Andoza,
Inaelekea hujui historia ya Waislam na elimu.
Unadhani kuwa Waislam walipuuza elimu ndiyo maana leo wako hivi.
Kitu kimoja ambacho mimi nimekushindeni ni kuwa mimi nimetafiti historia ya Waislam kwa ujumla wake kuanzia kwa nini walikuwa mstari wa mbele kupambana na ukoloni na ilikuwaje baada ya uhuru Waislam wakawa tena katika mapambano na Julius Nyerere mtu waliyempokea na kumfikisha pale alipofika.
Nadhani haya mnasoma kila siku katika makala zangu.
Sababu ya Nyerere kuivunja EAMWS na kuunda BAKWATA ni kuwa EAMWS ilikuwa inajenga Chuo Kikuu na ilikuwa inajenga shule za msingi na sekondari majimboni kote Tanganyika baada ya kupitisha azimio la kushughulika na elimu lililopitishwa na Muslim Congress mwaka wa 1962 baada ya uhuru tu kupatikana.
Waislam hawakutakiwa waelimike walitakiwa wabaki katika hali ile ile waliyokuwanayo katika ukoloni.
Inaaminika pia Kanisa Katoliki lilikuwa nyuma ya njama hizi.
Haya yote nimeyaeleza katika kitabu cha Abdul Sykes na hii pia ndiyo sababu za kufanyika juhudi za kufuta historia ya Waislam katika TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mkakati ukawa kuwazuia vijana wa Kiislam kupata elimu na Wizara ya Elimu imehusika sana katika hujuma hii.
Prof. Malima alipokuwa Muislam wa kwanza kuwa waziri katika wizara hii alikutana na mengi na aliitahadharisha serikali kuhusu hatari hii na hiki ndicho kikawa kisa cha Prof. Malima kuchukiwa na kupendwa na Waislam.
Sina haja ya kueleza hujuma za Baraza la Mitihani kwa shule za Kiislam.
Sheikh Ponda aliongoza maandamano yasiyo na kibali licha ya vitisho vilivyotolewa na polisi kufikisha ujumbe serikalini kuwa Waislam wanahujumiwa katika elimu.
Unaweza ukajiuliza tena kwa nini Sheikh Ponda kwa nini si BAKWATA.
Ikiwa unataka kuyajua haya soma kitabu cha Abdul Sykes (1998), kitabu cha Prof. Hamza Njozi, ''Mwembechai Killings....'' (2000), lakini hiki kimepigwa marufuku.
Vinginevyo bila kujua historia ya kweli itakuwa tabu kwako leo kuelewa imekuwaje Shura ya Maimamu wanazungumza jambo zito la dhulma dhidi ya Waislam na BAKWATA iko kimya na kwa nini kwa miaka yote hiyo serikali imekuwa kimya katika tatizo hili la elimu kama Waislam wanavyolalamika.
Nahitimisha kwa kueleza hatari ya jambo hili la Waislam kudhulumiwa katika elimu.
Baada ya yaliyokuwa yanafanyika Baraza la Mitihani kufahamika na serikali ilipopata taarifa kuwa Waislam wataandamana kwa kudhulumiwa katika elimu ikatoa onyo kali.
Ilikuwa siku ya Ijumaa Msikiti wa Kichangani.
Baada ya sala Sheikh Ponda akasimama kuwahutubia Waislam waliojaa msikitini akaeleza kwa kutoa ushahidi kuhusu hii dhulma ya elimu.
Nje ya msikiti yalitanda magari ya polisi na helicopter zikizunguka juu.
Ndani ya msikiti walikuwapo makachero wengi na nje kwa ndani ya uzio wa msikiti.
''Ndugu zangu Waislam kama hatukuandamana kwa hili nini Waislam tufanyiwe ili tuandamane?
Mimi nitaongoza maandamano haya na nitakuwa mstari wa mbele...''
Sheikh Ponda alipomaliza kusema maneno haya aligeuka akawapa mgongo wale aliokuwa akiwahutubia akaelekea kibla akanyanyua mikono yake kuomba dua kumtaka Allah msaada.
Mimi nilikuwa chini nyuma yake na tape recorder yangu na camera nikirekodi na kupiga picha.
Hii picha niliyoweka hapa ni katika picha zangu ninazozipenda sana kupita kiasi.
