Wasambaza picha za ngono, wanaojiuza mitandaoni, waliojifanya mawakala wa Freemason wakamatwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Timu Maalum ya Kuzuia na Kupambana na Uhalifu wa Mtandaoni, huku ikiwashirikisha Polisi Mkoa wa Morogoro, wamefanya Operesheni maalum kuanzia tarehe 18/05/2022 hadi 26/06/2022 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Morogoro na kufanikiwa kuwakamata Julius Simon Mwabula @ Kibegi, miaka 20, Mhehe, mkazi wa Ifakara Morogoro na wenzake ishirini na mbili (22) kwa tuhuma za kufanya uhalifu kwa njia ya mtandao.

Watuhumiwa hao wamekuwa wakijifanya wao ni Wakuu wa shule, Waganga wa kienyeji, Ndugu wa wahanga, Wahudumu wa makampuni ya simu (customer care) au mawakala wa Freemason, ambapo huwatumia watu ujumbe mbalimbali kupitia namba tofauti za simu na kujifanya wanania ya kusaidia watu badala yake huishia kuwaibia ( kuwatapeli).

MFANO WA UJUMBE NI
"Halo ndugu mzazi mwanao shuleni amepatwa na matatizo na anaumwa sana hivyo tuma pesa haraka ili nimpeleke hospitali” na muhalifu huyo anatoa namba ya kutuma hiyo pesa na ukituma unakuwa umeibiwa.

Watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo wanavitumia kufanya uhalifu huo, vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:
  • Kompyuta mpakato (laptop) 2,
  • Kompyuta ya mezani (desk top) 1,
  • Simu za aina tofauti 28,
  • Flash 2,
  • Modem ya mitandao yote 1,
  • Kadi za simu za mitandao mbalimbali zaidi ya 50
Katika Oparesheni hiyo, watuhumiwa wengine wa makosa ya mtandao pia walikamatwa, ambao ni: Marry Samson Sibora @ ASHA ZUNGU miaka 23, Mzanaki, mkazi wa Sinza Mugabe na Zainabu Yahaya Omary @ official Manka , miaka 23, Mrangi, mkazi wa Buguruni Wanatuhumiwa kwa makosa ya usambazaji wa picha za ngono na kuuza mwili kwa njia ya Mtandao ya kijamii ikiwemo facebook, WhatsApp, Tinder na Exotic tz .

Watuhumiwa wote wamehojiwa kwa kina na taratibu za kisheria zinakamilishwa ili wafikishwe Mahakani haraka iwezekanavyo.

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka zingine za kishria, linatoa onyo kali kwa watu wanao jihusisha na uhalifu kwa njia ya mtandao na njia nyingine, kuwa Serikali na vyombo vyake imejipanga kupambana na uhalifu wa aina yoyote, na wahalifu popote walipo watafuatwa, kukamatwa na kupelekwa Mahakamani.

Aidha, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Watanzania wote kutumia mitandao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na kuwa waangalifu na vitendo vya utapeli, ikiwemo kuchukuwa tahadhari wakati wa kutuma pesa au kufanya biashara katika mitandao ili kuepuka kutapeliwa, pia watu wajiepushe kufanya biashara haramu mitandaoni kama vile za kuuza mili na ngono.

Muliro J. MULIRO– ACP
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu 23 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya utapeli kwa njia ya mtandao.

Kukamatwa kwa watu hao ni matokeo ya oparesheni maalum iliyofanywa na kanda hiyo kwa kushirikiana na timu maalumu ya Kuzuia na Kupambana na Uhalifu wa Mtandaoni.

Operesheni hiyo iliyofanyika kati ya Mei 18 hadi Juni 26 ilifanyika pia katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Morogoro ambapo watuhumiwa wengine walikamatwa huko.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema waliokamatwa ni watuhumiwa waliokuwa wakijifanya wakuu wa shule, waganga wa kienyeji, ndugu wa waathirika, wahudumu wa makampuni ya simu au mawakala wa Freemason.

Amesema watuhumiwa hao huwatumia watu ujumbe mbalimbali kupitia namba tofauti za simu na kujifanya wanania ya kusaidia watu badala yake huishia kuwaibia.

Miongoni mwa waliokamatwa ni Julius Simon Mwabula (20) ambaye ni mkazi wa Ifakara Morogoro sambamba na wenzake 22.

Watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo wanavitumia kufanya uhalifu huo ikiwemo hivyo ni kama Kompyuta mpakato 2, kompyuta ya mezani 1, simu za aina tofauti 28, flash 2, modem ya mitandao yote na kadi za simu za mitandao mbalimbali zaidi ya 50.

Katika operesheni hiyo wamekamatwa pia wanawake wawili kwa kosa la kufanya biashara ya ngono mtandaoni na kusambaza picha za utupu kwenye mitandao ya kijamii.

