Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio maana siutaki muunganoJibu ni Rahisi,Ni kwa sababu ya watu wenye fikra kama hizi za kusema wanaonewa bila kuchukua hatua kubadili hali halisi.Somesheni watoto wenu,Jitangazeni watu wawajueni kwamba mnaweza,Onyesheni umahiri wenu katika kufanya mambo.Badala ya kutumia muda mwingi kutaka kubebwa wakati hata mkibebwa hambebeki wekezeni katika ilimu ya watoto wenu...
Sawasawa,kwa hiyo sheikh wetu mkuu siyo mufti?!!Mufti ni cheo cha kielimu kinachahusiana na masomo ya sheria,na kutoa fatwa.
Hahaha, hivi are u serious on your comment?UDOM mkaamua mtoe waislam muweke wakristo! Hongereni nchi yenu hii wengine tupo kwa bahati mbaya
Swala la utakatifu wa Nyerere lisiwatie wehu.Hili tuwaachie watu na Imani yao.Kama alikuwa muumini wao wanayo haki ya kumtangaza mtakatifu kwa mujibu wa desturi zao au na hilo linakuuma?Nikwambie kitu kimoja ambacho unatakiwa kukifahamu - (Tena umegusa kwenye shina; Elimu) suala la kuiandaa jamii ya kesho ni ya serikali. Hii ikiwa pamoja na elimu ambayo ndio dira ya kupata ajira. Ni ujinga baada ya miaka 60 ya uhuru tukaendelea kulia na makosa aliyoyafanya mkoloni, huku ni kukosa akili. Sasa tulidai uhuru ili iweje? Au unafikiri ili tuendeleze utaratibu ule ule wa mkoloni, tukibadili rangi tu ya mtawala.
Tena umetaja Mmakabila kama wachaga - Huwezi amini kuwa mkoa wa Kilimanjaro unashule nyingi za sekondari kuliko Dar es salaam ambapo uwiano wa wakazi wa mikoa hiyo hata haikaribiani. Tena shule nyingi zaidi zimejengwa baada ya uhuru na mkoloni mweusi. Usishangae kwani hii ndio sera ya serikali ikiwalipa walimu na kuendesha shule hizo kwa kodi za wananchi wote...
Mkuu,Naona nikujibu hivi,Si kweli kwamba shule ni nyingi kilimanjaro kwa sababu ya serikali au kwa sababu ya mkoloni hapana,shule ni nyingi kule kwa sababu kuna muamko wa elimu na watu ni wachapa kazi. Ukiwajengea shule wanaleta watoto wao kuja kusoma.Huku unakodai wamebaguliwa ni kwamba wengi walikuwa ni wavivu tangu enzi za mkoloni na hivyo wakoloni hawakuona namna ya kuwasaidia.Hata shule chache zilizoko huko kwenu bada hampeleki watoto wenu na zinasommwa na wachaga na hao mnaowachukia.Nilifikiri utajibu kwanini shule za sekondari Kilimanjaro ni nyingi kuliko Dar es salaam. Kwa vile umeshindwa kujibu hilo, nachukulia kuwa - meseji sent.
Pili. Elimu hii tunayoisoma leo darasani tumeletewa na wakoloni, hata hao unaosema wanapenda kwenda shule leo hawakupenda wakati huo inaletwa. Soma kitabu cha Ngugi wa Thiongo " The river between". Ninachotaka kusema ni kwamba hata hao unaosema hawapendi kwenda shule, ni jukumu la serikali kuwawekea utaratibu na mikakati ya kuijenga jamii hiyo kwa ajili ya kesho yao...
Ukienda kwneye mkampuni yao hicho ni kigezo.Kuna vijana wengi sana nawafahamu wakristo ambao wanatumia majina ya kiislamu ili tu wapate kazi katika makampuni ya waislamu na ambako bado wananyonywa sana.Ma abdool sijui wakoje.
hivi kwenye sifa za kazi kipengele cha dini huwa kipo?
For sure,Cousin hii imani inapaswa kuongezwa kwenye orodha ya calamities!
hata huko ambako wao ndio majority hii shida iko
Tatizo liko kwenu hapo hapo, hata elimu wengi mmeweka mkazo kwenye elimu ya dini, kwenye elimu nyingine mmo lakini kwa kawaida sana.Titi...
Tutafanyaje inapokuwa waumini wa dini moja tu ndiyo wanakuwa na sifa za elimu, uxoefu, uadilifu, uchapakazi nk. kwa hiyo ndiyo wanaoongoza serikali na wengine wako nje?
Katika hali kama hii tunafanyaje?
Kalamu...Bila shaka yoyote, hivyo ndivyo vigezo halisi kabisa.
Vigezo hivyo pia vinaanzia chini kabisa, kuhakikisha kwamba mTanzania yeyote anapewa fursa sawa ya kuinua maisha yake bila upendeleo unaohusiana na ukabila, udini au uchochote, hii inaanzia katika huduma za elimu katika maeneo yote nchini.
