Wasamaria:Fahamu chanzo chao na kwanini walikuwa hawachangamani na Wayahudi!

Asili ya wasamalia na kutengwa kwao ni hii:
Hapo kale, baada ya waisraeli kuchukuliwa utumwani babyloni waliachwa waisrael wachache kulinda mashamba. Watu kutoka babyloni pia walikuja israeli kutawala (kwa niaba ya mfalme wa babyloni). Mji wa Samaria ndio ukawa makao ya hawa watu kutoaka babyloni. Wageni hawa hawakufuata torati, walikuja na sheria zao na utaratibu wao wa kuabudu. wasamaria waliingia katika mtego huu na kuanza kufuata tamaduni za wageni na kusahau miiko yao.

Baada ya waisraeli kulejea kutoka uhamishoni babyloni, waliukuta mji wa samaria ukifuata tamaduni za kigeni, na ndio chanzo cha mji huu na watu wake kutengwa
 
Sii sahihi kusema "jambo lile lilimkera Mungu"

Ni sahihi kusema jambo lile lilimchukiza Mungu.
 
Hii imenishawishi kusoma zaidi
 
Uliyashuhudia au ulisoma kwenye maandiko ya wazungu?
Je ni kweli Mkwawa alijipiga bunduki?
Je ni kweli binadamu tumetokana na sokwe( evolution of man)
What about Gondwanaland?
Je kweli dunia ni duara?
Ni kweli ndege ya Malaysia ilipotea?
 
Uliyashuhudia au ulisoma kwenye maandiko ya wazungu?
Je ni kweli Mkwawa alijipiga bunduki?
Je ni kweli binadamu tumetokana na sokwe( evolution of man)
What about Gondwanaland?
Je kweli dunia ni duara?
Ni kweli ndege ya Malaysia ilipotea?
Wewe umeshuhudia mimi nipo?

Kushuhudia maana yake nini?

Sent from my Kimulimuli
 
Al-Watan wanaopenda kufuatilia maswala ya Kinjekitile Ngwale tu wachache,ukitaka kuamini,jaribu kuingia Jukwaa la Historia!
Lakini pia,ukitaka kuuza vitabu sokoni,mkononi una cha Waisrael na Kinjekitile,we unahisi kipi kitaanza kuisha kwa kununuliwa?
 
Dragoon mkuu,asante kwa mchango wako!
Ila ningependa kuweka kumbukumbu sawa!
Wayahudi waliorudi Uyahudini toka Babylon au Babeli ufalme wa Kusini,ni tofauti na wale waliochukuliwa utumwani toka Ufalme wa Kaskazini wa Israel!
Baada ya Ufalme wa Israel kumegwa na kuzaa falme mbili za:Yuda na Israel!
Wa kwanza kuharibiwa ulikuwa ule wa kaskazini uliokuwa unaitwa Israel wenye makao makuu yake katika mji wa Samaria!
Pia kama utakumbuka,mfalme aliyehusika na uharibifu huu aliitwa Shalmaneer wa dola ya Assyria ambayo makao makuu yalikuwa katika mji wa Ninawi!
Waisrael hawa hawakuwahi kurudi katika Nchi ya Ahadi na ndio mwisho wao tangu mwaka 722 K.K!
Ukifa ufalme wa kusini,nao ulianguka mwaka 586 mbele ya mkono wa Nebkadineza,na watumwa aliowachukia waliruhusiwa kurudi Nchi ya Ahadi na hawa ndio walioendeleza taifa la Israel!
 
Unaongelea historia ya Wayahudi iliyoandikwa na Wazungu gani mwaka gani? Labda tuanzie hapo.

Maana unaongelea Wazungu kwa kutaja nchi zilizoanza juzi hapa mpaka naona unataka kushindana kuogelea na mimi katika dimbwi la sentimeta tano.

Wazungu Gni walioanza Juzi?,
 
Unaongelea historia ya Wayahudi iliyoandikwa na Wazungu gani mwaka gani? Labda tuanzie hapo.

Maana unaongelea Wazungu kwa kutaja nchi zilizoanza juzi hapa mpaka naona unataka kushindana kuogelea na mimi katika dimbwi la sentimeta tano.
Kuna vitu ambavyo ni vigumu sana kudili navyo Mkuu,historia ya kidini na historia ya kikabira.

Lakini jf hawakuwa wajinga kuweka majukwaa tofauti,hiyo mada ebu kaulize jukwaa la siasa naisi utapata majibu mazuri sana.

Mengine itakuwa visa tu.

Sent from my Bravo Z11 using JamiiForums mobile app
 

Kwa nini unafikiri dini na siasa ni vitu tofauti?

Sent from my Kimulimuli
 
Kama uliisoma BIBLIA kwa nguvu za roho mtakatifu akakusaidia kuielewa usingeandika uongo huu,ila kama ulisoma kama vitabu vya historia uko sahihi, kutochangamana kwa wayahudi kuliagizwa na Mungu mwenyewe akiwaonya watakapofika katika nchi ya ahadi,wasioe wala kuoa Binti za makabila walioyakuta huko wala wasichangamane kwani walikuwa taifa teule la Mungu na yale makabila mengine yalikuwa yakiabudu miungu, ukisoma agano lakale hutokuta wakiitwa wasamaria kama usemavyo kulikuwa na Israel na Yuda. Wayaudi walikuwa ni Israel na Yuda kumbuka pale kisimani yule mwanamke msamaria alipoombwa maji alisema hawachangamani sababu Yesu ni myahudi nae msamaria, kumbuka mfano wa msamaria mwema pia utagundua ulichoandika ni upotoshaji labda uwadanganye wenye kusoma BIBLIA,ila kwa mwenye kulijua neno la Mungu hutompata. Asante ukipenda utajifunza kwa michango ya watu.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
enoah asante kwa mchango wako,kuna maeneo wote tupo pamoja,ila katika moja!
Wasamaria walikuwa sio Wayahudi wala Waisrael kwa asili!
Bali ni mjumuiko wa makabila mengi ya kigeni yaliyochukuliwa toka mataifa mbalimbali toka katika makoloni ya Mfalme wa Waassyria kuja kuijaza nchi ya Ufalme wa Kaskazini wa Israeli baada ya kuwaaua na kuwabeba waliobaki baada ya kuuteketeza mji wa Samaria na kumuua Mfalme wao aitwaye Hoshea!
Na ukumbuke ufalme wa Kaskazini wa Israeli uliundwa na makabila kumi ya taifa la Israeli,makabila ambayo yalipotelea utumwani kwani hayakufanikiwa kurudi tena Nchi ya Ahadi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…