Wasamaria:Fahamu chanzo chao na kwanini walikuwa hawachangamani na Wayahudi!

Mkuu Al-Watan naona unatoa darasa mujarab

Sent From Ikulu-Magogoni street
Hahaha,
Darasa muhimu.

Eti Mangi umetoka kwenu kuna majesty yote ya Mlima Kilimanjaro watu wanatoka dunia nzima kuja kushangaa barafu iliyo nyuzi 3 kusini ya Ikweta, jambo la ajabu.

Halafu unaambiwa kwenu sikitu, ukiswali shurti uelekee Kibla!

Unaambiwa Jerusalem ndiyo mji mtakatifu.

Haiyumkiniki.

Ikulu Magogoni Street tutachelea kulimia meno mkuu.
 
Sawasawa.
Swali kuu: wapo wapi descendants wa makabila yale mengine 10? Maana si sahihi kuwachukulia Jews (ambao ni makabila mawili tu) kama hao tu ndio uzao wote wa Yakobo na babu yake Ibrahim!
 
Utotole mkuu,acha nitafiti zaidi jibu lake utalipata!
Ila hata Biblia yenyewe haisemi chochote kuhusu makabila hayo kumi na wala haisemi lolote kuhusu vizaria vyao tangu watwaliwe utumwani!
 
Utotole mkuu,acha nitafiti zaidi jibu lake utalipata!
Ila hata Biblia yenyewe haisemi chochote kuhusu makabila hayo kumi na wala haisemi lolote kuhusu vizaria vyao tangu watwaliwe utumwani!
Sure. Ukisikiliza wasemaji wengi toka sehemu mbalimbali unakuta tayari mataifa ya ulaya yameshawagawana wana wa Yakobo. Nchi nyingi za ulaya zimeshapewa makabila yaliyopotea ya Israel. Eg. Descendants wa Reuben wanadai Ni Wafaransa, etc. Of course schools of thought ziko nyingi Sana.
 
Unaweza kunisaidia sehemu yoyote ya Torati inayoonesha Wayahudi wasichangamane kabisa na mataifa/makabila mengine yasiyoabudu Mungu wao? Niko interested kujifunza hapa zaidi
unapotaka kujifunza ukikuta thread yoyote pitia kwanza majibu ya mwanzo usisumbie watu kwa kutaka kujiridhisha nafsi yako. swali lako lishajibiwa vizuri kabsa hapo nyuma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
usipende kufananisha vitu ambavyo haviendani kijana ilimradi ujifurahishe. unawalazimisha watu wafuate akili yako?! ushajua wanachopenda sasa wakishafahamu ya kinjekitile vipi watawapa bunduki badala ya maji mwenyewe umekua umekuta maandiko tu yaloandikwa na wazungu alafu wajitia mjuaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unawezaje kumlazimisha mtu ambaye humjui, humuonina wala huna nguvu yeyote juu yake, kwa kupitia internet?

Huyo anayeweza kulazimishwa hivyo ni mtu au konokono?
 
Nadhani unahitaji kujifunza zaidi kuhusu makabila ya Israel na namna ya Taifa LA Yuda ililivyopatikana, Wasamaria na wayahudi wote ni waisrael Jifunze kwanza ilikuaje Baadhi ya waisrael wawe wayahudi na tabaka jingine waitwe Wasamari?? Ukijua utofauti wa Myahudi na Mwisrael utatoa maana na kwa nini wasichangamane
 
Unaweza kunisaidia sehemu yoyote ya Torati inayoonesha Wayahudi wasichangamane kabisa na mataifa/makabila mengine yasiyoabudu Mungu wao? Niko interested kujifunza hapa zaidi
anyway nilichokielewa mimi nikwamba wengi katika hii hoja hawajui tafsiri ya neno myahudi,msamalia na muisraeli,
Taifa la israeli lilikuwa na makabila 12 ndani yake kwapamoja yanaunda hilo taifa ,baada ya kifo cha mfalme suleimani hili taifa la israeli liligawanyika sehem mbili kabila 10 zilizokuwa zinakaa kaskazini mwa hilo taifa zilikataa kuendelea kutawaliwa na kabila la yuda so wakajitenga wakaweka makao yao makuu kwenye mji wa SAMALIA na taifa lao likawa linaitwa ISRAELI na kabila zingine mbili zilizobaki ilikuwa ni YUDA (JUDAH) na BENJAMINI wao walikuwa wanakaa kusini mwa nchi so wakabaki na taifa lao likawa linaitwa YUDA,na makao yao makuu yakawa Yerusalemu na wakawa wanatawaliwa na watu wa nyumba ya daudi kama Mungu alivyowaagiza,sasa ukianza kusoma 2Wafalme 16 wale waliobakia kusini wakaanza kutambulika kama WAYAHUDI (JEWS) kutokana na jina la taifa lao kuwa YUDA(JUDAH),sasa ukiendelea kusoma mbele zile kabila 10 za kaskazini zilizojitenga na ambazo hazikuwa zinatawaliwa na wazaliwa wa nyumba ya Daudi kama ilivyokuwa desturi badala yake zilitawaliwa na wafalme wasiofuata misingi ya Mungu wa baba zao wakachukuliwa utumwani na Mfalme wa ASSYRIAN wakaenda huko wakaendelea kutawaliwa na kuchangamana na watu wa mataifa wa huko ndio wakaitwa WASAMARIA,sasa kipindi Yesu anakuja alikuta bado huo mgawanyiko upo ule ufalme wa kaskazini (Samaria) na ufalme wa kusini (YUDEA) ambayo ilikuwa chini ya utawala wa WARUMI(ROMAN RULE),so utaona kwanini wayahudi walikuwa hawataki kuchangamana na wenzao tangia awali ,
Yesu na wanafunzi wake waliihubiri injili Judea yote kutafuta kondoo waliopotea kwa muda wa miaka mitatu na nusu then wayahudi wakamkataa Yesu kama Masihi wao wakafanikiwa kuwashawishi waroma kumuua Yesu na wakafanikiwa lakini baada ya siku tatu akafufuka akajionyesha wazi wazi kwa wanafunzi wake kabla ya kupaa kwenda mbinguni kuketi mkono wa kiume wa Mungu mwenye Enzi! ila kabla hajashikwa na kusulubiwa pale msalabani aliwaambia wanafunzi wake kuwa "Adhabu ya Wayahudi kumkaataa (soma kumb la torati 28) Mathayo 21:41,Yerusalemu itatwaliwa kimabavu na hekalu litavunjwa na wayahudi watachukuliwa utumwani kwenye mataifa yoote ya duniani, huu unabii ulitimia mwaka 70 baada ya Yesu ambapo mfalme TITUS aliyafanya hayo aliyoyasema Yesu!
So Waisraeli (zile kabila 10)au wasamalia waliadhibiwa wakatawanywa koote kama adhabu ya kuto kutii maagizo ya Bwana Mungu ,then YUDEA(JUDAH) nao wakatawanywa kama adhabu ya kumkataa masihi Yesu!
kinachofuata baada ya hapa ndio wakristo wengi tunakuja kutofautiana ...............Je hawa waliorudi pale wanaojiita taifa la israeli ndio wale waliotawanywa miaka takribani 2000 iliyopita?? au hawa ni fake na original bado wapo kwenye utumwa,dhiki,mateso na kila aina ya manyanyaso kama neno la Kristo linavyosema?????? kuna thread kama hii niliianzisha unaweza kuisoma pia kupitia hii link
https://www.jamiiforums.com/threads/uhalisia-wa-taifa-la-israeli.
 
