Waraka wa Yanga ukiwasihi mashabiki wake kuiheshimu TFF na Serikali

😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Jibu lipo verse ya pili
 
Hiyo idara ya Habari na Mawasiliano yao siku hizi haina mtu, Bumbuli katupwa kapuni, yule kichaa mwingine nae yuko Segerea ya TFF.
 
Jamani wananchi, uongozi umeshasema tuiheshimu TFF na Serikali, ikiwa ni pamoja na kuwa watulivu kwa maamuzi yoyote yanayotolewa na mamlaka hizo za juu

View attachment 2318787
Ukute na wewe una Masitazi?
Safi sana Yanga kwa Waraka mzuri unaohimiza amani michezoni. Mlichoandika kina umuhimu mkubwa kwa mustakabali wa soka la Tanzania na wala hakuna mahali mmesema Mashabiki na wapenzi muwaogope watu au viongozi Fulani. Hata viongozi wa Simba na timu nyingine wenye akili wanahimiza ushabiki Na siyo uadui.
Kuhimiza heshima na amani mwanzo wa musimu si unyonge ni ushujaa.
 
Hakuna shabiki wa Yanga mwenye akili timamu, anaweza kuiheshimu TFF ya Wallace Karia! TFF iliyojaa double standard, na inayotumia nguvu kubwa kuwanyamazisha wale wote wenye mtazamo tofauti na huyo Karia.

Kuhusu mamlaka ya nchi, hilo halina shaka yoyote ile. Ila siyo hii TFF ya Msomali na ambaye ni kada wa ccm! Shabiki na mwanachama wa Coastal Union ya Tanga, na simba ya Dar es salaam.
 
Sijui ni akili yangu ndogo kushindwa kuekewa. Mbona mimi nimeona kama huo waraka una lengo la kutoa utisho kwa mamlaka kuelekea maamuzi magumu dhidi ya msemaji na Rais?

Nilivyoelewa mimi nje ya boksi ni kama Yanga wanawafikirisha watoa maamuzi kwamba maamuzi yeyote hasi dhidi ya viongozi wao yanaweza kuleta vurugu na ikitokea hivyo wao wamenawa mikono.

Jaribu kuusoma huu waraka alafu jaribu kutafakari sana unaweza kukiona nachokiona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…