Warioba: Hatutachukua mawazo ya Katiba majukwaani wala kwa Mashinikizo ya Vyama vya Siasa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Jaji mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Mpya amewajia juu wanasiasa hasa wanaowaambia wafuasi wao waseme nini na mawazo mengine yanatolewa majukwaani kwa utashi wa kisiasa kwamba hawatayajumuisha na wasahau kama watayafanyia kazi.

Kadai kuna vyama vya siasa vinatoa mawazo kimaslahi ya kichama nao wasahau kwani Katiba ni ya Watanzania na si ya kichama!


===============================
Habari kwa kirefu
===============================

 
Katika hali ya kuonyesha Jaji ya Warioba ameelewa somo la Watanzania juu ya Muungano wa serikali mbili amepasua jipu kwa kusema "SITAPOKEA MAONI YA HELKOPTA" na akasisitiza kuwa alimtuma mbunge wake akawaambie Chama chake kuwa hatapokea maoni ya helkopta.

Itakumbukwa Mbowe mwenyekiti wa CHADEMA alitangaza hadharani kuwa CHADEMA watazunguka na helkopta kudai katiba!
 
badili title mood isomeke Warioba asema hatupokei maoni ya helkopter au ya kukaririshwa wanachama
 

Kwa hiki ulichokiandika hivi Jaji Warioba ana Mbunge? au umekurupuka tu.
 

Tunaweza kumuelewa vingine Jaji Waryoba, nadhani tumpe uhuru yeye na kamati yake kuwasikiliza wananchi badala ya wanasiasa kama alivyotanabahisha.
 
Kwa hiki ulichokiandika hivi Jaji Warioba ana Mbunge? au umekurupuka tu.

Tuwe na subira, ile tume siyo kama msajili wa vyama vya siasa mpaka tuanze kulumbana nayo.
 

Amesisitiza wanasiasa kuwaacha wananchi wajadili rasimu wenyewe
 
Nilikuwa najua kuwa hii tume ya Warioba italeta zengwe au kukumbana na zengwe na mwisho wake itakuwa malalamiko tele,mafanikio hakuna.

Kuna kila dalili hii tume italeta tu 'a standstill' ya kisiasa na Watanzania wasipate walichokitarajia.

1.suala la serikali tatu kugeuzwa ndo ajenda nambari one ya tume ilikuwa ni makosa makubwa..sasa kwakuwa CCM wanapinga na CHADEMA na upinzani wanaaunga mkono, limegeuzwa la kisiasa.

Busara ingetumika hata hili la serikali tatu liwekwe pending tungeanza na TUME HURU YA UCHAGUZI....hili lingerahisisha mno mengine yooote.....hasa kupata Tume huru kabla ya 2015.


Lakini kwa kugeuza 'serikali tatu' ndo main agenda ya Katiba mpya huku walioshikilia dola hawataki....basi dalili za kuchakachua mapendekezo mengine ya wananchi zipo waazi mno.

Sasa kuna mengi hatuyajadili kabisa.

1.Umri wa wagombea?nani alimwambia Warioba iwe miaka 40 kwa Urais?

2.serikali za mitaa,hazijaguswa kabisa kwa nini Mameya wasichaguliwe na wananchi?

3.Kwa nini wananchi wasichague mfano mkuu wa polisi?hasa wakuu wa polisi mikoani?

Na mengine mengi mno ambayo tulipaswa kuyajadili lakini hatuyajadili.

Issa Shivji alisema wazi...hii tume mbona haitoi transcript za hayo maoni ya wananchi?

Tuna uhakika gani hayo ni maoni ya wananchi? na sio ya Warioba na wenzie?
 
Saf sana Warioba kuna wanasiasa wanaewakaririsha wanachama wao maoni ya kwenda kuchangia. Hali hii itaharibu katiba nma haitakuwa katiba ya watanzania bali ya vyama. Bora Warioba kaliona.
 
Helkopta ni mbinu ya kuwafikia wananchi haitoi maoni jokes za warioba wakati mwingine ni dharau mbona hajasema habari za NAPE aliyemtukana matusi ya nguoni kumwambia amezeeka anangoja kufa
 
Mzee Warioba katumia falsafa ya juu, kwa watu wenye akili za haraka haraka watajua ni helkopta ya CHADEMA.
Jamani ikumbukwe kwamba CCM ndo wametoa mpaka waraka na kuwakaririsha wajumbe wao ili wapinge serikali tatu. Sasa kumekucha. Mzee Waryoba tunakuamini, tunakutegemea kwamba kwa zaidi ya miaka 50 ijayo LEGACY yako na tume itaendelea kuwepo. Usikubali mawazo ya kipuuzi ya kupinga mambo mazuri na mani ya wananchi wenyewe bila shinikizo la vyamya vya siasa.

Tunaamini wajumbe wote ni wajumbe wa MUNGU mwenyewemaana kama mtapoteza fursa ya kujiwekea LEGACY njema, mtawaachia wajukuu zenu sifa mbaya. HONGERENI SANA TUME YA WARYOBA.
 
Hivi mnajifanya mnaimani na huyo warioba wenu subirini mtamchukia kama gazeti la uhuru,

"Nchi ngumu hii"
 
Achebe mtu akikuita kichaa atakosea??
 
Natumaini ulikuwa tu ni UTANI wa kisiasa na sio MADONGO maala wale wenzetu wa kombati hawakawii wale
 
Ishakula kwa watawaliwa

"Nchi ngumu hii"
 
Warioba nae asijifanye kuwa na maamuzi juu ya kauli za wananchi. Wananchi ndo wataamua, na kama wakiamua wananchi na wakawatuma watumia Helicopter au kuwatuma wanaokaririsha , yeye ana tabu gani?
 
Umesahau amesema wala hataki mawazo ya helkopta ha ha haa
 
anayeamini kuwa katiba mpya italetwa na ccm ni mgonjwa wa akili.

exactly..
yeye ange concentrate na tume huru ya uchaguzi

masuala ya muungano uwe vipi yangefuata baada ya watu kuwa wamechagua
viongozi wao bila mizengwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…