Wasafi Media Mtegoni. Diamond, Kusaga wavurugana

Hili suala binafsi nilikuwa nalifahamu tangu 2011 wakati nafanya kazi kwenye media house. Wengi wenu humu JF hamjui mambo mengi sana ya mjini. Mmesoma ila mambo ya town mko nyuma sana.
Mimi nalifahamu tokea 2017 na sio kwa habari za kusikia, ni suala ambalo tulilifuatilia wenyewe.

Watu wanaleta ujuaji wa mambo ya darasani wakati hapa tunaongelea uhalisia.
 
View attachment 2929146Wakurugenzi wa Wasafi Media, Joseph Kusaga na Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ wanaripotiwa kukosa maelewano kati yao juu ya uendeshaji wa media hiyo inayomilikiwa na wawili hao.​

Chanzo ni TRA
Diamond ambaye amekuwa akitafutwa na maafisa kodi kwa muda mrefu, huku yeye akitumia 'janja janja' kuwakwepa, maafisa kodi hao wamehamishia majeshi kwa Joseph Kusaga.

Joseph Kusaga ambaye majukumu ya uendeshaji amemwachia Diamond, amekuwa akimpigia simu mara nyingi Diamond bila mafanikio.
Hivyo Diamond anawakwepa maafisa kodi, na huku simu za Kusaga pia hapokei.

Kusaga achoshwa na mabifu ya Diamond!
Inaarifiwa kuwa Kusaga amekuwa akilalamika mara nyingi juu ya mabifu ya Diamond na watu wengi ambayo yanaikwamisha Wasafi Media kukua.

Wakati anaanzisha media hiyo 2016, alikuwa na malengo makubwa ya kuikuza kuwa kubwa pengine kuizidi Clouds Media ambayo ni mali ya familia yao. Hivyo kupitia umaarufu wa Diamond alitegemea kuvuna wasikilizaji kutoka kila pembe ya nchi jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limefanikiwa ila kikwazo kikiwa ugomvi wa Diamond na watu wengi ambao wengi hutumia mabifu hayo kama fursa ya kuikwamisha Wasafi Media.

Kusaga Amgeukia Ali Kiba…
Habari za uhakika ni kwamba mastermind huyo wa biashara za vyombo vya habari na nyinginezo lukuki, ameelekeza nguvu zake kwa hasimu wa Diamond, Ali Kiba.

Wawili hao (Kusaga na Ali) wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha masuala muhimu likiwemo jina rasmi la kutumika kuitambulisha Media hiyo.

Kupitia chanzo changu makini nimefanikiwa kunasa jina linalopewa kipaumbele, Kings Media (Kings TV & Kings FM).

Pia watangazaji ambao tayari wameshawekwa kwenye list ni Abdallah Ambua ‘Dullah Planet’ aliyeng’oka EATV na EA Radio hivi karibuni, pamoja na Khalid Mohamed ‘TID’.

Kusaga na utajiri wa frequencies!
Kwa wafuatiliaji wa masuala ya media hasa radio, watakuwa wanafahamu ya kwamba hivi sasa hakuna frequency mpya hapa jijini Dar Es Salaam.

Yaani kwamba ukitaka kuanzisha redio huwezi kupata mawimbi ya kukuwezesha kusikilizwa Dar, labda ununue (frequency) ambayo inamilikiwa na wengine kisha uibadilishe kuwa redio yako.

Wajanja wa mjini wamezihodhi, akiwemo Joseph Kusaga ambaye anaarifiwa kuwa nazo kwa idadi ambayo haifahamiki.

Kupitia chanzo changu nyeti,

Nifah.
Unanikumbusha warumi ...nimelia Mimi.
 
