Waraka wa wazi kwa mwanangu Koku

Waraka wa wazi kwa mwanangu Koku

Mzee mwenzangu yote uliyonena nimekubalian na wewe kwa % 100, lakini hapo kwenye bold na nyekundu, mh! nimeshawishika kuweka mtazamo wangu, si unajua wazee wanapowashauri watoto wao kuna wakati huchota busara kwa wazee wenzao! Nomba niweke yangu machache hapa ingawa najua sio wengi wenye mtazamo huo.

Kwa mimi ningemshauri mwenetu Koku asome kwa bidii sana na aweke nguvu zake kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa, kwani huo ndio ukombozi pekee uliobaki kwa kizazi hiki tulicho nacho. Siku hizi yatupasa sisi wazazi tuonyeshe mwamko mpya wa kuwashauri wenetu kuweka uzingativu zaidi katika kujiajiri na kuwekeza, hata kama itatokea kuajiriwa, iwe ni njia tu ya kuelekea huko kwenye kujiajiri au kuwekeza.

Nakushukuru sana kwa barua barua hii ya wazi na sio kwa Koku tu bali pia naamini wenetu kama kina Cantalisa, Smile, Kabakabana na wengineo watakuwa wamenufaika na waraka huu.......................
Asante Baba,
Ujumbe umefika na kwa wakati muafaka,
Inshaala kwa uwezo wa mungu tutayaishi mausia haya.
 
eti eh? Muhuni huyu TF!
Mara wewe,mara SL,mara smile,sasa tumchukulie vipi?

ngoja aje

unamwogopa?

caring mhuni?sijawahi kusikia!lol!

case inamuhusu yeye. Au naweza kumjibia mashtaka?

mjibie,si mmeo mtarajiwa?

mmmhwhuut!

Asante Mzazi kwa kulitambua hilo
TF, tumeshachukua binti, anza tu kukusanya senene.

we mrembo hulali? saa saba usiku ulikuwa unafanya nini,ulikuwa unamuwaza TF au yuko mpwapwa?

acha naye huyo,nasikia kapanda shabiby anaelekea mpwapwa.
Amen Amen naona kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa
 
Mwanangu Koku,leo nakuandikia waraka huu nikiamini utakusaidia leo na siku za usoni hata kama sitakuwepo duniani.
Mwanangu,najua unatamani uwe mtu mzima ikiwezekana hata leo ili uondoke nyumbani uwe 'huru' kufanya unavyotaka na kupanga muda wako unavyotaka.Ni kawaida kwa mtoto kuwa na hamu ya kuwa mtu mzima.Kumbuka kipindi utakachokuwa mtu mzima ni kirefu kuliko kipindi cha utoto,hivyo haina haraka,inshallah mola akujalie uhai mrefu.Kumbuka maamuzi unayoyafanya leo ndiyo yatakuamulia maisha yako ya baadae.
Hakuna jipya chini ya jua hili,mbinu za kupata mafanikio zishajulikana,jifunze mbinu hizo,zitakusaidia.Usifanye jambo eti kwa kuwa wengine wanafanya hivyo,tenda jambo ambalo nafsi yako imekubaliana nalo,usifuate mkumbo,fuata dhamira yako.Kwepa vishawishi vinavyoweza kukutia aibu wewe,familia yako na jamii inayokuzunguka,miliki maisha yako.Kizazi chenu ni cha dot.com,kizazi cha facebook,twitter,bbm na kadhalika,kuwa macho katika ulimwengu wa cyber ,usiwe mwepesi wa kuzoeana na watu wala kutamani ukutane nao,inaweza kuwa hatari.Usijiruhusu kuwa 'addicted' na dunia hii ya mtandao,be real.Jifunze dunia inakwenda je na usitumbukie katika mtego wa kufuatilia maisha ya watu wengine.
Mwanangu,litakapokuja suala la kutafuta kipato,kazi kwanza starehe baadae.Osha vyombo kabla ya kuangalia TV,fanya homework kabla ya ku chat na marafiki zako,hii itakujengea nidhamu siku za usoni,ila usiache kujiburudisha ukipata muda,msongo wa mawazo(stress) ni mbaya.Shibisha moyo wako kwa dua.
Litakapokuja suala la kuchagua taaluma ,ikiwezekana chagua taaluma ambayo unaipenda,fuata moyo wako usijilazimishe kufuata mkumbo au kunifurahisha mimi mzazi wako.Katika taaluma yako fanya kazi kwa bidii na penda kazi yako.Hakuna mwajiri huwa anamlipa mwajiriwa stahiki yake,jifunze kudai unachostahili kulingana na uwezo na mchango wako kwa mwajiri.
Nimekufundisha kuweka akiba,endelea kutunza unachokipata,usitumie zaidi ya kipato chako.Pesa zako ni zako,usiruhusu mtu mwingine akupangie matumizi ya pesa zako,labda iwe ni kwa majadiliano lakini si kwa shurti.Usicheze kamari,kuiba wala kujiunga na mipango kama ya DECI.Hakuna pesa ya bwerere,pesa hutafutwa kwa jasho,na kwa maana hiyo kamwe usiuze utu wako kwa ajili ya pesa,una uwezo wa kutafuta pesa kama walizonazo hao wengine na kwa njia halali.
Utakapoingia kwenye mahusiano,usiangalie wengine wanasema nini,angalia wanafanya nini.Kuna siku utatumbukia kwenye lindi la mapenzi na utajiuliza 'hivi huyu ndo Mr Right?'.Ataweza kuwa ataweza asiwe.Akikuumiza usilie kupita kiasi ,jikusanye nyanyuka na usonge mbele.Muda ndo dawa ya machungu ya mapenzi,jipe muda utasahau,usijiue kwa sababu ya mtu mwingine mwenye baba yake na mama yake ambaye mmekutana ukubwani.Ukiolewa kumbuka mmeo kamwe hawezi kuwa baba yako,never.
Kuwa na marafiki wachache lakini wa ukweli,kuna siku watakusaidia.Epuka kuwa na watu wanaokusifia tu,anayekukosoa ndiye bora zaidi hata kama inauma.Ogopa marafiki wambeya na wasengenyaji,hata wewe watakusengenya.
Katika maisha yako utakutana na vikwazo vingi,jifunze kutokuwa na haraka ya kutoa maamuzi,tatizo lala nalo,litolee maamuzi ukiwa umetulia.Mwanangu,mdomo uliponza kichwa,chunga sana ulimi,neno likishatoka mdomoni ni kama cement ikisha kuwa zege hairudi kuwa cement.
Mwanangu nakutakia maisha mema yenye baraka tele,na siku zote ujue ninakupenda sana hata kama kuna wakati huwa unaona nakukwaza,yote huwa ni kwa nia njema tu.
Baba yako,
Bishanga Abashaija
Dar es salaam
29/11/2011

wosia bomba sana Baba Koku! Hasa pale pa kudai haki na kutokukubali mapenzi yasimtawale na kumuumiza! Mwambie aunt yake nipo pia kwa ushauri zaidi anipm!
 
atakuwa kapokea ujumbe kwa mikono miwili , lakini ujamwonya juu ya mafisadi viwembe, ujamuonya asiwe Muigizaji wa Bongo filamu maana maadili yao yao wanayajua BWASWATWA tu.
 
Back
Top Bottom