Warioba: Hatutachukua mawazo ya Katiba majukwaani wala kwa Mashinikizo ya Vyama vya Siasa

Warioba: Hatutachukua mawazo ya Katiba majukwaani wala kwa Mashinikizo ya Vyama vya Siasa

Ni kweli kuna mambo mengi sana yameachwa kujadiliwa na kupoteza muda mwingi juu ya serikali 3 au la, Lakini pia huyu mzee tusimwamini saaana, maana hawa jamaa tangu zamani wanatabia ya kulindana, hata siku moja huyu mzee haitatokea kuwasaliti wenzake wa chama alichotokea yeye na kushika nyadhifa zote hizo. Ndugu zangu hebu tufungue akili zetu na tuwe makini sana, hawa watu wanaweza kutuchezea kwa kutumia Psychology, wamejipanga kabisa kuwa ionekane eti Warioba hayupo upande wowote kwa kushikilia msimamo wake tu, kisha akiana Nape wajitokeze kama wanavyotoka na kauli mbalimbali za kupinga serikali 3. Huyu mzee anaweza kushikilia msimamo wake kwa sura na maneno tu lakini matendo akatenda kama wanavyotaka wenzake, na hapo hakuna atakaye mnyooshea kidole cha lawama maana sote tutaamini kuwa huo ni msimamo wake kama tume.
 
Nilikuwa najua kuwa hii tume ya Warioba italeta zengwe au kukumbana na zengwe na mwisho wake itakuwa malalamiko tele,mafanikio hakuna.

Kuna kila dalili hii tume italeta tu 'a standstill' ya kisiasa na Watanzania wasipate walichokitarajia.

1.suala la serikali tatu kugeuzwa ndo ajenda nambari one ya tume ilikuwa ni makosa makubwa..sasa kwakuwa CCM wanapinga na CHADEMA na upinzani wanaaunga mkono, limegeuzwa la kisiasa.

Busara ingetumika hata hili la serikali tatu liwekwe pending tungeanza na TUME HURU YA UCHAGUZI....hili lingerahisisha mno mengine yooote.....hasa kupata Tume huru kabla ya 2015.


Lakini kwa kugeuza 'serikali tatu' ndo main agenda ya Katiba mpya huku walioshikilia dola hawataki....basi dalili za kuchakachua mapendekezo mengine ya wananchi zipo waazi mno.

Sasa kuna mengi hatuyajadili kabisa.

The Boss, uko sahihi lakini kinachosumbua hapa ni kitu kimoja, rasimu hii ni ya muungano ambao LAZIMA uwe defined utakuwa wa aina gani (serikali 1, 2 au 3?). Muungano huu kwa ujumla wake una mambo machache makuu (mengi kama ulivyosema serikali za mitaa n.k yataachiwa nchi husika - zanzibar & Tanganyika). Ndiyo maana ingekuwa ni maoni yangu mchakato huu ungeanza na kura ya maoni ya yenye two key questions: je muungano uendelee? Je uwe wa aina gani? Then ingefuatiwa na tume ya kuandaa rasimu mpya ya Tanganyika kwa sababu Zanzibar wanayo tayari, na mwisho wangemalizia na katiba ya muungano, kwa sababu mambo ya muungano yatakuwa machache lakini yatakayokuwa dira ya nchi mbili zilizoungana. Sasa hivi nimeona huko vijijini ninakopita kwenye shughuli zangu wananchi wengine wanafikiri baada ya rasimu hii na katiba kukamilika ndiyo imetoka (mfano wanasema kutakuwa na bunge dogo sana na hii safi sana!!) wanasahau kuwa hili ni bunge la muungano inawezekana la Tanganyika likawa kubwa tu. Kingine wale wenye kuwania madaraka lazima wapinge serikali tatu kwani waanza kuchanganyikiwa kipi kitakuwa cheo kizuri urais wa muungano au wa Tanganyika??
 
exactly..
yeye ange concentrate na tume huru ya uchaguzi

masuala ya muungano uwe vipi yangefuata baada ya watu kuwa wamechagua
viongozi wao bila mizengwe