Ficha upumbavu wako. FM frequency kila mji unapangiwa masafa (frequency moja tu) na FM ina Total 100 Stations kwa kila mkoa:
The FM radio band is from 88 to 108 MHz between VHF television Channels 6 and 7. The FM stations are assigned center frequencies at 200 kHz separation starting at 88.1 MHz, for a maximum of 100 stations.
Dar es salaam Wajanja wameziomba na awajaanzisha Redio ila wanazilipia kila Mwaka..... hii pia ipo katika Telecom... wapo Matajiri walikuwa wanamiliki Frquency za kuanzisha makampuni ya simu kwa miaka mingi hapa Tanzania mpaka pale TCRA walipobadilisha mfumo wa umiriki wa hizo Frquencies . Ila kwa Radio na TV bado wapo watu wanazo na awajafungua stations. Ukizitaka unalipa hela ndefu ndo upewe. Kama unaweza omba TCRA ukapata FM frequency Dar ni PM tuyajenge nnahitaji moja
Umeongea kitaalam kabisa
 
Hiyo Paragraph ya mwisho uwongo,Frequency ni mali ya TCRA yy ndiye anaye panga na kuengineer na ukitaka nenda pale TCRA Frequency bado wanazo na ukimzingua anakunyang'anya Frequency zake.
Labda kabla ya kuuzwa ndiyo huwa mali yao, lakini zikishauzwa huwa ni mali ya aliyezinunua.

Ni kama shati ukishalinunua ni lako siyo ya la aliyekuwa akiliuza. Na watu kadhaa wamenunua, frequencies ni za kwao.

Ova
 
Bakhresa sio mogul wa media kwamba atafanya kufa au kupona apate jambo lake kwenye frequency.
Wala hajaianzisha UFM ili impe faida ya kifedha direct, bali atangaze bidhaa/huduma zake na hasa kwa vile Azam ina mkataba ligi kuu. Ndio maana UFM imejikita zaidi kwenye michezo.

UFM kwa Bakhresa ni kama mkuu wa mkoa alime ekari moja ya mahindi, jua likiwaka usidhani atalia na kusaga meno kwamba sasa atakula wapi. Ukitaja wakulima wa mahindi, huyo mkuu wa mkoa mtoe.
Ni kweli kabisa mkuu unachoandika, Bakhressa lengo lake kubwa ktk kuanzisha UFM ni kutangaza biashara zake. Na ndiyo maana huwezi kusikia UFM ikitangaza matangazo ya kamari kama wanavyofanya hao Wasafi media au Clouds media.
 
View attachment 2929146Wakurugenzi wa Wasafi Media, Joseph Kusaga na Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ wanaripotiwa kukosa maelewano kati yao juu ya uendeshaji wa media hiyo inayomilikiwa na wawili hao.​

Chanzo ni TRA
Diamond ambaye amekuwa akitafutwa na maafisa kodi kwa muda mrefu, huku yeye akitumia 'janja janja' kuwakwepa, maafisa kodi hao wamehamishia majeshi kwa Joseph Kusaga.

Joseph Kusaga ambaye majukumu ya uendeshaji amemwachia Diamond, amekuwa akimpigia simu mara nyingi Diamond bila mafanikio.
Hivyo Diamond anawakwepa maafisa kodi, na huku simu za Kusaga pia hapokei.

Kusaga achoshwa na mabifu ya Diamond!
Inaarifiwa kuwa Kusaga amekuwa akilalamika mara nyingi juu ya mabifu ya Diamond na watu wengi ambayo yanaikwamisha Wasafi Media kukua.

Wakati anaanzisha media hiyo 2016, alikuwa na malengo makubwa ya kuikuza kuwa kubwa pengine kuizidi Clouds Media ambayo ni mali ya familia yao. Hivyo kupitia umaarufu wa Diamond alitegemea kuvuna wasikilizaji kutoka kila pembe ya nchi jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limefanikiwa ila kikwazo kikiwa ugomvi wa Diamond na watu wengi ambao wengi hutumia mabifu hayo kama fursa ya kuikwamisha Wasafi Media.

Kusaga Amgeukia Ali Kiba…
Habari za uhakika ni kwamba mastermind huyo wa biashara za vyombo vya habari na nyinginezo lukuki, ameelekeza nguvu zake kwa hasimu wa Diamond, Ali Kiba.

