Wasabato msiwe kama Wayahudi wanaomsubiri Kristo wakati alishakuja miaka zaidi ya 2000 iliyopita!

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Tunaishi kipindi baada ya unabii. Mambo yaliyotabiriwa kumhusu Yesu Kristo yalishatokea. Msione Kitabu cha Ufunuo kimewekwa cha mwisho katika mpangilio wa vitabu vya Biblia mnafikiri hayo ni mambo ya baadaye. Ni kama unabii wa Isaya au manabii wengine ulishatokea.

Maono ya Yohana juu ya dunia mpya na mbingu mpya yalishatokea tangu ukombozi wa Kristo ulipotufikia. Tunaishi siku za ukamilifu wa nyakati na Yesu Kristo ndiye utimilifu wa unabii wote na nyakati zote.
 
Ufunuo 1:7
Tazama, Yesu anakuja pamoja na mawingu! Kila mtu atamwona, hata wale waliomchoma.[b] Watu wote wa dunia watamwombolezea.[c] Ndiyo, hili litatokea! Amina.
Hili nalo limeshatokea?
 
Ufunuo 1:7 Hili nalo limeshatokea?
Yesu alishakuja akazaliwa duniani alitokea Mbinguni ( mawinguni).

Watu wote duniani watamwombolezea. Dunia kwa wakati ule ilikuwa ni maeneo ya Middle East, uyahudi na maeneo yanayozunguka na sio kama ilivyo leo. Hata hivyo watu duniani wameshasikia kumhusu Yesu na wamemwombolezea.
 
Imeandikwa Kila mtu atamwona akiwa anakuja kutoka mawinguni,hata wale waliomchoma/waliomsulubu

Hilo limetokea?? Acha kukaza fuvu sasa nawewe
 
Inasemwa wasabato NDIO MAFARISAYO WA ZAMANI...πŸ˜ŠπŸ˜ŠπŸ€“πŸ€“
 
πŸ‘€πŸ‘€
 
Mkuu haya maneno umejifunza wapi, nipe source nami nikale nondo
 
Kwa hiyo unabii wa siku za mwisho umeshatimia na hukumu imeshasomwa na waovu wanateketea kwenye ziwa la moto, mbona tunaingizana chaka kimakusudi kabisa? au hii ndo imani ya wale wanaojiita jumba la ufalme la mashahidi wa yehova.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…