Embu waeleze mimi nachoka maana ukishaingia kwenye 'clash of the titan' lazima uchague upande ambao wewe unaona utashinda ni kama Brazil icheze mpira wa miguu na Korea Kaskazini alafu u side na Korea Kaskazini. If you fail to plan is you plan to fail.
Clous wameshatengeneza platform kubwa sana kuanzia wadau, maproducer, ma Dj sio ajabu ndo wamewatengeneza wao alafu aje kamtu kamvimbie.
Diamnond atambue kwamba kama anataka kufika mbali kwenye dunia ya leo lazima apate partner. Sasa analeta majidai ya kwao huko anavimba na kila mtu. Sasa wakikubania utalia maana Clous wakikunja misuli inamaana hutakuwa na fan base kwenye radio nyingine, majukwaa mfano Fiesta, Alex Msama promotion, Nyamachoma festival, Kili marathon etc. Diamond akibanwa kweli kweli nakuambia hatoboi kabisa.
Mimi nashangaa nyimbo za Diamond hit song kama Mbagala, Mawazo, Number one, etc. Number one ndo ilimletea kiburi ndo ikapeleka kama hit song Eneka, Iyena etc kuchuja haraka japo ni nyimbo nzuri
Daimond aache kiburi na ashirikiane na wengine sio maugomvi ya kijinga