Wasaidizi wa kazi kutembea na Baba wenye nyumba kuna madhara. Dada wa Arusha apokonyea Mwili wa marehemu

Wasaidizi wa kazi kutembea na Baba wenye nyumba kuna madhara. Dada wa Arusha apokonyea Mwili wa marehemu

Arusha Mfanyabiashara tajiri wa mawe ndugu Temu amefariki dunia na kuacha kizaazaa nyuma. Bwana huyo ana migodi, magari sita, mashamba, majumba na mahoteli na maviwanja.
Alioa mke aitwae Yasinta ndoa ya kanisani.

Akazaa nae watoto 5 Kama kawa huko chuga hawa mabilionea hua wanapenda chovyachovya.

Baba akazaa nje mtoto wa kwanza akaleta home mke alee, akanogewa akazaa mwingine tena akapeleka nyumbani mkewe alee. Mke akawa hana namna. Kiroho safi analea.
Mke nae amezaa watoto watano tena mmoja mchanga, ukijumlisha wawili wa baba wanakuwa saba.

Mama akaleta housegirl, baba alivyo na tamaa akaanza kutembea na housegirl mpaka akapata mimba. Baba akamfanya mke mdogo, akamjengea na akazaa naye watoto wawili. Yule housegirl ndo akawa na nguvu, mke mkubwa akawa anadharauliwa.

Mke kikawa kinamuuma lakini sasa ndo ashazaa watoto watano akaamua avumilie.

Mara paaap, tajiri kaumwa. Kapelekwa Muhimbili, kwa mapenzi ya Mungu akatwaliwa. Picha ndo ilianzia hapo, mke mkubwa akafika Muhimbili akashangaa anaambiwa na binamu wa mume eti kaa pembeni tutasimamia Mali za watoto na haki zao, akashangaa kiajee Sasa? Lakini kwavile yeye ndo mwenye cheti Cha ndoa akakabidhiwa mwili na cheti cha kifo.

Soma Pia: Arusha: Mfanyabiashara wa madini auawa mlima wa maombi, wauwaji watuma meseji

Ndugu na jamaa na marafiki wakaleta mwili Arusha mochwari ya Mt meru. Mke mkubwa akaelekeza mume azikwe wapi.

Sasa ndugu, marafiki na mke mdogo wakapanga pa kuzika na wakamweka kando bi mkubwa.

Siku ya kuzika bi mkubwa akaingia mahakamani kwa hati ya dharura kuomba zuio na akafanikiwa, issue ilikuwa serious kaburi lishachimbwa, mapadre ikabidi wakafanye Dua pale ya kufunga kaburi tupu na Ile pilau ya msiba wadudu waliifakamia sana.

Sasa leo amri imetolewa na mahakama mke halali amzike mume wake... Housegirl na wale ndugu hawaamini kilichotokea. Eti ndugu na marafiki wanapanga kususia maziko.

Na mke mkubwa amesema mume wangu ni mkristu na ana mke mmoja tu. Akimaliza kuzika anakusanya mali za mumewe baada ya kufungua mirathi.

Housegirl ataambulia simu na cheni za marehemu na nguo..ambazo hata hivyo bi mkubwa anaulizia vipo wapi. Housegirl amegeuka suria..ila wanae watapata mgao wa mali

Wadada wa kazi mnapoenda kufanya kazi kwenye nyumba za watu acheni tamaa kwani hamjui baba na mama wameanzia wapi na wamesotaje kupata mali. Pia ndugu na marafiki acheni upumbavu wa kuingilia mali za marehemu ikiwa ana mke na watoto
Ni somo zuri hata kwetu wanaume,tujipange vyema kwenye haya maisha!Hatujui kesho yetu .
 