Usisingizie serikali kuhusu suala la waislamu kutokusoma au kuwa na wasomi wachache. Tangu serikali ya awamu ya kwanza jitihada zilifanyika za kuhakikisha kwamba watoto wengi kama si wote wa Tanzania wanapata elimu ndio maana serikali ilitaifisha shule za dini za kikristo kuwa za serikali ili kuondoa kikwazo cha watoto wa kiislamu na hata wasiokuwa na dini kutopata nafasi ya kusoma maana serikali kwa wakati huo ilikuwa imerithi shule chache tu kutoka serikali ya mkoloni na uwezo wa kujenga shule mpya za kutosha ulikuwa ni mdogo sana.Nilifikiri utajibu kwanini shule za sekondari Kilimanjaro ni nyingi kuliko Dar es salaam. Kwa vile umeshindwa kujibu hilo, nachukulia kuwa - meseji sent.
Pili. Elimu hii tunayoisoma leo darasani tumeletewa na wakoloni, hata hao unaosema wanapenda kwenda shule leo hawakupenda wakati huo inaletwa. Soma kitabu cha Ngugi wa Thiongo " The river between". Ninachotaka kusema ni kwamba hata hao unaosema hawapendi kwenda shule, ni jukumu la serikali kuwawekea utaratibu na mikakati ya kuijenga jamii hiyo kwa ajili ya kesho yao.
Wakoloni walifanya hivyo kwa wachaga, wanyakyusa, wahaya nk. ni zamu ya serikali kuwa na utaratibu wa kuwainua huko ambako mkoloni hakufika au hakukuwekea utaratibu. Kama serikali iliendelea kule kule ambako mkoloni alikutengeneza, basi huo ni udhaifu mkubwa wa serikali iliyoongoza kwa miaka 60. Na ndio maana ni vigumu kujivunia uhuru wetu. Na ndio maana matabaka bado yanaendelea. Na ndio maana wahanga wataendelea kulalamika.
Uamini wangu katika kuyaandika hayo niliyoandika ni kwamba 'mteuzi' ni mtu mwenye uelewa na busara za kutosha kuweza kuona kwamba nchi yetu si ya kabila/dini moja na sifa nyingi nyingine.Kalamu...
Ulichosema ni kweli kabisa.
Lakini teuzi lazima zichukuliwe kwa tahadhari hasa katika maeneo ya dini na kabila.
Serikali ikijaza watu dini moja au kabila moja kwa kigezo kuwa hawa wana sifa zinazohitajika basi ijue inajenga matabaka na fitna kubwa na inajipalia makala.
Ikiwa hali ni hii hapa Tanzania au kwengineko basi jua kuna tatizo nchini na hiyo ni saratani mwishowe inaua.
Haiwezekani kuwa sifa ziwe kwa watu wa dini moja au kabila moja tu.
Bahati mbaya ninaposoma michango hapa jamvini hujiuliza kwa nini hawa wachangiaji wanashindwa kufanya uchambuzi na kuona tatizo?
Hili ni tatizo la vyuo vyetu au nini?
Hata kama shule ni moja tu.Inatosha kuleta mabadiliko kama ikitumika vizuri.Jaribu kufuatilia kwa karibu.Utaona kabisa kuna desturi kwa waislamu wengi kutohimiza ilimu kwa watoto wao,hasa wa kipato cha chini.Ukifuatilia zaidi utaona kuwa waislam wengi hutoa hadi majengo ya nyumba zao kuwa madrasa ya kufundisha elimu ya dini lakini hata kuwafundisha watoto elimu ya kawaida hakuna..
Kama story ya kijiweni vile. Haingii akilini. Kwa hiyo baada ya hapo waislamu wakasusa kupeleka watoto wao shule za serikali? Au Nyerere aliwakataza pia?Andoza,
Inaelekea hujui historia ya Waislam na elimu.
Unadhani kuwa Waislam walipuuza elimu ndiyo maana leo wako hivi...
Taifa haliwezi kuwa mateka wa historia miaka sitini na kuendelea.Inaelekea hujui historia ya Waislam na elimu.
Unadhani kuwa Waislam walipuuza elimu ndiyo maana leo wako hivi.
Walitolewa waislam 11 na msikiti kuvunjwa, hivi umelisoma bandiko tunalolijadili kweli?Hahaha, hivi are u serious on your comment?
Ukiambiwa uthibitishe hili utaweza? Hebu tuwekee ushahidi kamili hapa.
Daah,
Kwahiyo ilikuwa na uongo na ukweliUmeisoma lakini, au unafikia hitmisho hilo kwa vile imeletwa na watu wa dini?
Mimi nakushauri uisome. Nimeisoma karibu yote. Kuna baadhi nisiyokubaliana nayo, lakini sikuona "udini".
Wewe huo udini umeusoma wapi? Jaribu basi kuweka mfano wa udini uliouona wewe.