Hujui unachoongea wewe! Wasanii kibao kutoka Arusha wameenda pale Wasafi! Hata Weusi, wameshaenda pale Wasafi including Nick II. Wale wanaoendesha kipindi cha Block 89, kuna wengine wanatokea kaskazini! Yaani kutowepo Joh Makini tu ndo uone kuna ukabila?! Kwani Joh na Nick II wanatoka makabila tofauti?! Kwamba Huwezi kuona Mond au Wasafi wana-launch shows Arusha, unazungumzia shows zipi hasa?! Ukiona Mond, Harmonize, Mboso au yeyote ameenda mkoa X ni kwamba huko kuna promota kafika bei ndo maana wameenda! Sasa ulitaka waende Arusha hata kama hakuna Promota aliyehitaji hao wasanii waende huko na akafika bei?!
Swali ni je, kwanini mapromota wa Arusha hawawaleti Wasafi au Diamond?! In short Arusha mna usela mavi, manake usela wa fujo ni usela wa kishamba! Clouds walishawahi kupeleka Fiesta, ikaibuka bonge la vurugu hadi Clouds wakaachana na Arusha! Sasa unadhani kuna promota anaweza kuita msanii anayetaka pesa nyingi wakati hana uhakika ikiwa shoo itaisha salama?!
Acheni usela wa kishamba!
Lakini kama unazungumzia shows za Wasafi; ni shows zipi hasa?! Kama ni Wasafi Festival Festival, imefanyika mara moja tu tena kwa majaribio! Na mara moja yenyewe, kuna mikoa kibao haikufanyika including Dar es salaam! Sasa kwanini uone kutofanyika Arusha ni ukabila?! We unafikiri Wasafi au Diamond wanafanya charity work hadi udhani hawawezi kwenda sehemu eti kwa sababu za ukabila?
Kuna kila dalili, wewe ndo mkabila!