Salaam!!
Natumia hii account kwa mara ya tatu leo kwasababu maalum..
Mada yangu leo inawahusu warembo wa JF, jamani huu ukurasa hauna warembo wazuri?
Nimebahatika kufahamiana na kukutana na watatu ndani ya miezi kama 18 iliyopita..
Kiukweli tuliishia tu kupiga story mbili tatu, hata urafiki wetu ukaishia.. Maandishi yetu na anonymity plus qualities tunazopresent kwa story zetu ni tofauti kabisa na tunavyoonekana..
Ni vema tuwe real tu kwakweli.
BTW, naongelea ukawaida wa mwanadada, siyo urembo.. Niliobahatika kukutana nao ni below par kwa ukawaida.
Anyone to prove me wrong?
Sidhani kama huu uzi unahitaji povu
Adios!!
Wewe mheshimiwa unakautoto, kauvulana AMA la una psychology problem.
1. Uzuri wa mtu mwanamke/mwanaume ni macho na akili za mhitaji. Hata siku moja umpendaye wewe sio lazima tumpende wengine, mzuri kwangu sio lazima awe mzuri machoni pako.
2. Mambo ya kukutana kwenu nje ya jukwaa hili ni privacy zenu, zao. Ni kukosa ukomavu wa akili kuleta mambo yenu balazani/ jukwaani. Maana yake huna staha, heshima wala busara. Hii inashiria hata mambo yako ya ndani may be ukayapeleka mitandaooni Siku moja.
3. Uliokutana nao memba wa jukwaa hili ndio haohao unakutana nao mitaani, masokoni, mahotelini nk. Ni watanzania walewale either wapo JF, Facebook, Instagram etc either wapo mitaani na hawajajiunga na social media yoyote.
I. Hizi Tabia za kitoto au kivulana bora kuziacha
II. Heshimu waliokuheshimu wakaacha majukumu yao wakaja kukutana/kusalimiana/kubadilishana mawazo nawewe.
III. Mtu yeyote unapokutana Naye sio lazima uanzishe mahusiano,
sio lazima akupendeze machoni pako nasio lazima akukubali...... akiringa, akikataa, akisita akinata ...... achana Naye, mpe uhuru wake, usimsimange kwa lolote.... rangi, uzuri, ubaya, maringo, ujuwaji nk.
Hataki mwache yawezekana anawake ndio demokrasia yenyewe.
IV. Kupanga nikuchagua. Usijioneshe kujua ya ubora na ubaya wa wengine.... hata wewe unakasoro zako. No one is perfect
Mambo ya faraghani yabakie hukohuko.
Tuheshimu utu wa mtu.... mwaume/mwanamke na faragha zake.
Tusifedheheshane kwa vitu vidogovidogo visivo na msingi wowote kimantiki na kimaadili.
Ukijiheshimu utaheshimika, ukidharau wengine nao watakudharau.