Warioba:Tanganyika ina shutumiwa kwa kuvaa koti la Muungano na kufanya Tanzania ndiyo Tanganyika

Huwezi kuwaridhisha wazanzibari ni watu wenye kupenda malumbano. Zenj kuunganika na nchi kubwa ya tanganyika, si lazima tanzania ionekane kama ndio iliyokua tanganyika? ndio maana waasisi wakaona lazima zanzibar iendelee kua na utambulisho wake kwa kua na serikali yake ambayo hakika ina strong autonomy. Mfumo wa serikali tatu hakika hauna maslahi kwa zanzibar ila unatimilisha hatua muhimi kwa wale wanzibari wenye nia ya kuvunja muungano.
 

Alilazimika kutowa vidonge vichungu ili ubishi ukome!
 
Tutakuwa viziri mjini hapa kwa ving'ora vya misafara ya maraisi wa 3.....sasa wakiwa watembezi kama huyu bado watakuwa wanagongana angani

Kwa vile makao sasa hayatakuwa pahala pamoja basi kutakuwa hakuna mgongano, Rais wa Zanzibar atakuwa hana haja ya kupiga ripoti kwa Bwamkubwa kule magogoni na Slaa atafanya maskani yake kwao Moshi!
 
Umeishawahi kaa na wazanzibari mkaongea kuhusu muungano ukasikiliza maoni yao?

Unataka kuniambia Watanganyika hawataki kuongozwa na kitu serikali? Wanapoilaumu na kuiponda serikali ni kwa vile serikali haina cha manufaa kwao, hali hiyo sawa na muungano huu kwa zanzibar na ndio maana wanataka kuwepo na mkataba.
 
Huu muungano hauna maslahi kwa Tanganyika ipigwe kura ya maoni ili uvunjiliwe mbali...na zanzibar haiwezi kuwa alqaeda cos ni ka nchi kadogo US atakatumia drones 3 tu kwishney....serikali tatu ni mzigo kwa walipa kodi kwa nchi masikini kama tanzania....muungano uvunjwe tu asap.
 
tunazunguka sana ila suluhisho ni serikali moja na znz iwe mkoa rasmi au muungano uvunjwe tukutane EAC,kwa hali hii matatizo yatajirudia tena na znz wataendelea kulalamika wanataka mamlaka kamili

Mambo huenda taratibu hakuna haja ya pupa!
 
Marais 3!!!!!! what a nice chance to become a president one day


Migogoro ndani ya vyama itapunguwa mfano CDM Kabwe atatupwa Zanzibar, Slaa Bara na Mbowe Muungano. Mrejesheni 'msaliti' wenu, sasa kiini cha ugomvi kishapata suluhu!
 

Hivyo bwanamkubwa unadai kutaka kuridhisha mtu kwa kitu chake mwenyewe? Ama kweli watu wengine hamueleweki, kwani mtu kutaka chake uungwana si kumpa tu.
Kwani Wazanzibar wanadai kitu gani kutoka Tanganyika? wanachodai mamlaka ya Zanzibar na Watanganyika hiyari yao na nchi yao.
 
Ndugu yangu Nguruvi3 uko wapi? Unaonaje maneno ya Jaji Warioba?
 
Nitaraji kuona kuinuliwa kiuchumi zaid. Sasa madaraka zaidi. Elimu Afya hakuna kitu. Mawaziri na Wabunge mishahara kwao na idadi yao ni wangapi. Mishahara Walimu na Waganga. Mapinduzi ya Joachim ni bora kuliko hayo madaraka lukuki eti serikali 1+1=3? Mh sielewi
 

Lakini nimemsikia mh Rais, akisema wadau watakaoteuliwa kwny Bunge la Katiba wakae kama team, waweke maslahi ya Taifa mbele,ushindani wa kivyama wauweke pembeni ili kulivusha Taifa letu. Ametumia maneno ya hekima na kwa hakika nilimuona anaongea kwa mwenekano akiwa na hisia kuonyesha anachoongea anamaanisha nia yake ya dhati kutupatia katiba, Legacy muhimu na kubwa ndani ya utawala wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…