Hao hawatusemei waislamu wote.....hao Wala hawatambuliki KISHERIA kutusemea....
Muislam Mimi SIYATAKI HAYO WAYASEMAYO.....
Muislam mimi na wenzangu tulio wengi tunataka kuiona tume HIIHII iendelee kwani iko KISHERIA na haina dosari zozote.......
Waislam tunasemewa na BARAZA letu kuu BAKWATA......
WENGINE WANAKUWAGA WALE WACHOCHEZI WACHACHE.
Jumbe Brown,
Inaelekea hujui historia ya Waislam na elimu.
Unadhani kuwa Waislam walipuuza elimu ndiyo maana leo wako hivi.
Kitu kimoja ambacho mimi nimekushindeni ni kuwa mimi nimetafiti historia ya Waislam kwa ujumla wake kuanzia kwa nini walikuwa mstari wa mbele kupambana na ukoloni na ilikuwaje baada ya uhuru Waislam wakawa tena katika mapambano na Julius Nyerere mtu waliyempokea na kumfikisha pale alipofika.
Nadhani haya mnasoma kila siku katika makala zangu.
Sababu ya Nyerere kuivunja EAMWS na kuunda BAKWATA ni kuwa EAMWS ilikuwa inajenga Chuo Kikuu na ilikuwa inajenga shule za msingi na sekondari majimboni kote Tanganyika baada ya kupitisha azimio la kushughulika na elimu lililopitishwa na Muslim Congress mwaka wa 1962 baada ya uhuru tu kupatikana.
Kinara wa haya yote alikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na taasisi yake Daawat Islamiyya fi Tanganyika (Wito kwa Waislam wa Tanganyika).
Waislam hawakutakiwa waelimike walitakiwa wabaki katika hali ile ile waliyokuwanayo katika ukoloni.
Inaaminika pia Kanisa Katoliki lilikuwa nyuma ya njama hizi.
Haya yote nimeyaeleza katika kitabu cha Abdul Sykes na hii pia ndiyo sababu za kufanyika juhudi za kufuta historia ya Waislam katika TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mkakati ukawa kuwazuia vijana wa Kiislam kupata elimu na Wizara ya Elimu imehusika sana katika hujuma hii.
Prof. Malima alipokuwa Muislam wa kwanza kuwa waziri katika wizara hii alikutana na mengi na aliitahadharisha serikali kuhusu hatari hii na hiki ndicho kikawa kisa cha Prof. Malima kuchukiwa na kupendwa na Waislam.
Sina haja ya kueleza hujuma za Baraza la Mitihani kwa shule za Kiislam.
Sheikh Ponda aliongoza maandamano yasiyo na kibali licha ya vitisho vilivyotolewa na polisi kufikisha ujumbe serikalini kuwa Waislam wanahujumiwa katika elimu.
Unaweza ukajiuliza tena kwa nini Sheikh Ponda kwa nini si BAKWATA.
Ikiwa unataka kuyajua haya soma kitabu cha Abdul Sykes (1998), kitabu cha Prof. Hamza Njozi, ''Mwembechai Killings....'' (2000), lakini hiki kimepigwa marufuku.
Vinginevyo bila kujua historia ya kweli itakuwa tabu kwako leo kuelewa imekuwaje Shura ya Maimamu wanazungumza jambo zito la dhulma dhidi ya Waislam na BAKWATA iko kimya na kwa nini kwa miaka yote hiyo serikali imekuwa kimya katika tatizo hili la elimu kama Waislam wanavyolalamika.
Nahitimisha kwa kueleza hatari ya jambo hili la Waislam kudhulumiwa katika elimu.
Baada ya yaliyokuwa yanafanyika Baraza la Mitihani kufahamika na serikali ilipopata taarifa kuwa Waislam wataandamana kwa kudhulumiwa katika elimu ikatoa onyo kali.
Ilikuwa siku ya Ijumaa Msikiti wa Kichangani.
Baada ya sala Sheikh Ponda akasimama kuwahutubia Waislam waliojaa msikitini akaeleza kwa kutoa ushahidi kuhusu hii dhulma ya elimu.
Nje ya msikiti yalitanda magari ya polisi na helicopter zikizunguka juu.
Ndani ya msikiti walikuwapo makachero wengi na nje kwa ndani ya uzio wa msikiti.
''Ndugu zangu Waislam kama hatukuandamana kwa hili nini Waislam tufanyiwe ili tuandamane?
Mimi nitaongoza maandamano haya na nitakuwa mstari wa mbele...''
Sheikh Ponda alipomaliza kusema maneno haya aligeuka akawapa mgongo wale aliokuwa akiwahutubia akaelekea kibla akanyanyua mikono yake kuomba dua kumtaka Allah msaada.
Mimi nilikuwa chini nyuma yake na tape recorder yangu na camera nikirekodi na kupiga picha.
Hii picha niliyoweka hapa ni katika picha zangu ninazozipenda sana kupita kiasi.
''Tension,'' niliyoshuhudia ndani ya msikiti ilikuwa ya kutisha na nikasema ndani ya nafsi yangu kuwa ikiwa serikali hii itakuwa na ujinga ikaamuru askari wake wawashambulie Waislam kwa kukataa kudhulumiwa katika elimu basi leo damu itamwagika.
Maandamano yalipofika Jangwani zikaja taarifa kuwa Waislam wanaombwa waandamane kwa amani waelekee Kidongo Chekundu na pale viongozi wao watachukuliwa hadi Wizara ya Mambo ya Nje na waraka wao kwa serikali utapokelewa pale na Waislam wabakie pale hadi viongozi wao watakaporejeshwa Kidongo Chekunde na viongozi wao ndiyo watatoa amri ya Waislam kutawanyika.
Ukiingia kujadili mambo ya Waislam nawe huna elimu ya historia yao utatabika sana.
Hapo chini ni ''paper'' zangu katika somo hili:
1. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
2. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
3. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
4. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).