Juxi nilicheka saana kuna mtu mkubwa Ana miaka ZAIDI 60 MTANGANYIKA na mbunge ccm aliniambia kuwa watu au mtu yeyote anaeshabikia na kutaka serikali mbili au tatu AKILI ZAO ZIMEGANDA!! JAWABU TOSHA NI SERIKALI MOJA TU HATA mie ninasema serikali moja ndio dawa ya kuwa na muungano imara ambae hataki ajiondoe ili tena ibaki serikali moja kila upande!cha ajabu HATA humu jf ni wachache Mnaongelea serikali moja je AKILI ZIMEGANDA Kama hao wanaowakaririsha au wanaotumia helicopter.??
 
Hapa Musitegemee ya kwamba mawazo yaliyotolewa na wananchi ndio yatakayo kuwepo bali Mutegemee mawazo ya mabosi wao waliowatuma kazi ndio yatakayokuwepo.Uchama na hasa UCCM ndio unaojibainisha zaidi katika mchakato huu wa katiba,matokeo yake tutapata katiba ya CCM na siyo ya Tanzania.POLENI SANA WATANZANIA
 
Ni kweli kabisa hata mimi nimeshituka juu ya hilo, maana muda nao ndo unakwenda hivyo huku wakikalia mjadala mmoja tu, na hayo maoni tunahitaji transcript ili tuamini, maana akina Nape wanatuzengua sana na kwakuwa wao wapo jikoni wanaweza kutuharibia katiba, na huyu mzee naye tusimuamini saaaana eti hawezi kuwasikiliza wenzie sio kweli. Hawa jamaa bwana tangu enzi zile kulindana ndio sera yao kuu. Huyu mzee hawezi kuwasaliti hata siku moja ni ujanja tu wa ki Psychology wanautumia anajidai kama vile hayupo pamoja nao kwa sura na kauli tu, lakini matendo atatenda kama wanavyotaka, kwa hali hiyo hatutaweza kumsonta kidole tutaamini kuwa huo ni msimamo wake tu!

tume ya katiba Sio warioba pekee,acha ubwege na unafiki.
 
MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, amekemea vyama vya siasa, kupenyeza maoni yao katika mabaraza ya Katiba huku vikikejeli wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Alisema hayo jana wakati akifunga mjadala wa siku mbili wa Rasimu ya Katiba, uliofanywa na Baraza la Katiba la Wabunge Wanawake mjini hapa.

“Nazungumza wazi hapa leo, vyama vya siasa ni taasisi, vifuate utaratibu vijadili kama Baraza la katiba la Taasisi na kutuwasilishia maoni yao, sisi Tume hatutachukua maoni ya jukwaani wala ya kwenye helikopta.

“Ukiangalia kwenye Katiba hii, utaona kuwa wananchi wanataka dira ya Taifa, dira ya uchumi, kisiasa na kijamii, lakini cha kushangaza mambo yanayozungumzwa ni machache tu ya madaraka, sasa haya mengine yataboreshwaje?,''alihoji.

Alitaka wanasiasa wasitafute mchawi katika mvutano na mjadala unaoendelea wa kipengele cha Rasimu ya Katiba kinachopendekeza serikali tatu, kwa kuwa kimetokana na maoni ya wananchi na si ya Tume.

“Hili jambo tujue Watanzania wote wamechangia, sisi Tume tumekusanya maoni, wapo waliotaka serikali moja, mbili, tatu na wengine hadi nne, tulichofanya ni kuchanganua maoni na kuyaweka kwenye Rasimu, naomba katika hili asitafutwe mchawi.

“Nasisitiza, hakuna mchawi, mimi nimepokea maoni kutoka kwa Watanzania na naamini walikuwa na akili timamu walipokuwa wakizungumzia suala hili, lakini pia suala la serikali tatu halikuzungumzwa na wananchi pekee, wapo pia viongozi walipendekeza, chonde tusitafute mchawi jamani,” alisisitiza.