Chanzo: Mwananchi
 
Watoto wa ifakara muhola..hahaaaaa ..ifakara ndio inaongoza kwa scamming na fraud za namna hii tz nzima....
 
Bado waganga feki wanaoweka matangazo yenye namba kwenye nguzo za simu
 
Serikali ibadili sheria faini iwe kubwa na kifungo kiwe miaka 5
 
Nachukia mno kwa suspect(s)kutangazwa majina yao kabla hawajasimama mahakamani, elewa kuwa suspect ana haki zote hadi hapo atakapotiwa hatiani,huyo kijana wa kihehe yes anaweza kuwa na case ya kujibu, ila hao wadada
Hawajatenda kosa lolote hapa
 
Duh ilibaki kidogo nimle asha zungu mtoto ana ta.ko murua yule,
 
TCRA watuambie. Inakuaje mtu mmoja anamiliki line 50 za simu?
line zote hizo majina tofauti na kuna wengine hata hawajui kama nida zao zimesajilia line ya simu unakuja kustuka tu pila nje una kesi ya mauaji kupitia simu yako wakati hata hyo no huijui
 
Hao vijana wa ifakara ni wadogo sana , afu wanatembea kwa makundi wanajiita halo halo mwaka juzi nilipishana nao ifakara, walikuwa wako wazi sana sijui kwann mamlaka imechelewa kuwakamata
 
line zote hizo majina tofauti na kuna wengine hata hawajui kama nida zao zimesajilia line ya simu unakuja kustuka tu pila nje una kesi ya mauaji kupitia simu yako wakati hata hyo no huijui
Mtandao wa TIGO ndio unaoingiliwa zaidi na hawa matapeli. Sijajua kwanini.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Timu Maalum ya Kuzuia na Kupambana na Uhalifu wa Mtandaoni, huku ikiwashirikisha Polisi Mkoa wa Morogoro, wamefanya Operesheni maalum kuanzia tarehe 18/05/2022 hadi 26/06/2022 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Morogoro na kufanikiwa kuwakamata Julius Simon Mwabula @ Kibegi, miaka 20, Mhehe, mkazi wa Ifakara Morogoro na wenzake ishirini na mbili (22) kwa tuhuma za kufanya uhalifu kwa njia ya mtandao.

Watuhumiwa hao wamekuwa wakijifanya wao ni Wakuu wa shule, Waganga wa kienyeji, Ndugu wa wahanga, Wahudumu wa makampuni ya simu (customer care) au mawakala wa Freemason, ambapo huwatumia watu ujumbe mbalimbali kupitia namba tofauti za simu na kujifanya wanania ya kusaidia watu badala yake huishia kuwaibia ( kuwatapeli).

MFANO WA UJUMBE NI
"Halo ndugu mzazi mwanao shuleni amepatwa na matatizo na anaumwa sana hivyo tuma pesa haraka ili nimpeleke hospitali” na muhalifu huyo anatoa namba ya kutuma hiyo pesa na ukituma unakuwa umeibiwa.

Watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo wanavitumia kufanya uhalifu huo, vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:
  • Kompyuta mpakato (laptop) 2,
  • Kompyuta ya mezani (desk top) 1,
  • Simu za aina tofauti 28,
  • Flash 2,
  • Modem ya mitandao yote 1,
  • Kadi za simu za mitandao mbalimbali zaidi ya 50
Katika Oparesheni hiyo, watuhumiwa wengine wa makosa ya mtandao pia walikamatwa, ambao ni: Marry Samson Sibora @ ASHA ZUNGU miaka 23, Mzanaki, mkazi wa Sinza Mugabe na Zainabu Yahaya Omary @ official Manka , miaka 23, Mrangi, mkazi wa Buguruni Wanatuhumiwa kwa makosa ya usambazaji wa picha za ngono na kuuza mwili kwa njia ya Mtandao ya kijamii ikiwemo facebook, WhatsApp, Tinder na Exotic tz .

Watuhumiwa wote wamehojiwa kwa kina na taratibu za kisheria zinakamilishwa ili wafikishwe Mahakani haraka iwezekanavyo.

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka zingine za kishria, linatoa onyo kali kwa watu wanao jihusisha na uhalifu kwa njia ya mtandao na njia nyingine, kuwa Serikali na vyombo vyake imejipanga kupambana na uhalifu wa aina yoyote, na wahalifu popote walipo watafuatwa, kukamatwa na kupelekwa Mahakamani.

Aidha, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Watanzania wote kutumia mitandao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na kuwa waangalifu na vitendo vya utapeli, ikiwemo kuchukuwa tahadhari wakati wa kutuma pesa au kufanya biashara katika mitandao ili kuepuka kutapeliwa, pia watu wajiepushe kufanya biashara haramu mitandaoni kama vile za kuuza mili na ngono.

Muliro J. MULIRO– ACP
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.
Advertisement Bure Bure 🤣🤣
 
Back
Top Bottom