Wawili hao (Kusaga na Ali) wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha masuala muhimu likiwemo jina rasmi la kutumika kuitambulisha Media hiyo.

Kupitia chanzo changu makini nimefanikiwa kunasa jina linalopewa kipaumbele, Kings Media (Kings TV & Kings FM).

Pia watangazaji ambao tayari wameshawekwa kwenye list ni Abdallah Ambua ‘Dullah Planet’ aliyeng’oka EATV na EA Radio hivi karibuni, pamoja na Khalid Mohamed ‘TID’.

Kusaga na utajiri wa frequencies!
Kwa wafuatiliaji wa masuala ya media hasa radio, watakuwa wanafahamu ya kwamba hivi sasa hakuna frequency mpya hapa jijini Dar Es Salaam.

Yaani kwamba ukitaka kuanzisha redio huwezi kupata mawimbi ya kukuwezesha kusikilizwa Dar, labda ununue (frequency) ambayo inamilikiwa na wengine kisha uibadilishe kuwa redio yako.

Wajanja wa mjini wamezihodhi, akiwemo Joseph Kusaga ambaye anaarifiwa kuwa nazo kwa idadi ambayo haifahamiki.

Kupitia chanzo changu nyeti,

Nifah.
I love it! Huu ni udaku pro b..., details zilizopo humu zinakufanya uwe kwenye dunia yako kwenye habari za udaku mtandaoni.

Hii inawezekana kwamba Nassib anataka madeni kodi yalipwe na Joe, kwani yeye analipa gharama za kila siku za redio.

Na kwa miezi kama minne hivi mishahara ya watumishi wasio mastaa wakubwa imekuwa na utata kidogo pale.

Asante b... Mwalimu wangu wa uandishi kaka mzuri anastahili pongezi. Alinionyesha njia za uandishi, nami nazingatia.

Tatizo watu wabishi b..., wanadhani haya mambo tunaamka tu na kuandika bila uhakika.
 
Kwenye kuhabarisha ni lazima ubishi uwepo kwa kuwa hii siyo taarifa ya press conference, bali ni taarifa ya kuchimba.

So, ni kama ilivyokuwa na Thomaso alipopokea taarifa za Yesu, alianza kwa kubisha hadi Yesu alipomtokea ndiyo akaamini.

Na habari ikiwa haisababishi mjadala wowote (ubishi ni mjadala), basi hiyo habari waswahili wa siku hizi hutumia neno la haina mashiko.

Ova
 
Dada yangu hilo eneo ni field yangu japo sasa nafanya kitu kingine, ila ninacho kizungumza na kijua theoretical mpaka mathematical.

Wewe kama unakubali kudanganywa ni ww, ila Frequency moja haziwezi kuisha wala kuwa mali ya mtu,anaye zimiplan,kuzicontrol,kuzimonitor,kuzimiliki na kuengineer ni TCRA.
Kila mkoa una idadi ya frequency, kama zikishajaa basi unalazimika kwenda mkoa mwingine. Ndiyo maana akina Mjini FM wanapitia kwingine na ofisi ziko Dar.

Hapo nyuma kuna mtu mmoja, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa kigogo JW, alianzisha redio ya dini na alilazimika kutumia Frequency na Bakwata ili aruke Dar.

Studio zilikuwa pale Al Haramain, ila baadaye kuna mambo alifanya sivyo ndivyo, Bakwata wakaamua kuchukua Frequency zao. Jamaa akaamua kuachana na redio.

Hata Eric Shigongo akiamua kuanzisha redio leo hii, itaruka Dar, kwa sababu ana frequency kitambo za hapo Dar.

Nyie wajuzi wa mambo sijui kwanini huwa mnachelewa mpaka walugaluga wanatusumbua hapa.
Asante kwa kuweka mzani sawa b...
 
Back
Top Bottom