Warioba:Tanganyika ina shutumiwa kwa kuvaa koti la Muungano na kufanya Tanzania ndiyo Tanganyika

Warioba:Tanganyika ina shutumiwa kwa kuvaa koti la Muungano na kufanya Tanzania ndiyo Tanganyika

Mapunduzi ya kiuchumi yakipatikana kwa kila mmoja wetu hakuna atakaye sema habari za kero. Serikali itazame madeni kwanza kwa watumishi wake ndipo tuone uwezekano wa kutanuwa mamlaka. Mawaziri wasiwe wabunge pesa za Mawaziri za wabunge zitatoka wapi. Au ndo kukamuliwa kodi hadi tone la mwisho. Haya mambo hayatakiwi mas' hara wala kujaribu ni kujadili sana kichwani kwa kituo
 
Mimi nilishasema siku nyingi. Ipigwe kura ya maoni, ili muungano uendelee iwe lazima upate simple majority both sides.

Kura ya maoni ni njia pekee ambayo Watanzania wa pande zote watakuwa na haki ya ku-determine their right to self-determination. Haya mengine ya sijui serikali tatu ni kupotezeana muda na matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima.

Yaani nchi mmoja inakuwa na Marais watatu? Kwa hiyo siku wakitembelewa na mkuu wa nchi nyingine, watakuwa wanajipanga mbele yake na kujitambulisha mimi ni wa Tanzania, mimi wa Tanganyika na mimi ni wa Zanzibar? Hiki ni kioja.

Ukiachilia mbali Urais bado kutakuwa na Bunge la Muungano ambalo litakuwa na wabunge sijui 70 or so achilia mbali Waziri Mwandamizi, Mawaziri wa wizara za muungano, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu wa Wizara hizo hizo za Muungano. Nadhani na serikali shiriki zitakuwa na watu kama hao pia.

Badala ya ku-address tatizo tunalizungazunga na kulipaka rangi za kuvutia. Wapo wanaodai kuwa pendekezo la serikali tatu limewekwa ili kurahisisha kuvunjika kwa muungano.

But justice delayed is justice denied. Tunajua muungano utavunjika tuu, but the earlier the better.
 
Hapa ndipo serikali(ya Tanganyika na ya zanzibar) zitawajibika kupitia ushindani wa kimaendeleo.
 
Mawaziri wasiwe wabunge pesa za Mawaziri za wabunge zitatoka wapi.

Kwani kwa sasa unadhani kuwa hao Mawaziri ambao ni wabunge hawatwangi kotekote?

Ukitaka kujua hayo kwa undani ukifikia nusu ya marupurupu na posho anazopata waziri kutokana na Ubunge na uwaziri (anatwanga kotekote) utazimia wewe manake naona huna kifua cha kufunuliwa hayo!
 


What kind of an opinion is this? Plastic brains!

chris-jestina-na-wadau-wengine-wakikusanya-misaada-mbalimbali.jpg


Ahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa people this is too personal kwikwi kwi
 
Neno nyika linamanisha fukwe/pwani/coast halafu Tanga=matanga vile vyombo vya asili vya majini mfano wa mashua, kwa hiyo enzi za biashara kati ya afrika mashariki na Asia katika bahari ya hindi matanga mengi yalitia nanga katika nyika ya mkoa wa Tanga. Kwa hiyo asili ya Jina Tanganyika ni huko mkoani Tanga na si Kigoma!!
nipe asili ya ziwa Tanganyika
 
Naunga mkono serikali tatu Na huo muungano sioni faida zake uvunjwe tu
Unachotaka kueleza hapa nini. Haiwezekani uunge mkono serikali 3 at the same time usitake muungano. Tunaounga mkono serikali 3 tunahitaji muungano, ila tunataka uwe modified kuondoa au kupunguza kero.

Wewe kama huungi mkono muungano basi hii katiba ya Jaji warioba haikuhusu maana ni katiba ya muungano.

Wewe unachotakiwa kudai ni kuvunja muungano na kutaka kila nchi iandae katiba yake kivyake.

