Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,473
- 13,629
Nakumbuka miaka ile ya utotoni namna chuo cha uongozi cha kivukoni kilivyokuwa maarufu. Ukipanda pantoni pale feri ndani ya dakika chache umeshafika Kivukoni. Walikuwepo makada halisi wa Chama waliokuwa wakiandaliwa na Hayati Julius Nyerere akishirikiana na wakongwe wengine.
Yale yalikuwa ni maoni kwa Tanzania ya kesho ambayo ndio hii ya leo hii. Walijua kuwa wao hawatakuwa na muda mwingi juu ya ardhi hii iitwayo Tanzania wakaona ni bora watafute viongozi vijana ili wawe wanawafundisha kidogo kidogo siasa za Taifa leo. Wakawa wanatembea nao mikutanoni ili wazoee aina ya kazi za kisiasa walizopanga wazifanye baada ya wao kuwa wameshapitwa na wakati.
Wiliiam Lukuvi, George Mkuchika, Abdulrahman Kinana, Jakaya KIkwete, Edward Lowassa na Jaka Mwambi kwa kuwataja wachache walikuwa wakipikwa ili waje wachukue nafasi ya kina Mwalimu Nyerere, Kawawa, Ali Sykes na wakongwe wengine waandamizi.
Cha ajabu kilichokuja kutokea ni kuwa hao warithi waliopikwa pale Kivukoni wakashindwa kuwa na mioyo inayoangalia maslahi ya kiuongozi na ya kitaifa wakaanza kuangalia maslahi binafsi ya kwao. Wakaanza kutengeneza wigo wa mtandao ambao ni kama utando fulani wa kisiasa. Wigo wa kujizungushia tabaka fulani la wanasiasa wenye vionjo kama vya kwao.
Hekima iliyokusudiwa na Mwalimu Nyerere ikaishia njiani, ikakosa muendelezo wa watu wenye unyenyekevu wa kivitendo na kifikra. Aliyeshindwa na kupoteza akawa na Mama Tanzania na aliyeshinda akawa ni ubinafsi, uwepo wa mitandao ya kujuana na kikabila, kupenda kufukuzia mali na utajiri unaotokana na wizi wa mali ya umma. Leo hii kila mtu analalamika, kila mtu analia.
Siasa za kusifiana na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa zimeshamiri. Ni vigumu kumlaumu Mwalimu Nyerere kwa sasa, ni hayati asiyeweza kujitetea kwa namna yoyote ile. Lakini alipokuwa hai aliongelea kwa kina maono yake na akautumia ualimu wake kutufundisha ni wapi kama Taifa tufikirie kufika. Lakini warithi aliotembea nao akitumia kodi ya serikali kuwafundisha maana ya uadilifu na utumishi ni kama wamefeli somo walilopewa kwa gharama kubwa! Inasikitisha sana kwa kweli.
Chuo cha Kivukoni hata kama kipo au kinategemea kufufuliwa kitakuwa na mengi sana ya kuyarudisha ili warithi wa wanasiasa waliorithishwa na kizazi cha Nyerere waweze kusimama mbele ya watu na wakaheshimiwa. Udalali wa mali za Taifa ukiwa ndio fasheni ya masuala ya siasa hapo ni mwendo wa kutengeneza roho za uasi kwa Mama Tanzania.
Hata wale watumishi walioitanguliza nchi yao kwa upendo wakitaka kufanya makubwa yawasaidie watanzania wa kesho ni rahisi sana kuzungukwa na watu wenye nia za wizi na za kupenda starehe zinazopita kama upepo.
Wale warithi wa falsafa za Mwalimu Nyerere wameshindwa kutengeneza warithi wao wenye kufanana na unyenyekevu wa Mwalimu, hii ni kwa hasara ya Taifa ambalo kitakwimu limekuwa likikua. Mwalimu Nyerere hakuwezi kuwasoma vijana aliotembea nao miaka ile na kuiona kesho yao ikiwa ni hii iliyozungukwa na tamaa na mambo mengi yasiyo na ustaarabu.
Maono yake yalikuwa na mipaka ya kibinadamu, japokuwa nia yake ndio itakayomtetea kila litakapokuwa likijadiliwa Taifa hili na mustakabali wake. Wapendwa Idd Mubarak.