Warioba:Tanganyika ina shutumiwa kwa kuvaa koti la Muungano na kufanya Tanzania ndiyo Tanganyika

Warioba:Tanganyika ina shutumiwa kwa kuvaa koti la Muungano na kufanya Tanzania ndiyo Tanganyika

Muungano??????? upo kweli ??? !!!!!!!!!!! serikali 3 ? ! tehe teeehheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
haya mambo yote ya muungano huu ni ujanja ujanja tuu,na baada ya kuimeza znz wakachululiwa watu hao 85 wanaoitwa wabunge na mawazir kuiwakilisha znz, hapa hapahitajiki kugaiwa mafungumafungu mambo ya kupewa znz isipokua umefika wakati wakufuta neno Tanzania na kurejesha Tanganyika bila ya kutafuna maneno.

Turudishe znz ya 63 na Tanganyika ya 61 muda umefika tusizungushane na kutumia pesa nyingi.

Kwa upande wa Znz huu sio mwisho wa kinyamazisha mpk ifike pahali kila taasisi iwe inafanya inachokitaka kwa Uhuru na sio kuigaia kama imekuja kuomba na kuiangukia Tanganyika.
 
Tutakuwa viziri mjini hapa kwa ving'ora vya misafara ya maraisi wa 3.....sasa wakiwa watembezi kama huyu bado watakuwa wanagongana angani
teh teh, yatakuwa ni mashindano ya kula kodi za watanzania huko ulaya...
 
Mzee Warioba amesema zipo shutuma kwamba Tanganyika ilijivua na kuvaa koti jipya la muungano ambalo hapana shaka Tanzania bara kuonekana kufaidi matunda ya muungano kuliko Wazanzibari hata kupelekea Tanzania kuonekana ndiyo ile Tanganyika iliyo kufa.

Hali hiyo ndiyo inayofanya ongezeko la kero za muungano.Kwa maneno yake Wazanzibari wanaona ni ujanja tu ulitumika kuinyang'anya mamlaka yake Zanzibar nakisha kuiua kabisa na labda ndiyo chanzo cha hali duni za maisha ya Wazanzibari.

Wangetamani wajiunge na umoja wa nchi kama OIC unaojumuisha nchi za kiislamu hatua ambayo ingebadili kipato chao lakini haiwezekani kwakuwa koti linavaliwa Bara kwa mgongo wa muungano.

amesema tume yake ime angalia options nyingi ili kuondosha Muonekano huo lakini imeshindwa kupata balikurejesha pendekezo la kwenye rasimu ya kwanza la serikali tatu.

Ame chukua muda mrefu hadi kuchosha kuelezea hilo naona baaba ya kuhisi ccm wasinge taka hata kusikia serikali tatu.Kwakweli ameonyesha kuwa Wazanzibari walikuw wanataka kitu kingine siyo serikali mbili tena kitu ambacho ni mwiba kwa ccm.

Na hadhani kama wangetaka serikali moja kwani hiyo ni kuimeza kabisa Zanzibar.amesema zaidi ya 60%ya Watanzania Bara walitaka tatu hali kadhalika huko Zanzibar.

Nakiasi kikubwa Zanzibar walitaka muungano wa mkataba.

Tupo katika takuli kubwa wa kuu hali ndiyo hiyo
kinachotakiwa hapo ni kufuata maoni ya wengi hata kama wana ccm wote wakipinga serikali tatu bado watakuwa ni wachache kulinganisha na wanaotaka serikali tatu,vinginevyo ni kutoitakia kheri nchi yetu
 
haya mambo yote ya muungano huu ni ujanja ujanja tuu,na baada ya kuimeza znz wakachululiwa watu hao 85 wanaoitwa wabunge na mawazir kuiwakilisha znz, hapa hapahitajiki kugaiwa mafungumafungu mambo ya kupewa znz isipokua umefika wakati wakufuta neno Tanzania na kurejesha Tanganyika bila ya kutafuna maneno.

Turudishe znz ya 63 na Tanganyika ya 61 muda umefika tusizungushane na kutumia pesa nyingi.

