Oficer), Bw. Wema Mbegu (Legal Oficer), Bw. Khamis Mkanachi (Mwalimu wa Idara ya Historia).
Barua zao za uhamisho hazikuonesha makosa katika utendaji wao wa kazi au uongozi. Pamoja na kutokuwa wakosaji, uhamisho wao uliambatana na udhalilishaji mkubwa, kunyimwa haki stahiki za uhamisho, kuhamishiwa katika nafasi za chini kinyume na hadhi zao.
Baada ya uhamisho huo, Serikali ilifanya uteuzi mwingine katika chuo hicho hicho cha Serikali.
Katika uteuzi huo walioteuliwa walikuwa 11, wote Wakristo: Prof. Leonard James Mselle, Prof. Adam B. Swebe Mwakalobo, Prof. Julius William Nyahongo, Prof. Justin Ntalikwa, Prof. Frowing Paul Nyoni, Prof. Odass Bilame, Prof. Ainory Piter Gasese, Dkt. Victor George Mareale, Dkt. Alex Shayo, Dkt. Calvin Swai, Dkt. Augustine Mwakipesile.
Kuhamisha wahadhiri 11, katika Chuo Kikuu si jambo dogo.
Vilevile kuhamisha Wahadhiri 11, wa dini moja (Waislamu) katika Chuo Kikuu ukaingiza wahadhiri 11 wa dini moja (Wakristo), na hao Waislamu 11, baadhi yao ukawatoa kabisa katika mfumo wa elimu kwa kuwapeleka sekta nyingine na zisizo lingana na hadhi zao si jambo dogo. Wala si hatua ya kitaalamu ya kuboresha mfumo wa Elimu wa Taifa.
Na wala si hatua ya kijinga bali ya werevu uliofurutu ada dhidi ya maslahi ya Taifa.
Hatuwa hiyo ni salamu nzito kwa jamii yao na Taifa kwa ujumla. (Ndio maana katika maoni yetu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tulipendekeza Katiba Mpya imtambuwe Mwenyezi Mungu na Dini liwe suala rasmi na la wazi katika uendeshaji wa nchi).''