Alionya vyama vya siasa vinavyofanya kampeni na kuingilia majadiliano ya mabaraza ya Katiba ya wananchi, kupenyeza maoni yao huko, kuwa Tume itayabaini kwa kuwa kwa sasa ina uzoefu wa kutosha.

Kukejeli wajumbe Warioba alisema amepokea pia malalamiko kutoka kwa wajumbe wake ambao walidai kuwa tangu kutoka kwa Rasimu hiyo, wamekuwa wakikejeliwa na kuhusishwa moja kwa moja na yaliyomo.

Alisema wajumbe walionesha kufedheheshwa na kejeli hizo kwa kuwa kazi waliyofanya ni kukusanya maoni ya wananchi, kuyachanganua na kutengeneza Rasimu inayoonesha dira ya nini Watanzania wanataka.

“Nimewaambia wasiwe na wasiwasi, wafanye kazi kwa moyo mmoja, ukifanya kazi ya Taifa lazima ubezwe na hii si mara ya kwanza, hata tulipoanza tulikejeliwa na kubezwa, jambo la msingi ni kuhakikisha wanafanya kazi yao kwa juhudi na weledi,” alisema.

Mambo yaliyoachwa Wakati Tume ikikusanya maoni, Warioba alisema katika eneo la elimu wananchi walitaka shule za kimataifa zifutwe, kwa kuwa zinasababisha matabaka ya elimu kwa watoto wa walionacho, viongozi na watoto wa wananchi wa kawaida, jambo ambalo halileti usawa.

Alisema katika afya, pia wananchi walipendekeza safari za viongozi na wagonjwa wengine nje ya nchi kwa matibabu zifutwe, kwa kuwa wananchi wengi wasio na uwezo hupoteza maisha katika hospitali za nchini, jambo ambalo pia linasababisha matabaka.

“Sasa haya na mengine mengi kama vile kwenye kilimo, wakulima kudai kuwa wanatengwa na wafanyakazi, kwamba wafanyakazi wanapewa kipaumbele sana, ndio yanayotakiwa kujadiliwa na kuboreshwa, ili kupatikana Katiba itakayohakikishia Watanzania wote usawa na haki,” alisema.

Alisema hatua iliyobaki katika kujadili Rasimu ni ndogo na kushauri Watanzania kuwa huu si muda wa kulumbana, kusemezana na kutafuta uchawi, bali kuheshimiana na kupeana fursa ya kutoa maoni yatakayotengeneza Katiba yenye manufaa kwa wote.

Awali akimkaribisha Jaji Warioba kufunga mjadala huo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake, Anna Abdallah, alisema Baraza lao lilijadili masuala ya jinsia na yanayosababisha ukatili dhidi ya mwanamke ili yapigwe marufuku na kuingizwa kwenye Katiba hiyo ili yatambulike kisheria.

Pamoja na hayo, kiongozi huyo alizitaka taasisi zote zinazotambulika na kukubalika kisheria, vikiwamo vyama vya siasa, kufuata utaratibu wa kujadili Rasimu na kuwasilisha maoni yao kwa Tume, kwa kuwa tume haitachukua wala kuzingatia maoni ya majukwaani.

Kwa hisani ya Habarileo.
 
Watanzania tunapenda sana kujadili kwa nguvu zote vitu vidogo ambavyo pia vina zero au negative impact katika maisha yetu.

Kwa sasa inavyoonekana swala la kujadili rasimu ya katiba tumeliacha kwa vyama vya siasa kana kwamba vyama vya siasa ndiyo dira yetu mbadala katika maisha yetu ya kila siku. Vyama navyo kwa ubinafsi wake, vimebaki na ajenda mbili tu mezani ambazo ni muundo wa serikali katika muungano na pia kupiga vijembe mapendekezo ya vyama vingine vya siasa

Kinachofanyika ni chama kimoja kuanza kuchambua mapendekezo ya chama kingine na kuyapiga rungu la maneno ya kejeri na dharau bila hata wao kujenga hoja ya mapendekezo yao na jinsi yatakavyolinufaisha taifa kwa ujumla katika miaka 50 ijayo.