Nina mashaka kama unajua nini kinaendelea.
Huu ni mfano wa mambo yanayoonyesha hali halisi ya upeo wa huyu jamaa yetu
 
Hivyo hata kidogo sielewi inamaana sasa TANU NA AFRO SHIRAZ VINARUDI? VILIUNGANA KUELEKEA TAIFA MOJA TU. WABABE WA DUNIA KWA HILA ZAO WAKATUTAKA TUWE NA VYAMA VINGI ILI VIPATE KUTUGOMBANISHA KWAO VICHACHE ILI HALI MAJIMBO WAMEUNGANA NA UCHUMI MZURI WA VIWANDA. JE HAPA NDO KUBANA MATUMIZI YA SERIKALI AMA NI FAIDA KUBWA ITOKANAYO NA KODI? SIJAMWELEWA VIZURI MHESHIMIWA. TUNACHO HITAJI NI WATAALAMU WA SAYANSI NA UFUNDI NDIKO DUNIA INAKO KWENDA. MIAKA 50 BADO TUNAPANGA NAMNA YA KUJITAWALA. TUFUFUE KILIMO TUSHIBE NA VIWANDA TUVAER
 
Tukishiba na kuvaa vyema hutasikia mtu akizungumza 1.muungano 2. Mawaziri waajiriwe 3 wabunge kivyaovyao 4. Madaraka makubwa hoo madogo. Cha msingi kama muungano upo rekebisha kero zilizopo basi. Ikiwa jamhuri ya muungano tz kwenye ndimi tumeendeleza utanganyika na uzanzibar lazima haya yaje. Sasa natakiwa ni jiite kitaifa mtanzania naona kuchanganyikiwa hapo hapo mz.bar na kuna mt.nyika na mtz hatuwezi kupata katiba mpya zaidi ya kuboresha tu iliyopo. Jambo muhimu ni kuimarisha serikali yetu huko z.bar asili ilivyo ni hao hao wahiyao wangoni wamakonde wasukuma wazigua wazaramo waruguru wadigo nk nk pamoja na mwingiliano wa washiraz na waliokwepo hapo kisiwani. Tujitambue
 
Lukosi watu walikuwa wanakubeza kumbe pia ni mzalendo, hapo pia nakuunga mkono. Japo kuwa umerudi ccm labda kwa faida ya biashara zako, lakini bado unaonyesha kuwa una damu ya mageuzi(revolution) ila huja pata chama kinacho kulidhisha. Hata hivyo kwa sasa bado nitasema kuwa unadamu ya cdm, ccm unaiunga mkono ili biashara zako ziende vizuri. Najua baadae utarudi tu.

unampongeza wakati anataka serekali 3 bila muungano,zitatokea wapi?msaidie kufafanua labda
 
Kumbuka jina tanga nyika limetokea tanga sio kigoma bro. Walio mjini tanga waendapo shambani walikuwa wakiita nyika maeneo ya mashambani. Ni jna lililobuniwa haraka haraka nchi ilpo pata madaraka. Kutokupata historia na jiografia kumewaacha vijana wengi kutambua nchi yao. Mdharau kwao mtumwa
 
Ahsate kwa kuelimisha kwani Wtz huwa ni watu wa kudandia mambo bila kupima madhara yake wala faida itokanayo
 
Unachotaka kueleza hapa nini. Haiwezekani uunge mkono serikali 3 at the same time usitake muungano. Tunaounga mkono serikali 3 tunahitaji muungano, ila tunataka uwe modified kuondoa au kupunguza kero.

Wewe kama huungi mkono muungano basi hii katiba ya Jaji warioba haikuhusu maana ni katiba ya muungano.

Wewe unachotakiwa kudai ni kuvunja muungano na kutaka kila nchi iandae katiba yake kivyake.

Nina mashaka kama unajua nini kinaendelea.
Haya ni mawazo ya mtu mwenye busara sana kutotaka muungano ni kuturudisha nyuma ya mchakato mzima wa katiba mpya ya Jamuhuri ambao sasa unakaribia mwisho wake
 
Ni jna lililobuniwa haraka haraka nchi ilpo pata madaraka. Kutokupata historia na jiografia kumewaacha vijana wengi kutambua nchi yao. Mdharau kwao mtumwa
TANU iliundwa kabla ya uhuru, niambie T katika neno TANU ina maana gani? kabla ya hapo kulikuwa na TAA, je T katika TAA inasimamia nini?

Upotoshaji juu ya upotoshaji.
 
Back
Top Bottom