Kaandika kiushabiki mwili umetoka dar na mkewe na msiba uko kwa mke moshono....yeye mkewe ndio anadai cheni,pete magari yaletwe kwake ndio azike,mara akabadili gia angani apewe doc za mali....marehemu alikimbia kwake mwaka mzima kwa vile mke malaya na watoto wawili mabodaboda wamemzalisha....ukiowa changu tegemea matatizo kwenye maisha yako....istoshe mke hana document yeyote hapo anapiga kelele tu
Hata kama hana Doc yoyote,kisheria ye ndio anatambulika msimamizi wa mali zote,hao walioshikiria Doc wanajisumbua tu,

Japo simtetea huyo mwanamke kama yasemwayo nikweli,ila ndoa zenu wakristo ngumu sana
 
Wanaume wanakufa kwa mengi, mengine ya kujitakia kuwa na husiano zaidi ya moja ni kujipa misuko suko bila sababu. Its mentally and physically draining 😪. R.I.P tajiri wa madini pole kwa wake na watoto.
Mbona baba wa imani Ibrahim pia alikuwa na wake wengi na aliishi miaka 150,na nabii suleiman wake elfu moja na aliishi umri mrefu pia,

Mwanaume kuwa na mwanamke mmoja ndio kunafanya ufe mapema kama haujui bibie
 
Na mara nyingi wanaume wenye wanawake wengi na watoto kutoka kwa wamama tofauti huwa hawanaga maisha marefu sijui kwa nini. Huenda stress za hao wanawake au situation nzima ikawa inachangia au kukawa na namna ya infanyika atangulie kuzimu na mara nyingi hao hao wake zake wanahusika.

Utakuta siku ya msiba mke wa ndoa wala hana machozi wala halii na ukimuona ni kama amepata relief kwa huyo jmaa kuondoka. Wanaolia ni mama mzazi na dada wa marehemu lakini mwenye haki zote ni yule yule mke anayefurahia rohoni kuondoka kwa huyo fala..
Halafu ukute we ni dume
 
Inafunguliwa kesi mahakama inachagua so hapo muhitasari kwa mazingira hayo unakuwa haupo
Mahakama inachaguwaje msimamizi wa Mirathi ambae hana documents zozote!? Hata cheti cha kifo huna,unapewaje usimamizi wa Mirathi na Mahakama!? Labda kama huyo Muheshimiwa mshikaji wako na kaamua kuendesha kazi za Mahakama kishikaji hapo sawa!! Tena siku hizi naona wameongeza hadi takwa la wadhamini wawili ambao siyo warithi, yaani msimamizi wa Mirathi lazima ulete wadhamini wawili na wanakula kiapo pia!!
 
Mahakama inachaguwaje msimamizi wa Mirathi ambae hana documents zozote!? Hata cheti cha kifo huna,unapewaje usimamizi wa Mirathi na Mahakama!? Labda kama huyo Muheshimiwa mshikaji wako na kaamua kuendesha kazi za Mahakama kishikaji hapo sawa!!
Mali za marehemu zinakusanywa zijulikane hvo kukosa document sio ishu
 
Mahakama inachaguwaje msimamizi wa Mirathi ambae hana documents zozote!? Hata cheti cha kifo huna,unapewaje usimamizi wa Mirathi na Mahakama!? Labda kama huyo Muheshimiwa mshikaji wako na kaamua kuendesha kazi za Mahakama kishikaji hapo sawa!!
Cheti cha kifo ni public document hata wewe ukitaka cheti cha kifo cha Sokoine unapewa na RITA bora uombe na ulipe fee.
 
Umekufa umeacha aibu bado uliowaacha wanautaabisha mwili wako wanakuzidishia aibu.
 
Cheti cha kifo ni public document hata wewe ukitaka cheti cha kifo cha Sokoine unapewa na RITA bora uombe na ulipe fee.
Cheti ni kimoja tu kinatolewa, siyo kila anaetaka anapewa chake, upande mmoja wa marehemu wamesha chukua cheti cha kifo na wanacho, sasa huyo anaetaka kufungua mirathi peke yake atafungua na nini wakati ule upande wenye cheti hawaelewani!!?? Hapo dawa wakae chini pande zote mbili zielewane ili mambo yasiwe magumu kwa kila pande!!
 
Mkuu Mahakama tangulini ikachangua msimamizi wa mirathi kwa sheria zipi? Kikao cha ukoo ndiyo kitampiticha msimizi wa mirathi.
Nilimaanisha anayetambuliwa na mahakama kwa mujibu wa kikao cha familia
 
Back
Top Bottom