Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wenzetu kenya waliipata baada ya miaka 20 ya vuta nikuvute. labda sisi itakua miaka 10.anayeamini kuwa katiba mpya italetwa na ccm ni mgonjwa wa akili.
Warioba hoja ya serikali tatu imegonga mwamba.
Ushauri: Rasimu ya pili uje na serikali mbili kabla hujaabika mbeleni.
Game over.
Nataka kujua kutoka kwa warioba kipi kije mwanzo ni katiba ya muungano au katiba ya tanganyika,cjawahi kuona gari ya punda kuwepo mbele punda mwenyewe yupo nyuma.
Warioba hoja ya serikali tatu imegonga mwamba.
Ushauri: Rasimu ya pili uje na serikali mbili kabla hujaabika mbeleni.
Game over.
utakuwaje na katiba ya Tanganyika wakati Tanganyika haipo?ni lazima kuwe kwanza na katiba ya Tanzania inayoitambua Tanganyika ndipo utakapoweza sasa kuunda katiba ya Tanganyika
Big up papaa Warioba. Katiba ni ya Watanzania! Maoni mliyokusanya na kuya summarize kwenye rasimu ni ya watanzania na zoezi lote la Katiba ni la Watanzania. Heko kwa msimamo usioyumba!!Jaji mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Mpya amewajia juu wanasiasa hasa wanaowaambia wafuasi wao waseme nini na mawazo mengine yanatolewa majukwaani kwa utashi wa kisiasa kwamba hawatayajumuisha na wasahau kama watayafanyia kazi.
Kadai kuna vyama vya siasa vinatoa mawazo kimaslahi ya kichama nao wasahau kwani Katiba ni ya Watanzania na si ya kichama!
Ni kweli kabisa hata mimi nimeshituka juu ya hilo, maana muda nao ndo unakwenda hivyo huku wakikalia mjadala mmoja tu, na hayo maoni tunahitaji transcript ili tuamini, maana akina Nape wanatuzengua sana na kwakuwa wao wapo jikoni wanaweza kutuharibia katiba, na huyu mzee naye tusimuamini saaaana eti hawezi kuwasikiliza wenzie sio kweli. Hawa jamaa bwana tangu enzi zile kulindana ndio sera yao kuu. Huyu mzee hawezi kuwasaliti hata siku moja ni ujanja tu wa ki Psychology wanautumia anajidai kama vile hayupo pamoja nao kwa sura na kauli tu, lakini matendo atatenda kama wanavyotaka, kwa hali hiyo hatutaweza kumsonta kidole tutaamini kuwa huo ni msimamo wake tu!Nilikuwa najua kuwa hii tume ya Warioba italeta zengwe au kukumbana na zengwe na mwisho wake itakuwa malalamiko tele,mafanikio hakuna.
Kuna kila dalili hii tume italeta tu 'a standstill' ya kisiasa na Watanzania wasipate walichokitarajia.
1.suala la serikali tatu kugeuzwa ndo ajenda nambari one ya tume ilikuwa ni makosa makubwa..sasa kwakuwa CCM wanapinga na CHADEMA na upinzani wanaaunga mkono, limegeuzwa la kisiasa.
Busara ingetumika hata hili la serikali tatu liwekwe pending tungeanza na TUME HURU YA UCHAGUZI....hili lingerahisisha mno mengine yooote.....hasa kupata Tume huru kabla ya 2015.
Lakini kwa kugeuza 'serikali tatu' ndo main agenda ya Katiba mpya huku walioshikilia dola hawataki....basi dalili za kuchakachua mapendekezo mengine ya wananchi zipo waazi mno.
Sasa kuna mengi hatuyajadili kabisa.
1.Umri wa wagombea?nani alimwambia Warioba iwe miaka 40 kwa Urais?
2.serikali za mitaa,hazijaguswa kabisa kwa nini Mameya wasichaguliwe na wananchi?
3.Kwa nini wananchi wasichague mfano mkuu wa polisi?hasa wakuu wa polisi mikoani?
Na mengine mengi mno ambayo tulipaswa kuyajadili lakini hatuyajadili.
Issa Shivji alisema wazi...hii tume mbona haitoi transcript za hayo maoni ya wananchi?
Tuna uhakika gani hayo ni maoni ya wananchi? na sio ya Warioba na wenzie?