Hizi hassle zote za nini?. Kwani nani amesema wananchi wanataka muungano?.
kwa mazingira yalivyo kwa sasa nchini, serikali tatu ni njia ya kuelekea katika uvunjifu wa Muungano wakati huo huo serikali mbili kwa sasa wala hazina hata mandate ya Watanzania wengi.
Kwa nini kama nchi mbili tunapita njia ndefu yenye gharama kubwa za kisiasa na kiuchumi wakati kuna njia fupi isiyo na gharama kubwa kama hizo!.
Kura ya maoni kuhusu kuwepo muungano au hapana ni mwarobaini kisiasa na bila hivyo, ni kuwalazimisha wananchi wakubali au kukataa serikali tatu huku wameziba options zingine za serikali moja, mbili, etc.
Itakuwaje wananchi au bunge likikataa hii Rasimu ya Katiba hasa kipengele cha aina ya serikali?.
Ndiyo maana tume ya Jaji Warioba inataka iendelee kuwepo hata wakati wa mchakato wa bunge la Katiba na kura ya maoni kwa sababu ulaji bado uko mezani kwa maana kuwa, wanafahamu kuna uwezekano mkubwa baadhi ya vipengele vya Rasimu ya Katiba (serikali tatu) vikakataliwa na wabunge wengi hasa ikichukuliwa kuwa sera ya CCM ni serikali mbili.
Tutaona na kusikia mengi!.