Nikwambie kitu kimoja ambacho unatakiwa kukifahamu - (Tena umegusa kwenye shina; Elimu) suala la kuiandaa jamii ya kesho ni ya serikali. Hii ikiwa pamoja na elimu ambayo ndio dira ya kupata ajira. Ni ujinga baada ya miaka 60 ya uhuru tukaendelea kulia na makosa aliyoyafanya mkoloni, huku ni kukosa akili. Sasa tulidai uhuru ili iweje? Au unafikiri ili tuendeleze utaratibu ule ule wa mkoloni, tukibadili rangi tu ya mtawala.
Tena umetaja Mmakabila kama wachaga - Huwezi amini kuwa mkoa wa Kilimanjaro unashule nyingi za sekondari kuliko Dar es salaam ambapo uwiano wa wakazi wa mikoa hiyo hata haikaribiani. Tena shule nyingi zaidi zimejengwa baada ya uhuru na mkoloni mweusi. Usishangae kwani hii ndio sera ya serikali ikiwalipa walimu na kuendesha shule hizo kwa kodi za wananchi wote.
Kifupi utaratibu wa maandalizi ya mwananchi yamefanywa kimakusudi kabisa huku wakijua kuwa wao watashikilia tu kuwa hawa hawana elimu.
Kwa ufahamu zaidi soma kitabu cha muandishi Sykes, ndio utaona mpango halisi. Ni lazima mwenendo huu ubadilike toka kwenye elimu, hakuna vipofu sasa hivi. Mambo yote yapo hadharani, humfichi mtu kitu.
J. K. Nyerere amewekwa kama candidate na kanisa katoliki ya kupewa U- Saint, si kwa bahati mbaya. Ni kwa vile katekeleza mpango mahsusi wa kuhakikisha kuwa kuna kikundi fulani kinapata upendeleo. Tunachosema ni kuwa yaliyopita ni ndwele tugange ya sas na yajayo.