Arusha Mfanyabiashara tajiri wa mawe ndugu Temu amefariki dunia na kuacha kizaazaa nyuma. Bwana huyo ana migodi, magari sita, mashamba, majumba na mahoteli na maviwanja.
Alioa mke aitwae Yasinta ndoa ya kanisani.
Akazaa nae watoto 5 Kama kawa huko chuga hawa mabilionea hua wanapenda chovyachovya.
Baba akazaa nje mtoto wa kwanza akaleta home mke alee, akanogewa akazaa mwingine tena akapeleka nyumbani mkewe alee. Mke akawa hana namna. Kiroho safi analea.
Mke nae amezaa watoto watano tena mmoja mchanga, ukijumlisha wawili wa baba wanakuwa saba.
Mama akaleta housegirl, baba alivyo na tamaa akaanza kutembea na housegirl mpaka akapata mimba. Baba akamfanya mke mdogo, akamjengea na akazaa naye watoto wawili. Yule housegirl ndo akawa na nguvu, mke mkubwa akawa anadharauliwa.
Mke kikawa kinamuuma lakini sasa ndo ashazaa watoto watano akaamua avumilie.
Mara paaap, tajiri kaumwa. Kapelekwa Muhimbili, kwa mapenzi ya Mungu akatwaliwa. Picha ndo ilianzia hapo, mke mkubwa akafika Muhimbili akashangaa anaambiwa na binamu wa mume eti kaa pembeni tutasimamia Mali za watoto na haki zao, akashangaa kiajee Sasa? Lakini kwavile yeye ndo mwenye cheti Cha ndoa akakabidhiwa mwili na cheti cha kifo.
Soma Pia: Arusha: Mfanyabiashara wa madini auawa mlima wa maombi, wauwaji watuma meseji
Ndugu na jamaa na marafiki wakaleta mwili Arusha mochwari ya Mt meru. Mke mkubwa akaelekeza mume azikwe wapi.
Sasa ndugu, marafiki na mke mdogo wakapanga pa kuzika na wakamweka kando bi mkubwa.
Siku ya kuzika bi mkubwa akaingia mahakamani kwa hati ya dharura kuomba zuio na akafanikiwa, issue ilikuwa serious kaburi lishachimbwa, mapadre ikabidi wakafanye Dua pale ya kufunga kaburi tupu na Ile pilau ya msiba wadudu waliifakamia sana.
Sasa leo amri imetolewa na mahakama mke halali amzike mume wake... Housegirl na wale ndugu hawaamini kilichotokea. Eti ndugu na marafiki wanapanga kususia maziko.
Na mke mkubwa amesema mume wangu ni mkristu na ana mke mmoja tu. Akimaliza kuzika anakusanya mali za mumewe baada ya kufungua mirathi.
Housegirl ataambulia simu na cheni za marehemu na nguo..ambazo hata hivyo bi mkubwa anaulizia vipo wapi. Housegirl amegeuka suria..ila wanae watapata mgao wa mali
Wadada wa kazi mnapoenda kufanya kazi kwenye nyumba za watu acheni tamaa kwani hamjui baba na mama wameanzia wapi na wamesotaje kupata mali. Pia ndugu na marafiki acheni upumbavu wa kuingilia mali za marehemu ikiwa ana mke na watoto