Nilikuwa msabato na bado naipenda sana Sabato mpaka leo hii, ila kwa sasa nimeshakuwa Mlokole! Tatizo kubwa sana nililonalo sasa hivi ni kwamba najua yote yaliyoko kwenye usabato na baadhi tu ya yaliyoko kwenye ulokole, na hilo ndiyo tatizo pekee linalonifanya niendelee kuwa mlokole! Nadhani siku nikishayajua yote yaliyoko kwenye ulokole, naweza nikarudi tena Sabato. Tatizo lililopo ni kuwa itikadi ya walokole imejikita kwa Roho Mtakatifu aliyeshuka siku ya Pentekoste, wiki kadhaa baada ya Yesu kuwa amepaa mbinguni. Sasa huyu Roho Mtakatifu ni FACT kuwa hana mwanzo na wala mwisho, ila tofauti na mimi, mwanzo ninao japo nami mwisho sina.. Sasa najiuliza ni lini yaliyoko kwenye ulokole nitakuja kuyajua yote, ili angalua nipate tena nafasi ya kuhamia kwingine? Msaada tafadhali katika hili, kama upo!