Kwa upande wa Znz huu sio mwisho wa kinyamazisha mpk ifike pahali kila taasisi iwe inafanya inachokitaka kwa Uhuru na sio kuigaia kama imekuja kuomba na kuiangukia Tanganyika.
jina Tanganyika halitakiwi kwa sababu itaonekana wenye hasili ya nchi hii ni watu wa Kigoma
 
Huu muungano utavunjika mara serikali ya Tanganyika itaporudi, kwa sababu rahisi kabisa. Kutakapokua na serikali ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika uchangiaji wa kuchangia serikali ya muungano watataka uwe nusu kwa nusu, ama kwa creteria fulani ambayo kwa uhakika kuna upande hauta kidhi hilo takwa.
 
Umeishawahi kaa na wazanzibari mkaongea kuhusu muungano ukasikiliza maoni yao?

chris lukos, kumbe sometimes unakuwa objective! waZenji kiufupi hawautaki muungano, na sisi tunajibembeleza tuu, sijui sababu ni nini haswa!

ukikaa nao falagha utajua jinsi wasivyoupenda muungano, ila unafiki unawasaidia na ndo kisa muungano upo! serikali tatu ni option ya kwanza, kama iki fail we do the needful
 
Hapo ndio target ya wazanzbr,zanzibr hapo ndipo itakapo shuhudia jua la uhuru.
 
warioba wewe na wenzako wote ni wazalendo na ndio maana hata bungeni hamtakuwepo mtakuwa wasikilizaji kama sisi huku. je wale wa kura za ndiyo waliopeleka hoja bungeni kuwa kazi yanu iishie hapo/ kukabithi kwa Rais rasimu kisha urudi bunda ukalime mawazo hayo yatapitishwa na watu hao?
 
Hizi hassle zote za nini?. Kwani nani amesema wananchi wanataka muungano?.

kwa mazingira yalivyo kwa sasa nchini, serikali tatu ni njia ya kuelekea katika uvunjifu wa Muungano wakati huo huo serikali mbili kwa sasa wala hazina hata mandate ya Watanzania wengi.

Kwa nini kama nchi mbili tunapita njia ndefu yenye gharama kubwa za kisiasa na kiuchumi wakati kuna njia fupi isiyo na gharama kubwa kama hizo!.

Kura ya maoni kuhusu kuwepo muungano au hapana ni mwarobaini kisiasa na bila hivyo, ni kuwalazimisha wananchi wakubali au kukataa serikali tatu huku wameziba options zingine za serikali moja, mbili, etc.

Itakuwaje wananchi au bunge likikataa hii Rasimu ya Katiba hasa kipengele cha aina ya serikali?.

Ndiyo maana tume ya Jaji Warioba inataka iendelee kuwepo hata wakati wa mchakato wa bunge la Katiba na kura ya maoni kwa sababu ulaji bado uko mezani kwa maana kuwa, wanafahamu kuna uwezekano mkubwa baadhi ya vipengele vya Rasimu ya Katiba (serikali tatu) vikakataliwa na wabunge wengi hasa ikichukuliwa kuwa sera ya CCM ni serikali mbili.

Tutaona na kusikia mengi!.
 
Duhm kazi kwelikweli! sasa umeongea nini?

Unapounga mkono serikali tatu maana yake unaunga mkono na serikali ya tatu ya Muungano wa shirikisho lenye Tanganyika na Zanzibar.

Halafu unasema muungano huoni faida yake na uvunjwe! Sasa kauli yako ya kwanza inamaanisha nini?

Try to shake your head before use!
Mkuu kwa kifupi mimi binafsi huo muungano siutaki hata kidogo,

Ni mzigo wa misumari tu na hauna faida kwetu
 
jina Tanganyika halitakiwi kwa sababu itaonekana wenye hasili ya nchi hii ni watu wa Kigoma

Neno nyika linamanisha fukwe/pwani/coast halafu Tanga=matanga vile vyombo vya asili vya majini mfano wa mashua, kwa hiyo enzi za biashara kati ya afrika mashariki na Asia katika bahari ya hindi matanga mengi yalitia nanga katika nyika ya mkoa wa Tanga. Kwa hiyo asili ya Jina Tanganyika ni huko mkoani Tanga na si Kigoma!!
 
Hizo gharama zake, ikipitishwa mtaanza tena kulialia,bongo bongolala
 
Back
Top Bottom