Maelezo mazuri. Na aya yako ya mwisho ndilo swali kuu. Je hawa wanaoitwa Waisrael ambao kimsingi wanatarajiwa kuwa wale wa YUDA (jews) ndio wale wale kweli ambao walichukuliwa utumwani Babeli na kurudi na kisha tena kutawanywa enzi ya agano jipya? Au ni wengine walijipandikiza hapo? Je wale watokanao na makabila mengine 10 wako wapi hadi sasa?
 
Itakuwaje iandikwe na watu wanne na kila moja ina utofauti na nyengine? Iliyo kuwa sawa ni ipi ?

Post sent using JamiiForums mobile app
Ukisoma kitabu cha Injili ya Luka sura ya kwanza mstari wa kwanza utapata maana halisi ya kwa nini waandishi wa Injili wapo wanne na hata wakiwepo zaidi. Luka 1:1...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Isitoshe Yesu Kristo alipokuja duniani alileta sheria ya matendo ya imani, yaani shahidi wa mtu awe ni nafsi yake na si kama hapo mwanzo ilikuwa ni kama tu kutimiza wajibu na si kwa uwazi wa moyo na kwa kupenda. Ndiyo maana ni ngumu sana kupata haki kwa matendo ya sheria. Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo umemjibu bila shaka. Pia kulikuwa ugomvi kati ya wasamaria na wayahudi wakati wa kujenga hekalu, wakina Ezra walikutana na upinzani mzito sana kutoka kwa wakazi waliokuwa wameachwa katika mji ule hicho kikawa chanzo kukibwa kabisa cha uadui kati ya wayahudi na wasamaria, lakini wote walikuwa ni taifa moja hapo awali kabla ya uhamisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa inategemea sana unavutiwa na kitu gani zaidi katika kujifunza. Historia ya Biblia kwa mtu anayesoma kwa kumaanisha haibakii kuwa historia tu bali ni roho kamili inayo huisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utotole mkuu,acha nitafiti zaidi jibu lake utalipata!
Ila hata Biblia yenyewe haisemi chochote kuhusu makabila hayo kumi na wala haisemi lolote kuhusu vizaria vyao tangu watwaliwe utumwani!
biblia haisemi,ila inasema wameshapotea hawatarudi kamwe,

lakini ukweli ni kua baada ya israel kingdom kuanguka,na ikabaki Judah kingdom,
makuhani wa judah walihakikisha wanayapoteza maandiko ya israel kingdom,
kimsingi hizi nchi mbili baada ya kifo cha solomon,zilikua ni nchi adui,
kwahiyo waandishi na makuhani walihakikisha maandiko ya history na imani ya israel yanapotea,
mfano israel waliabudu mungu aitwae El na ndo asili ya neno el kuwa katika jina israel,
tofauti ya yahwew mungu wa wayahudi,

kimsingi baada ya solomon kufa na nchi kugawanyika,yale makabila 10 ndo yalibaki na jina la israel,
wakati utawala wa kusini uliokua umebaki na makabila mawili wakachagua kujiita Judea,
jina hilo ndo baadae wenyeji walijulikana kama wayahudi,na mungu wao ni simba wa yudah kwa maana ya yahwew ama jehova kiswahili,

kwa maana hiyo ni wazi kuwa unaweza kukuta muisrael,lakini asiwe myahudi,kwani uyahudi sio hata kabila bali asili yake ni yule mtoto wa jacobo alieitwa yuda,

maandiko yalichanganywa mno kama husomi critically,huwezi gundua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…