Warumi (RIP) nimekumiss mwenzio

Tutapumzika tuu kama tumemaliza kazi tuliyotumwa. Tuombeane mwisho mwema orturoo
Sawa mama D ,nakuombea kifo chema na wana jf wote wakati ukifika Tupumzike kwa amani,nitakukumbusha tukikutana mbinguni
 
Tutapumzika tuu kama tumemaliza kazi tuliyotumwa. Tuombeane mwisho mwema orturoo
Wakati mwingine hata hatumalizi missions tulizo tumwa, let alone ours , the world is not fair kwa kweli
 
Tutapumzika tuu kama tumemaliza kazi tuliyotumwa. Tuombeane mwisho mwema orturoo
Tumalize kazi tusimalize, wakati ukifika tutakwenda tu, kisha huko ndio tutajajiwa kwa kazi tuliyotumwa kama tumeimaliza ndani ya muda tuliopewa au lah..
Mathalani.. Ofisi imekupa kazi fulani kwa muda wa miaka miwili, basi miaka miwili ikikata ww unarudi makao makuu, kisha itategemea na ufanisi wako katika kazi uliyotumwa, aidha uule ama ile kwako

Ingekuwa tunaondoka kwa kumaliza kazi, basi soote ni mwendo wa kujichelewesha tu maana kifo kinatisha mpendwa.. [emoji23] Nacheka kama mazuri vile
 
NA SISI TUPUMZIKE KWA AMANI KWA WAKATI UJAO.....RIP FOR ALL OF US
Tujiandae kwa kufanya mema. Lazima tupendane, tuheshimiane, tuthamiane, tuwasaidie mayatima, tuwajali wajane, chuki, roho ya korosho tupa kule, unacho na una uwezo wa kusaidia saidia, usisaidie ukajigamba..
 
Sawa mama D ,nakuombea kifo chema na wana jf wote wakati ukifika Tupumzike kwa amani,nitakukumbusha tukikutana mbinguni

Mungu atujalie tufike huko
 
Wakati mwingine hata hatumalizi missions tulizo tumwa, let alone ours , the world is not fair kwa kweli

Na wengi hatujui hata tulichotumwa, na wale tunaojua tulichotumwa ya dunia yanatuzongazonga kweli.... kila siku tunasema tutafanya hadi tunatwaliwa bila kukamilisha.

Mungu atusaidie kumpa yeye kwanza nafasi ili mengine yote yafanyike katika yeye
 

Kila mwanadamu aliyepata kibali cha kuzaliwa duiniani na kuishi ametumwa kwa mission maalum ya Mungu.

Kila kazi tunayofanya tunatakiwa kuifanya kwa sifa na utukufu wa Mungu. Tukitumia akili na hekima tuliyojaliwa na Mungu katika kukamilisha yale aliyotuagiza kuyakamilisha
 

Hahah!!

Unataka usife halafu kitokee nini?
 
Ohooooo, Mama D mbona kama unatuaga vile? [emoji2297][emoji2297]
 
Kweli hata uchambuzi wa Paula ungetolewa r.i.p him.

Lakini kumbuka hizo sifa hazimufikii kwa nini msiwe mnatoa sifa mtu akiwa hai?

mama D hebu kama kuna mtu mwingine anakufurahisha humu mpe sifa akiwa hai ili azipokee
 
Kila mtu ataondoka Getang'wan hata usipoaga utaondoka tuu

Usiseme mimi nakuaga sababu wewe mwenyewe unaweza kukuta huna hata dakika5 kwenye uhai wako uliobakia hapo ulipo


Hapo sina ubishi kabisa Mama D. Ila ni kuwa watu tunajisahau sana na wala hatufanyi maandalizi ya kufika mwisho mwema kwa kuwa hatujui siku wala saa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…