Wasafi Media Mtegoni. Diamond, Kusaga wavurugana

Wasafi Media Mtegoni. Diamond, Kusaga wavurugana

Bakhresa sio mogul wa media kwamba atafanya kufa au kupona apate jambo lake kwenye frequency.
Wala hajaianzisha UFM ili impe faida ya kifedha direct, bali atangaze bidhaa/huduma zake na hasa kwa vile Azam ina mkataba ligi kuu. Ndio maana UFM imejikita zaidi kwenye michezo.

UFM kwa Bakhresa ni kama mkuu wa mkoa alime ekari moja ya mahindi, jua likiwaka usidhani atalia na kusaga meno kwamba sasa atakula wapi. Ukitaja wakulima wa mahindi, huyo mkuu wa mkoa mtoe.
Mbona unatumia nguvu nyingi kubishana na wajinga?
 
Hivi vitu ni optional halafu unaweza kufika dau ya mmiliki wa frequence nzuri anazohold nae akagoma sio lazma akuuzie sababu na yeye sio njaa kivile

Pili ni huwezi jua hata io 107.3 je km nayo alinunua? Na ndio aliyoipata


FIkiria nje ya boksi
Umefafanua vizuri mkuu, ni kama Joe hauzi frequency kwa bei yoyote, kama ukizitaka mgawane umiliki wa hiyo redio.

Hata huyo SSB ni hizo UFM na UTV ndizo zimeanzia hapo TZ, nyingine zimeanzishiwa kwingine huko na TZ zimekuja kuruka tu kwa kisimbuzi.

Ova
 
Umefafanua vizuri mkuu, ni kama Joe hauzi frequency kwa bei yoyote, kama ukizitaka mgawane umiliki wa hiyo redio.

Hata huyo SSB ni hizo UFM na UTV ndizo zimeanzia hapo TZ, nyingine zimeanzishiwa kwingine huko na TZ zimekuja kuruka tu kwa kisimbuzi.

Ova
Kwani wale waliomeza madesa ya darasani wako wapi lakini? Wajuzi mmekuja wamepotea.
Natamani waje wabishe tena.
 
Na yule kusaga aliyekuwepo jana na huyo diamond pamoja na mendez viwanja vya leaders, ni crones wale kwa tony osborn.
Au hapokei siimu kivipi?
Si ndio waandaaji wa show ya jana ile.
Kuna mtu anapromoti kiredio chake aliiga kwenye lebo akapoteana tunamkaribisha kwenye media tumtoe kinyesi
 

Wakurugenzi wa Wasafi Media, Joseph Kusaga na Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ wanaripotiwa kukosa maelewano kati yao juu ya uendeshaji wa media hiyo inayomilikiwa na wawili hao.

Chanzo ni TRA
Diamond ambaye amekuwa akitafutwa na maafisa kodi kwa muda mrefu, huku yeye akitumia 'janja janja' kuwakwepa, maafisa kodi hao wamehamishia majeshi kwa Joseph Kusaga.

Joseph Kusaga ambaye majukumu ya uendeshaji amemwachia Diamond, amekuwa akimpigia simu mara nyingi Diamond bila mafanikio.
Hivyo Diamond anawakwepa maafisa kodi, na huku simu za Kusaga pia hapokei.

Kusaga achoshwa na mabifu ya Diamond!
Inaarifiwa kuwa Kusaga amekuwa akilalamika mara nyingi juu ya mabifu ya Diamond na watu wengi ambayo yanaikwamisha Wasafi Media kukua.

Wakati anaanzisha media hiyo 2016, alikuwa na malengo makubwa ya kuikuza kuwa kubwa pengine kuizidi Clouds Media ambayo ni mali ya familia yao. Hivyo kupitia umaarufu wa Diamond alitegemea kuvuna wasikilizaji kutoka kila pembe ya nchi jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limefanikiwa ila kikwazo kikiwa ugomvi wa Diamond na watu wengi ambao wengi hutumia mabifu hayo kama fursa ya kuikwamisha Wasafi Media.

Kusaga Amgeukia Ali Kiba…
Habari za uhakika ni kwamba mastermind huyo wa biashara za vyombo vya habari na nyinginezo lukuki, ameelekeza nguvu zake kwa hasimu wa Diamond, Ali Kiba.

Wawili hao (Kusaga na Ali) wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha masuala muhimu likiwemo jina rasmi la kutumika kuitambulisha Media hiyo.

Kupitia chanzo changu makini nimefanikiwa kunasa jina linalopewa kipaumbele, Kings Media (Kings TV & Kings FM).

Pia watangazaji ambao tayari wameshawekwa kwenye list ni Abdallah Ambua ‘Dullah Planet’ aliyeng’oka EATV na EA Radio hivi karibuni, pamoja na Khalid Mohamed ‘TID’.

Kusaga na utajiri wa frequencies!
Kwa wafuatiliaji wa masuala ya media hasa radio, watakuwa wanafahamu ya kwamba hivi sasa hakuna frequency mpya hapa jijini Dar Es Salaam.

Yaani kwamba ukitaka kuanzisha redio huwezi kupata mawimbi ya kukuwezesha kusikilizwa Dar, labda ununue (frequency) ambayo inamilikiwa na wengine kisha uibadilishe kuwa redio yako.

Wajanja wa mjini wamezihodhi, akiwemo Joseph Kusaga ambaye anaarifiwa kuwa nazo kwa idadi ambayo haifahamiki.

Kupitia chanzo changu nyeti,

Nifah.
Kings FM ni radio ipo Njombe mjini . Labda watafute jina mpya
 
Nilivyomuelewa jamaa ni kwamba kuna watu tayari wameshazinunua hizo frequency toka TCRA kwahio ukitaka kuanzisha kituo chako, lazima ununue kwa watu ambao walishazinunua hizo frequency toka TCRA maana TCRA washauza kila frequency kwa hapa dar
Nyie ndio wale watu wanaoamini mpaka sasa kuwa Michael Jackson alisema bongo inanuka.
 
Back
Top Bottom