Vyama vinatumia muda mwingi kupitia mapendekezo ya vyama vingine vya siasa ili kujenga hoja hasi za kisiasa kwa mtaji wa kisiasa kwa mapungufu katika mapendekezo ya chama kingine cha siasa bila hata kutoa hoja angalifu kuhusu manufaa ya mependekezo yao kitaifa ambayo yatapambana na mazingira ya miaka mingine 50.

Huwezi kujadili rasimu ya katiba kama taasisi kwa kupitia kipengele na kipengele kwenye mikutano inayochukua masaa mawili katika majukwaa ya kisiasa ambapo wasemaji wanakuwa ni viongozi wa vyama pekee achilia mbali kwenye helikopta kama Mzee Warioba alivyodokeza.

Mikutano katika majukwaa ya siasa haiwezi ikawa ni sehemu mwafaka katika majadiliano zaidi ya kuwa ni sehemu ya kutoa matamko na mapendekezo yasiyojadiliwa kiundani zaidi ya kusikilizwa.

Political parties must act kama taasisi zingine na siyo ku-monopolize majadiliano ya rasimu ya katiba. Vyama vya siasa ni taasisi zenye haki sawa kama zilivyo taasisi zingine zinazotambuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 18 (6) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ambapo Taasisi, Asasi na Makundi ya Watu wenye malengo yanayofanana yameundwa ili kuijadili rasimu ya katiba katika mabaraza ya katiba.

Haiwezi kupatikana katiba nzuri na endelevu kama wananchi hawako SERIOUS katika maswala ya msingi katika maisha yao.
 
Huyu mzee sasa anafikiri inaandikwa katiba ya ukoo wake.
 
Sasa watasema WARIOBA ni CHADEMA maana ukitetea wananchi au ukisema ukweli unaambiwa wewe ni chadema alafu unabambikiziwa kesi ya ugaidi.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Saf sana Warioba kuna wanasiasa wanaewakaririsha wanachama wao maoni ya kwenda kuchangia. Hali hii itaharibu katiba nma haitakuwa katiba ya watanzania bali ya vyama. Bora Warioba kaliona.

Ni kweli kabisa wengine wamedriki hadi kutoa waraka wa kuwaelekeza wananchi cha kufanya utafikiri wananchi ni mazuzu ambao hajui cha kufanya.
 
amenukuliwa na vyombo vya habari akisema “Nazungumza wazi hapa leo, vyama vya siasa ni taasisi, vifuate utaratibu vijadili kama Baraza la katiba la Taasisi na kutuwasilishia maoni yao, sisi Tume hatutachukua maoni ya jukwaani wala ya kwenye helikopta."-Jaji Warioba.
 
amenukuliwa na vyombo vya habari akisema “Nazungumza wazi hapa leo, vyama vya siasa ni taasisi, vifuate utaratibu vijadili kama Baraza la katiba la Taasisi na kutuwasilishia maoni yao, sisi Tume hatutachukua maoni ya jukwaani wala ya kwenye helikopta."-Jaji Warioba.

unaweza kuviorodhesha?
 
Huyu mzee si tumeambiwa na Nape kuwa anasubiri kufa...
Hope wale 2.6 milioni aliwafikia Kinana Jangili hakukuwa na jukwaa huko.
 
Katiba ni inclusive lazima akubal kukusanya maoni kwa njia tofauti ili mradi uwafikie wengi. Asipokuwa mwangalifu inaweza kukataliwa kwenye kura ya maoni ikawa kazi bure
 
Hiyo katiba anataka kuitengeneza kibabe.!!
 
Huyu mzee Nape ndo anajua kuwa ni lini hatma yake..Ila mzee Warioba maoni yaliyokusanywa kwenye hifadhi za tembo za Serengeti,Ngorongoro,Mikumi,Ruaha,Mkomazi,"Manyara na Selous utayachukua? maana nasikia eti yako milioni 2.6!!
 
kwani sheria inasemaje kuhusu namna ya kuchukua maoni
 
Back
Top Bottom