Yoav Gallant
JF-Expert Member
- May 23, 2023
- 2,122
- 4,699
Kosa alifanya mke kuleta house girl pisi kali
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh kumbe ndivyo ilivyokuwaga? Niliona title kwa millard ila sikufuatilia.Arusha Mfanyabiashara tajiri wa mawe ndugu Temu amefariki dunia na kuacha kizaazaa nyuma. Bwana huyo ana migodi, magari sita, mashamba, majumba na mahoteli na maviwanja.
Alioa mke aitwae Yasinta ndoa ya kanisani.
Akazaa nae watoto 5 Kama kawa huko chuga hawa mabilionea hua wanapenda chovyachovya.
Baba akazaa nje mtoto wa kwanza akaleta home mke alee, akanogewa akazaa mwingine tena akapeleka nyumbani mkewe alee. Mke akawa hana namna. Kiroho safi analea.
Mke nae amezaa watoto watano tena mmoja mchanga, ukijumlisha wawili wa baba wanakuwa saba.
Mama akaleta housegirl, baba alivyo na tamaa akaanza kutembea na housegirl mpaka akapata mimba. Baba akamfanya mke mdogo, akamjengea na akazaa naye watoto wawili. Yule housegirl ndo akawa na nguvu, mke mkubwa akawa anadharauliwa.
Mke kikawa kinamuuma lakini sasa ndo ashazaa watoto watano akaamua avumilie.
Mara paaap, tajiri kaumwa. Kapelekwa Muhimbili, kwa mapenzi ya Mungu akatwaliwa. Picha ndo ilianzia hapo, mke mkubwa akafika Muhimbili akashangaa anaambiwa na binamu wa mume eti kaa pembeni tutasimamia Mali za watoto na haki zao, akashangaa kiajee Sasa? Lakini kwavile yeye ndo mwenye cheti Cha ndoa akakabidhiwa mwili na cheti cha kifo.
Soma Pia: Arusha: Mfanyabiashara wa madini auawa mlima wa maombi, wauwaji watuma meseji
Ndugu na jamaa na marafiki wakaleta mwili Arusha mochwari ya Mt meru. Mke mkubwa akaelekeza mume azikwe wapi.
Sasa ndugu, marafiki na mke mdogo wakapanga pa kuzika na wakamweka kando bi mkubwa.
Siku ya kuzika bi mkubwa akaingia mahakamani kwa hati ya dharura kuomba zuio na akafanikiwa, issue ilikuwa serious kaburi lishachimbwa, mapadre ikabidi wakafanye Dua pale ya kufunga kaburi tupu na Ile pilau ya msiba wadudu waliifakamia sana.
Sasa leo amri imetolewa na mahakama mke halali amzike mume wake... Housegirl na wale ndugu hawaamini kilichotokea. Eti ndugu na marafiki wanapanga kususia maziko.
Na mke mkubwa amesema mume wangu ni mkristu na ana mke mmoja tu. Akimaliza kuzika anakusanya mali za mumewe baada ya kufungua mirathi.
Housegirl ataambulia simu na cheni za marehemu na nguo..ambazo hata hivyo bi mkubwa anaulizia vipo wapi. Housegirl amegeuka suria..ila wanae watapata mgao wa mali
Wadada wa kazi mnapoenda kufanya kazi kwenye nyumba za watu acheni tamaa kwani hamjui baba na mama wameanzia wapi na wamesotaje kupata mali. Pia ndugu na marafiki acheni upumbavu wa kuingilia mali za marehemu ikiwa ana mke na watoto
Ukoo wa mume unahusikaje.Hiyo mirathi sio nyepesi.
Nawaza tu muhtasari wa kikao cha mirathi. Utasainiwa vipi na ukoo wa mume na hao watoto wa nje. Maana mahakama watauitaji kwenye mirathi
Wanawake hao ndio walivyo akipata nafasi ya kuwa mchepuko tayari anajiona mke. Ukiwa mzembe lazma atakuharibia kwa wife akiamini anaweza pindua meza aolewe yeye.shida ilianzia kwa mke mdg kutaka kujiweka mbele angekua mpole haya yasinge mkuta
sema wapambe wake wanamwendesha na kumshauri hovyo wakiwa na lengo apate mali zote wazitumbue
iran na israel wachapane tu tujue moyo sio kukaa na hisia za kibwege bwege za nani atapigwa
Mabinti waache tamaa, watapigwa na kitu kizito hawatakuwa na pakukimbilia
Wewe ni mpuuzi.. uwe raped uzae na watoto tena wawili?????...Aache tamaa kivipi ? Binti karepiwa ndani weeee, halafu akafanywa mke.
Kazaa watoto wawili, kajengewa nyumba, kabanwa mbavu miaka kibao, tena mwanzoni kwa kurepiwa, kila aina za milalo, ya kisheria na kinyume na kisheria, huyo ni common law wife! Katoa huduma, anastahili chake, hana tamaa!
Tamaa aje?Millard Ayo huyo..ameacha kipengele kikubwa kuhusu huyo mchepuko wa marehemu.
Mabinti waache tamaa, watapigwa na kitu kizito hawatakuwa na pakukimbilia
Nimemsoma huyo mwehu nimeishia kucheka tu. Ubakwe uzae mara mbili[emoji23][emoji23][emoji23] mashankupe ya mjini tu na zaid hata jamaa nae alikosea sana unamke wako mzuri unahangaika na washenzi wengine wa kazi gani..Wewe ni mpuuzi.. uwe raped uzae na watoto tena wawili?????...
Na wanatafutaga upenyo tu kidogo tu, na mke unaruhusu binti anamfulia boksa mumeo, mara amtengee maji ya kuoga mara chakula, mara akirud ampokee, na faza unaruhusu tu,Siyo kosa la Mahouse girl! Ni makosa ya Mama wenye nyumba!
Mama ukiruhusu housegirl tayari jua huyo ni mke mwenza wako!
Nyumba ikigonga gari ni habari ila gari ikigonga nyumba si habari..kati ya ndugu 'bilionea marehemu' na house girl nani alimuanza mwenzie?Arusha Mfanyabiashara tajiri wa mawe ndugu Temu amefariki dunia na kuacha kizaazaa nyuma. Bwana huyo ana migodi, magari sita, mashamba, majumba na mahoteli na maviwanja.