''Tension,'' niliyoshuhudia ndani ya msikiti ilikuwa ya kutisha na nikasema ndani ya nafsi yangu kuwa ikiwa serikali hii itakuwa na ujinga ikaamuru askari wake wawashambulie Waislam kwa kukataa kudhulumiwa katika elimu basi leo damu itamwagika.
Maandamano yalipofika Jangwani zikaja taarifa kuwa Waislam wanaombwa waandamane kwa amani waelekee Kidongo Chekundu na pale viongozi wao watachukuliwa hadi Wizara ya Mambo ya Nje na waraka wao kwa serikali utapokelewa pale na Waislam wabakie pale hadi viongozi wao watakaporejeshwa Kidongo Chekunde na viongozi wao ndiyo watatoa amri ya Waislam kutawanyika.
Mzee wangu Mohamed Said,Nakubaliana na wewe kwamba mimi sio msomi wa Historia ya Waislam na huwa naheshimu sana jitihada zako za kutaka kuweka sawa historia ya nchi yetu mintarafu nafasi ya "Uislam" Sitaki kusema kwamba kuna ukweli au hamna ukweli katika maelezo yako na ya wengine ila nataka mimi na wewe tukubaliane kwamba Islamic radicalization ni tatizo hata ndani ya uislamu wenyewe.
Na hili ndilo tatizo kubwa linalokabili jamii nyingi duniani za kiislam yaani Religious extremism.
Pili mimi na wewetukubaliane kwamba wasomi wengi wa kiislamu hawautendei haki uislamu hasa katika eneo la kuhamasisha dhidi radical sentiments ndani ya uislam.Adui mkubwa wa uislamu na waislamu wenyewe kwa kushindwa kutenganisha harakati za kidini,harakati za kisiasa na harakati za kimaisha.Lazima tukubali kwamba zama zimebadilika na utamaduni wetu lazima ubadilika.
Hebu tutafakari kwa pamoja ni kwa nini nyerere alikosana na wale waislam waliompokea Dar es Salama?Je aliuchukia uislamu au kulianza kuibuka kwa radical sentiments na Nyerere hakuwa Tayari kuruhusu hilo litokee kwamaslahi makubwa ya taifa?Najua unaweza usikubali lakini maandiko yako yanaonesha kabisa kwamba hicho ndio chanzo."Nyerere alihofia radical sentiments ndani ya uislamu na akachukua hatua kudhibiti"Binafsi nafikiri ulikuwa uamuzi sahihi kwa kuzingatia mazingira.
Mzee wangu wewe umebahatika kupata ilimu kidogo ya kutosha,nafikiri kwa kiwango chako cha elimu tunaweza kusema ulikutana na mengi katika safari yako ili sidhani katika yote uliwahi kunyimwa elimu kwa sababu ya dini yako.Naamini kabisa ungebaguliwa wakati ukitauta elimu yako usingekuwa hapa ulipo.Nina hakika uliweka jitihada ndio maana uko hapa leo.Na hata maanikio yako uliyo nayo katika taaluma yako ni matokeo ya jitihada zako na bahati kidogo.
Jaribu kufikiri wakristu uliosoma nao tangu msingi na waislamu uliosoma nao halafu uangalie kwa kina kabisa kama kuna sehemu wakristo walibebwa zaidi ya waislamu(Achilia mbali zile personal connection ambazo ni kawaida katika maisha)Nazungumzia nyakati ambazo yupo muislam na mkristu wenye vigezo vyote sawa na mwislamu akaachwa mkristu akachukuliwa.Kama hayo matukio yapo ni machache sana kuweza kuwa kielelezo cha ubaguzi.
Ambianeni ukweli kwamba lazima muweke jitihada ya kupatia wanenu hamasa pamoja na elimu ya kutosha.Haitoshi tu kuwa mazamifu katika elimu akhera,elimu dunia pia ina nafasi yake.
Religious extremism ni tatizo sio tu kwa waislam bali kwa dini zote.Yote kwa yote Tanzania hatuna kiwango cha ubaguzi wa dini kama mnavyotaka kutuaminisha ingawa kuna weza kuwa na changamoto hapa na pale lakini haziwezi kufika kiwango cha kuitwa ubaguzi wa kidini tena "Systemic"