Warioba: Hatutachukua mawazo ya Katiba majukwaani wala kwa Mashinikizo ya Vyama vya Siasa

Warioba hoja ya serikali tatu imegonga mwamba.
Ushauri: Rasimu ya pili uje na serikali mbili kabla hujaabika mbeleni.
Game over.
 
Umekunywa viroba vy a kwenye friji ndo madhara hayo
 
Nataka kujua kutoka kwa warioba kipi kije mwanzo ni katiba ya muungano au katiba ya tanganyika,cjawahi kuona gari ya punda kuwepo mbele punda mwenyewe yupo nyuma.
 
Wala usihofu, mara zote mfa maji haishi kutapa tapa. Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu. Wala usogope maana Waryoba si mjinga aharibu LEGACY yake kwa vizazi na vizazi eti kwa kuwafurahisha kina Nape, Ndugu yangu TUME HURU ya Uchaguzi ni suala la kuleta sheria Bungeni na kujadiliwa na kupitishwa tu, Wewe wasikilizie tu utakuja kuelewa baadaye.
 
Ccm hawawezi kuleta katiba yenye tija kwa taifa hili, ni mpaka tufanye ya misri, vijana walio ccm wapo kwenye mrija wa kutoa asali na maziwa wanakula mpaka kusahau kwamba kuna wenye njaa, so wao kwanza mengine potelea mbali
 
Warioba yupo vizuri sana....ni watu tu hawajamwelewa....nikiicheki ile rasimu ni nzuri hayo yote imeyajibu vizuri sana...
 
Watanganyika hamna pa kutokea mwaka huu jiti limewaganda,zanzibr yenye mamlaka kamili lazimaa...
 
Nimependa msimamo wa huyu mzee.......ila kwa uwezo wake ulivyo mkubwa akicheka na mambumbu km akina nape ntamshangaa sana...
 
Warioba hoja ya serikali tatu imegonga mwamba.
Ushauri: Rasimu ya pili uje na serikali mbili kabla hujaabika mbeleni.
Game over.

Serekali 2 zipi?
 
Jaji Warioba hana matatizo yeye na tume ya katiba wako sawa kabisa. Wenye matatizo ni nyie watumwa wa wanasiasa.

Ukweli upo palepale katiba si ya vyama ni ya wananchi
 
Nataka kujua kutoka kwa warioba kipi kije mwanzo ni katiba ya muungano au katiba ya tanganyika,cjawahi kuona gari ya punda kuwepo mbele punda mwenyewe yupo nyuma.

utakuwaje na katiba ya Tanganyika wakati Tanganyika haipo?ni lazima kuwe kwanza na katiba ya Tanzania inayoitambua Tanganyika ndipo utakapoweza sasa kuunda katiba ya Tanganyika
 
utakuwaje na katiba ya Tanganyika wakati Tanganyika haipo?ni lazima kuwe kwanza na katiba ya Tanzania inayoitambua Tanganyika ndipo utakapoweza sasa kuunda katiba ya Tanganyika

Unajua maana ya neno tanzania?
 
"Nlimwambia mbunge wangu Mdee akawaambie hatutapokea maoni ya Helcopter" Warioba
 
Big up papaa Warioba. Katiba ni ya Watanzania! Maoni mliyokusanya na kuya summarize kwenye rasimu ni ya watanzania na zoezi lote la Katiba ni la Watanzania. Heko kwa msimamo usioyumba!!
 
Kweli siku itakuja tu hao CCM tutaweka jina lao kwenye National Archieve kwani watafutika tu na kuiacha Tanganyika kwa wananchi wenyewe. Time will tell.
 
Ni kweli kabisa hata mimi nimeshituka juu ya hilo, maana muda nao ndo unakwenda hivyo huku wakikalia mjadala mmoja tu, na hayo maoni tunahitaji transcript ili tuamini, maana akina Nape wanatuzengua sana na kwakuwa wao wapo jikoni wanaweza kutuharibia katiba, na huyu mzee naye tusimuamini saaaana eti hawezi kuwasikiliza wenzie sio kweli. Hawa jamaa bwana tangu enzi zile kulindana ndio sera yao kuu. Huyu mzee hawezi kuwasaliti hata siku moja ni ujanja tu wa ki Psychology wanautumia anajidai kama vile hayupo pamoja nao kwa sura na kauli tu, lakini matendo atatenda kama wanavyotaka, kwa hali hiyo hatutaweza kumsonta kidole tutaamini kuwa huo ni msimamo wake tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…