Mlinzi anadai kuwa alikaribishwa na Zainab. Lakini hamna ushahidi kama hii ni kweli. Ni kawaida ya mtu anaeshutumiwa na kosa kama hili kumgeuzia kibao mwanamke kwa kusema ndie aliyeanza kumtaka.
Lakini vile vile hoja ya Zainab kuwa jamaa aliyekuwa amekusudia kumbaka alikubali kwenda kutafuta kondomi ili aje ambake kwa usalama na yenyewe haijakaa vizuri.
Tatizo ni kuwa hawa ndugu zetu wa Nigeria wana sifa ya usanii. Binafsi sishangai kuwa Zainab alitaka mshiko ( haijathibitishwa) ili akae kimya. Ni tabia inayoendana na baadhi yao.
Huyu mlinzi anastahili adhabu hata kama alikaribishwa kwa kosa la kutoka kwenye lindo lake na kuanzisha uhusiano na wateja wa hoteli.
Amandla...